Mgomo wa madaktari Kenya si wa mchezo mchezo!!

Mnyerede

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
210
230
Mgomo wa madaktari wakidai kuongezwa
mishahara waathiri maisha ya wagonjwa
Wagonjwa katika hospitali za umma
wanaathirika vikali kutokana na mgomo wa
madaktari ulianzishwa kwa niaba ya
kuomba mishahara yao iongezwe na
serikali.
Wagonjwa kadhaa wameripotiwa kufariki
kutoka na mgomo wa madaktari ulianzishwa
Desemba mwaka 2016 wakidai kuongezwa
mishahara yao.
Mgomo huo uliotolewa wito na madaktari
umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya afya
nchini Kenya.
Wagonjwa wamekuwa mahospitali bila ya
kupewa matibabu tangu kuanzishwa kwa
mgono mwezi Desemba.
Madakatari 7 walikamatwa na kufungwa
kwa kutoa wito wa maandamano hayo
Desemba mwaka 2016.
 
Tuweke masihara pembeni hawa watani wetu wanajua kuidai haki yao. Kenya kila nikienda kutembea naona wanapiga hatua kwa haraka sana. Sisi tupo wakimya, wapole, mabwege, wapumbavu na malofa kabisa. Tunaogopa kuidai haki yetu sababu,Kila daktari anaogopa kumfika kama yale ya Ulimboko.

Ndukiiiii
 
Woga ni dhambi kuu kuliko zote. Ni ngumu kutubia dhambi ya woga sababu ni kama dhambi uongo. Kuogopa ni kujiaminisha kuwa huna viwango vya kusimamia unachoamini; na kwamba umejiaminisha kuwa maisha yako mikononi mwa mwanadamu mwingine. Mwanadamu huyo ambaye pia amezaliwa na mwanamuke ana utisho sababu tu ya ridhaa aliyopewa na mfumo wa utawala, na hajui kuwa cheo ni dhamana tu. Ukishajiambia uongo na ukaamini, utauishi uongo. Woga unatokana na uongo tunaojiambia. Woga ni dhambi isipokuwa tu pale mtu anapoogopa kutenda dhambi au kufanya udhalimu wowote dhidi ya mwingine.

Madakitari wetu hawawezi kuwa na ujasiri wa wakenya sababu ya makuzi ambayo yamewafanya waamini kuwa hawawezi kudai haki bila kuwa victimized.
 
Tuweke masihara pembeni hawa watani wetu wanajua kuidai haki yao. Kenya kila nikienda kutembea naona wanapiga hatua kwa haraka sana. Sisi tupo wakimya, wapole, mabwege, wapumbavu na malofa kabisa. Tunaogopa kuidai haki yetu sababu,Kila daktari anaogopa kumfika kama yale ya Ulimboko.

Ndukiiiii
Malofa wapo Ufipa Sawa!!
 
Hakuna serikali yoyote yenye akili ingeruhusu mgomo wa madaktari hadi kwa miezi mitatu, hii sio demokrasia ni ujinga wa kiwango cha juu kabisa.
 
Tatizo ni kwamba ukiwaongezea madaktari, kesho watakuja walimu utawaongezea, watakuja zimamoto utawaongezea na wengine na wengine.

Kufikia hapo nchi itakua ina mzunguko mkubwa wa pesa ambao utasababisha bei za bidhaa kupanda na mahitaji kuongezeka, baada ya muda kuna kundi litaingia tena mtaani baada ya bidhaa kua hazishikiki kwa mshahara walioutaka mwanzo litaongezewa.

Chain itakua hiyo mpaka kujikuta mnaishi na inflation na uchumi kucollapse.
 
Hakuna serikali yoyote yenye akili ingeruhusu mgomo wa madaktari hadi kwa miezi mitatu, hii sio demokrasia ni ujinga wa kiwango cha juu kabisa.
Ikiwa muajiri wako hataki kukupa haki yako ya nyongeza, na ushaidai kwa njia ya upole. Utafanya nini ikiwa hataki kukupa?
 
Tuweke masihara pembeni hawa watani wetu wanajua kuidai haki yao. Kenya kila nikienda kutembea naona wanapiga hatua kwa haraka sana. Sisi tupo wakimya, wapole, mabwege, wapumbavu na malofa kabisa. Tunaogopa kuidai haki yetu sababu,Kila daktari anaogopa kumfika kama yale ya Ulimboko.

Ndukiiiii
:D:D
 
Back
Top Bottom