Mgomo wa madaktari

mnapogoma ni sawa na kuuwa kwa Muda maana watu wakikosa matibabu watakufa huyo mmoja mnaemuacha wa emergency hatoshi......................... ila yote kwa yote nawaunga mkono kwenye kudai haki zenu

shuleni tulifundishwa we should never turn our backs to those whom we consider as emergency cases hila serikali isipo acha kiburi hata hao wa emergency tutawatoa...shukran kwa support
 
Sasa mimi niko njiani kuonana na dr wangu pale MOI ni-aje? Da! Lakin poa tu, dktr wangu anapuuzwa!?, nitamsubiri akisikilizwa atanihudumia vizur!
 
Unanikumbusha mgomo ulee, Mh Mwinyi alipoacha kusikiliza M.DR akaenda kucheza kwasa kwasa na Kanda Bongo Man! Sijui ilikuwa uwanja wa taifa ule? Jamani viongozi wetu, yani wote wanafanana, sijui ni hewa wanayopumua au ni maji wanayokunywa inawafanya wafanane hv?
 

Ndugu MAT imewekwa pembeni kidogo kwa manufaa yake kwa sababu tupo mbioni kukiupgrade kuwa trade union.
Waliobaki mnh ni wale tuliowaweka kama emergeny team.
Mikoani ndo wanajimobilise.
Viombo vya habari vingine vinapotosha na kutoupa umuhimu suala hili.
Mimi mzazi wangu alinilea kuamini i should always do my best kwenye kile ninachokiamini na hata nikifeli lakini nilijaribu kuleta mabadiliko kuliko kukaa chini na kukubali kuonewa halafu nilalamike chini kwa chini......carpe diem as the latin would say
 
shuleni tulifundishwa we should never turn our backs to those whom we consider as emergency cases hila serikali isipo acha kiburi hata hao wa emergency tutawatoa...shukran kwa support

acheni tufe tu ila na nyinyi mtatukuta kwenye anga zetu, tumeenda shule pia na tuna miiko ya kazi na tunanyaswa kama nyie tunavumilia tu maisha yaende, acha tufe tufiwe na ndugu zetu ila kuna watakaobaki watakumbuka madhara ya mgomo wenu wa mwaka 2012!! ninyi ni watu wazima na wasomi mnajua kabisa at the end of the day serikali ita give in na kulipa hayo madai yenu lakini watu wengi watapoteza maisha wakiwemo ndugu zenu maana kuna vitu kama ajali havichagui, sasa hivi mkitoka hapo Russian culture kwenda home mmoja wenu anaweza pata ajali matokeo ya mgomo wenu yatawarudia!! remmember it will always come back to you!
 
mkuu kamshauri blandina kuhusu madhara ya mgomo kwani alikuwa na muda na uwezo wa kuepusha hili.
 

Unajua na siye tunauchungu kama wahanga wa huduma mbovu ya afya...nina wenzangu watatu wamepoteza watoto wao mnh kwa upuuzi kama hamna ors,hamna gloves za kufanya procedure,gauze zimeisha so tunakijua tunachokidai ndugu.ndugu point yako ya kuendelea kunyanyaswa ndo inawapa kiburi viongozi wetu mpaka wanajiona miungu watu.am sure sekta zote zingedai haki zao wasingetunyanyasa hivi.tumepandishiwa bei ya umeme,tumekaa kimya,vyakula vimepanda bei,kimya,sukari imepanda bei hata mwalimu akifufuka atashangaa
 
mkuu kamshauri blandina kuhusu madhara ya mgomo kwani alikuwa na muda na uwezo wa kuepusha hili.

Exactly mkuu...tusingefika huku kaka.
Wanajf wanajua maana ya jina lako?wanajua ni wangapi tunawapata,be it bacterial,viral or fungal na tunashindwa kuwahudumia vizuri kisa sindano za lumbar puncture hatuna
 
hii serikali baila migomo haiendi,naomba hawa wakuu waumwe then wakose watu wa kuwatibu,ndipo watakuwa na adabu
 
hii serikali baila migomo haiendi,naomba hawa wakuu waumwe then wakose watu wa kuwatibu,ndipo watakuwa na adabu

Thanks for your support.Ndugu yangu watajuaje kama kila wakiumwa wanaenda kutibiwa nje?mtu anaumwa kitu ambacho hapa tanzania kinatibika halafu serikali inampeleka nje,unajua hiyo hela tungeweza kuitumia kuboresha huduma za afya....watanzania tutaamka lini?kwanini tumekuwa vilaza kiasi hiki???
 

Waacheni wanapolitics waule wamesotea sana kwa wachawi. Wakivua suti zao utakimbia chale na hirizi walizojipamba, ni maprofessional wale!
 
Waacheni wanapolitics waule wamesotea sana kwa wachawi. Wakivua suti zao utakimbia chale na hirizi walizojipamba, ni maprofessional wale!

dah! kumbe ndo maana maamuzi yao ni km ya waganga wa kienyeji?
 
ndugu tumeshaanza....yaani wangetuma hata mwakilishi akatusikiliza siku ya kwanza tusingfika huku


Dr, mimi naomba kupata ufafanuzi kidogo kuhusiana na mgomo wenu. Nimekuwa nikitaka kutoa maoni yangu katika mjadala huu lakini nashindwa kwa kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusiana na kiini cha mgomo huu. Serikali inasema hivi, vyombo vya habari vyombo vya habari vinasema vile na wanasiasa wanasema hivyo. Naamini wewe ukiwa mhusika wa mgomo utakuwa na taarifa za kuaminika zaidi ambazo zinaweza kupambanishwa na taarifa za serikali kupitia Waziri Mkuu hatimaye tukapata picha kamili na kuwa na meno ya kuweza kuchangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…