ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Harakati za kugomea huduma za simu zinazofanywa na mkazi wa Marekani anayejitambulisha kwa jina la kujificha kama Mzee Mwanakijiji UMEFELI.
Kilichosababisha kufeli kwa mgomo huu ni kukosa tija.
Mwanaharakati huyo ambaye pia ni kinara wa kuitengenezea Tanzania maadui duniani alitamani kuona watanzania wanazima simu zao na kukosa huduma hiyo muhimu wakati yeye akiendelea kupata huduma zake bila matatizo.
Ikumbukwe kuwa mgomo huo umeitishwa siku za kazi ambazo wanafunzi watakuwa shuleni. Hii ni kumaanisha kuwa Mwanakijiji anahamasisha wazazi wazime simu na kutojali iwapo kutatokea habari ya dharura toka shuleni kuhusu watoto wao!!!
Tabia hii ya Mwanakijiji ambaye ni mwanaharakati wa Chadema inafanana na kitendo alichokifanya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dr. Wilbroad Slaa Iringa ambapo alihamasisha vijana kukaidi amri halali ya Polisi na yeye mwenyewe akaitii amri hiyo na kujifungia hotelini. Uchochezi huu wa Dr. Slaa ulisababisha kifo cha mwandishi Mwangosi. Kila anapoulizwa kwanini hakuwepo eneo la tukio wakati yeye ndiye aliyeitisha maandamano Dr. Slaa amekuwa akipepesapepesa macho kwa aibu.
Bado haijafahamika kwanini Mwanakijiji amekuwa mchochezi wa vurugu nchini Tanzania ilhali yeye mwenyewe hataki hata kutembelea nchi hiyo ambayo kuna taarifa ambazo bado hazithibitishwa kuwa uraia wake ameshaubwaga.
Miongoni mwa vurugu alizochochea Mwanakijiji ni pamoja na :
kuhamasisha walimu wasifundishe wanafunzi
Kuhamasisha madaktari wasitibie wagonjwa
Kuhamasisha watu wasilipe kodi
Kumchochea Kadinali Pengo aanzishe vita
Kuhamasisha watanzania kususia mchakato wa Katiba Mpya
Kuhamasishwa wananchi waikataze serikali kununua mitambo ya kuzalisha umeme
Kusambaza habari za uongo juu ya Rais wa Nchi
Kuhamasisha chama cha siasa kuanzisha kikundi cha vurugu
Kuhamasisha watu waukatae Muungano
Kuhamasisha wananchi wakatae kushiriki shughuli za maendeleo.
Ni bayana kuwa mwanya wa kodi mpya ya simu unatumiwa na wenzetu hawa wasioitakia mema nchi yetu ili kutuchonganisha na kutusahaulisha jukumu letu kuu la kuijenga nchi yetu. Kwa bahati mbaya pamoja na kwamba Tanzania ni nchi yetu sote, lakini wapo wenzetu wanaofurahi kuona nchi inakuwa kwenye matatizo na migogoro!
Kufeli kwa mgomo huu ni ujumbe muhimu kwa wachochezi wa vurugu. Watanzania wameshatambua kuwa wachochezi hawa hawana malengo mema.
Kuhusu kodi ya simu, nchi yetu ina mfumo wa uwakilishi kwa njia ya Bunge. Tutumie mfumo huu kutoa mapendekezo yetu ya jinsi tunavyotaka kodi zetu zilipwe. Mfumo umewekwa ili tuishi kama jamii iliyostaarabika inayopanga mambo yake kwa utaratibu maalum. Tuendelee kukataa hawa wanaoibuka na kutufanya tuvutane katika vitu ambavyo tumeshaweka utaratibu wa kuvishughulikia.
Hongereni watanzania kwa kukataa uchochezi...
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania...