Mgomo wa madakta unatufundisha nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madakta unatufundisha nini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by step, Jan 29, 2012.

 1. s

  step Senior Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka haya maneno ya EL "Fanyeni maamuzi, ni bora kuamua kuliko kutoamua" ukitafakari vizuri mgomo huu usingetufikisha pabaya kama ilivyo sasa. Viongozi wa serikali ndiyo hasa wakulaumiwa kwa lack of seriousness.
  - Kejeli
  - Majibu mepesi mepesi kwa maswali magumu
  - Kuweka mikakati ya kuwadanganya wananchi kama kawaida kwa kila tatizo.
  - Kukwepa maswali kama sungura
  - kutokuwa na ubunifu, kujiamini na ujasiri katika kazi ( hili nalo pia lina kwenda mbele sana na upeo wa uelewa wa viongozi wenyewe).
  - Kubwa zaidi ni lack of leadership skills kila tatizo hata la kitaalamu kujibiwa kisiasa tuu, angalia umeme, umaskini baada ya miaka 50 na sasa afya.

  Wananchi inatupasa kuelewa kiini cha matatizo ya wenzetu madaktari na watumishi wa afya kuwa hayawezi kujibiwa kisiasa tuu, viongozi wanapaswa kufanya maamuzi na kuvua uanasiasa kwa kila tatizo tulilonalo. viongozi wasio wabunifu, na wasiojiamini hawatatuvusha popote tutabaki hivi hivi hata miaka mingine 50 ijayo. Malengo ya millenia ampayo wao walishiriki katika kuyaweka na sasa wameyasahau hayatabadilika kama ile misemo tuliyoizoea hakuna siasa hapa we have to be serious.
   
 2. H

  Hussein Mustafa Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ilikuwa na ombwe la uongozi makosa tuliyofanya ni kuchagua msimamizi ndio kinachotutesa leo mpaka miaka minne ijayo!
   
Loading...