Mgomo wa Madaktari: Wagonjwa Muhimbili warudishwa makwao

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Ikiwa bado baadhi ya vyombo vya habari vye serikali vikizidi kuficha hali halisi ya mambo Mgomo wa madaktari jijini Dar es Salaam umeanza kushika kasi ambapo katika baadhi ya hospitali ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wagonjwa walikosa huduma na kuishia kutangaziwa warejee nyumbani hadi watakapopata taarifa kuwa mgomo huo umeisha.

mgomo huo umeshika kasi zaidi Muhimbili na Hospitali ya Amana ambako baadhi ya vitengo vya huduma za afya vilifungwa ili kuongeza nguvu ya madaktari katika vitengo vya dharura.

Katika Hospitali ya Muhimbili wagonjwa wamezagaa na kujazana hasa katika Kitengo cha Mifupa (MOI) huku wengine wakiwa wamekata tamaa ya kupatiwa huduma.

Katika maeneo ya wodi za hospitali hiyo, hali ilikuwa mbaya kwa kuwa wagonjwa walilalamika kutopata huduma yoyote ya matibabu zaidi ya madaktari na wauguzi kuwapitia na kuwaulizia hali tu huku wauguzi wengine wakitoa lugha za kashfa.

Mmoja wa maofisa wakuu hospitalini hapo aliyekataa jina lake kutajwa gazetini kwa kuwa si msemaji, alilihakikishia gazeti hili kuwa mgomo wa madaktari upo kwa kuwa madaktari wengi wa hospitali hiyo jana hawakufika kazini na kusababisha baadhi ya vitengo kufungwa.

Source: HABARILEO


 
"serikali sikivu" kauli hii huwa siielewi kabisa "madkatari kwa kufanya hivyo hakuna mtakacho poteza isipokuwa ni minyororo mliyofungwa na serikali yenu sikivu" polen sana wagonjwa
 
Back
Top Bottom