Mgomo wa madaktari in a Human face!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari in a Human face!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by safariwafungo, Feb 3, 2012.

 1. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pamoja na changamoto nyingi zinazolikabili taifa letu nadhani namna tunavyoshungurikia stakihiki za madaktari si njema sana kwa maslai na ustawi wa Taifa na si dhani kwamba migomo inayoendelea kwa upande wa madaktari kwamba ndio suluhicho na si dhani kama anayedhurika ni serikali la hasha anayedhurika ni mama yangu aliyepo kakonko kigoma vijijini ambapo kupata usafiri kwenda walau kwenye hizo hospitali binafsi ina mgharimu takribani zaidi ya masaa 72 sasa sielewi kama atakuwa bado yupo katika hali ya kuridhisha.

  Na chelea kufikiria namna gani dada zetu na mama zetu wanavyoteseka ktk kujifungua na leo hii tunadiriki kutumia siraha ya uweledi wetu kuwasurubu watanzania, ni ngumu kidogo kuingia akili. Sikatai kwamba madaktari wana matakwa sahihi kabisa kama ilivyo mimi, yule kwenye vyombo vyetu vya usalama, walimu na kadharika sasa mimi nadhani ni vyema tukakaa pamoja tukaona ni namna gani tunaweza kutatua changamoto anuai zinazo tukabili.

  Adhabu tunayowapatia watanzania ni kubwa sana nadhani hawastahili hata kidogo, shime watanzania wenzangu tujaribu kuwa sehemu muhimu ya kutafuta suluhisho ktk jamii zetu badala ya kuendelea kuwa watazamaji ama washabiki. Mwenyezi mungu atuwekee wepesi katika kutatua changamoto zetu!

   
Loading...