CCM yatoa maelekezo sakata la mgomo wafanyabiashara Kariakoo, Katiba Mpya

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,616
21,014
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Jumapili Mei 21, 2023 imeingiza mguu katika sakata la mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo huku ikiitaka Serikali kutafuta kiini cha tatizo na kukitafutia ufumbuzi.

Kamati hiyo imetoa maelekezo hayo katika kikao chake maalum kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea na kujadili taarifa kuhusu mgogoro wa wafanyabiashara wa soko hilo la kimataifa.

“Kamati Kuu baada ya kujadili imeielekeza Serikali kufanya uchambuzi wa kina wa masuala yaliyoibuliwa na kulalamikiwa na wafanyabiashara wa Kariakoo ili kutafuta kiini cha tatizo halisi na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu,”imesema taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi,

Vilevile, Kamati Kuu imeielekeza Serikali kuhakikisha inatengeneza utaratibu wa kutatua changamoto mapema kabla hazijaleta madhara katika jamii kama ilivyokuwa katika mgogoro wa soko la Kariakoo.

Kamati Kuu imetoa maelekezo hayo kwa Serikali ikiwa ni siku nne zipite tangu wafanyabiashara wa soko la Kariakoo wamalize mgomo wao ambao ulifanyika kwa siku tatu mfululizo kwa kufunga maduka yao kushinikiza kutolewa kwa kodi ya stoo na kukomeshwa kwa kile walichokiita kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Hata hivyo, mgomo huo ulitamatika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya vikao viwili na wafanyabiashara hao huku kikao cha kwanza kilichofanyika Mei 15, 2023 kisifue dafu na baadhi ya wafanyabiashara waliendelea na mgomo hivyo kulazimika tena Mei 17, 2023 kufanya kikao kingine cha wazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Katika kikao cha pili kilichohudhuriwa na mamia ya wafanyabiashara wa soko hilo maarufu nchini lenye kila aina ya pilikapilika kilifanikisha kumaliza mgogoro huo baada ya Majaliwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji kuwasikiliza wafanyabiashara hao wakitema nyongo kuhusu kero zinazowasibu na baadaye kuunda kamati ya watu 14 kushughulikia matatizo hayo ikiwahusisha wafanyabiashara na watumishi wa Serikali.

Kwa upande mwingine, Kamati Kuu imempongeza Rais Samia kwa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya na kukamilisha ujenzi wa Ikulu Mpya ya Chamwino iliyozinduliwa rasmi Jumamosi Mei 20, 2023.
 
CCM huwa inawadanganya na kuwa tapeli wananchi:

Kamati kuu wajumbe ni Wale Wale walioko kwenye serikali sasa kamati kuu inaiagiza serikali ipi !!!

Mfano Waziri mkuu, makamu wa Rais na Rais wote ni viongozi wa kiserikali na ni members wa Kamati kuu sasa ni ccm ipi inaiagiza serikali ifanye wakati ni hao hao wanaoshindwa kufanya au kutekeleza wakigeuka upande wa pili wanajiagiza tena wanasema chama kimesema?

Mfano, Tulia Akson ni spika wa bunge, wakati huo huo ni mjumbe wa Kamati kuu ya ccm Taifa, ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm Taifa, mkoa,wilaya, ni mjumbe wa kamati Za siasa kata, wilaya,mkoa, Taifa Ana vyeo 42.

Ushauri : viongozi wa kamati kuu wasiwe viongozi wa serikali na viongozi wa serikali wasiwe wajumbe wa kamati kuu.
 
CCM huwa inawadanganya na kuwa tapeli wananchi:

Kamati kuu wajumbe ni Wale Wale walioko kwenye serikali sasa kamati kuu inaiagiza serikali ipi !!!

Mfano Waziri mkuu, makamu wa Rais na Rais wote ni viongozi wa kiserikali na ni members wa Kamati kuu sasa ni ccm ipi inaiagiza serikali ifanye wakati ni hao hao wanaoshindwa kufanya au kutekeleza wakigeuka upande wa pili wanajiagiza tena wanasema chama kimesema?

Ushauri : viongozi wa kamati kuu wasiwe viongozi wa serikali na viongozi wa serikali wasiwe wajumbe wa kamati kuu.
Acha wengine tuwe wazito wa kuelewa kwa kweli!
 
Kwa mantiki hiyo, viongozi walioko ccm ngazi ya juu , wakigeuka upande wa pili wana kuwa viongozi wa ngazi ya juu wa serikali.

Ngazi ya mkoa, wilaya, Kata, vijiji viongozi wa ngazi ya juu wa ccm wakigeuka upande wa pili ni viongozi wa ccm kinyume na viongozi wa ccm ngazi ya juu.

Madhara yake, iwapo ccm ngazi ya juu wanakuwa na viongozi dhaifu automatically serikali viongozi wa juu wana kuwa dhaifu na kinyume chake.

Nilichokielezea hapo juu ukija ukichanganya na muundo wa Muungano + CCM ambayo haieleweke Hata wenye Phd original wanafeli kuiongoza nchi.

Hapa ccm inachanganya waliosoma akili. Muundo huu ni hatari sana iwapo itatokea ccm ikawa KANU .
 
“Kamati Kuu baada ya kujadili imeielekeza Serikali kufanya uchambuzi wa kina wa masuala yaliyoibuliwa na kulalamikiwa na wafanyabiashara wa Kariakoo ili kutafuta kiini cha tatizo halisi na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu,
Ikichunguzwa sana kiini cha tatizo ni CCM🐒

"Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu,

kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu,

Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua?

Zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua ?
"
 
CCM huwa inawadanganya na kuwa tapeli wananchi:

Kamati kuu wajumbe ni Wale Wale walioko kwenye serikali sasa kamati kuu inaiagiza serikali ipi !!!

Mfano Waziri mkuu, makamu wa Rais na Rais wote ni viongozi wa kiserikali na ni members wa Kamati kuu sasa ni ccm ipi inaiagiza serikali ifanye wakati ni hao hao wanaoshindwa kufanya au kutekeleza wakigeuka upande wa pili wanajiagiza tena wanasema chama kimesema?

Ushauri : viongozi wa kamati kuu wasiwe viongozi wa serikali na viongozi wa serikali wasiwe wajumbe wa kamati kuu.
Yaani ni matapeli wakubwa wa kisiasa
 
Hii ishu ya katiba kwanini wanapeana wanasiasa kuisimamia? Kwanini isiwe ishu ya wananchi wenyewe wao serikali wakasimamia tu.
 
Ikichunguzwa sana kiini cha tatizo ni CCM🐒

"Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu,

kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu,

Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua?

Zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua ?
"
Mie huwa nikiona kitunguu kinanipa machozi machozi na kitupia kwenye kikaangio cha mafuta moto.

Wakikangwa kaangwa jinsi hii labda ndio watajirekebisha.
 
CCM huwa inawadanganya na kuwa tapeli wananchi:

Kamati kuu wajumbe ni Wale Wale walioko kwenye serikali sasa kamati kuu inaiagiza serikali ipi !!!

Mfano Waziri mkuu, makamu wa Rais na Rais wote ni viongozi wa kiserikali na ni members wa Kamati kuu sasa ni ccm ipi inaiagiza serikali ifanye wakati ni hao hao wanaoshindwa kufanya au kutekeleza wakigeuka upande wa pili wanajiagiza tena wanasema chama kimesema?

Ushauri : viongozi wa kamati kuu wasiwe viongozi wa serikali na viongozi wa serikali wasiwe wajumbe wa kamati kuu.
Ccm kwa utapeli wamekubuhu
Magufuli aliwahi sema Kinana nimemtuma India kutibiwa
 
Ila Hii nchi tunafanyana maboya sana. Eti kamati kuu ya CCM imepongeza mchakato wa katiba mpya, hivi aliyekuwa anapinga ni Nani?
CCM huwa inatengeneza Tatizo inarudi kulitatua wanasema wametatua Kumbe walilileta wenyewe.

Hata hivyo kwa muundo wa ccm kupata katiba mpya ni ndoto kwani katiba mpya itawaondoa madarakani..

Muundo wa ccm wa sasa polisi, Jeshi, TISS, magereza, serikali, wakulima na wafanyabiashara wote ni CCM.
 
Kamati Kuu imeielekeza Serikali kuhakikisha inatengeneza utaratibu wa kutatua changamoto mapema kabla hazijaleta madhara katika jamii kama ilivyokuwa katika mgogoro wa soko la Kariakoo.
Tatizo linalioonekana hapa, na ninavyolisoma, nikuwa, haya madhara yaliyotokea n yametokea Lumumba. Sasa kwaavile limewagusa kwa ukaribu kabisa,ndii wanajifanya wanafanyia kazi manung'uniko au Njaa za mitaani.

Hatahivyo, nastaajabishwa. Kwamba katika karne hii hawana mkakati wa kuangaza na kuchukua hatua stahiki wakati kuna hali kama hiyo?,(mgomo)kwa sababu ilikuwa dhahiri hali hiyo ingetokea na walikuwa na Taarifa mapema.
Walipuuza?
Walifikiri tisha toto😂😂😂😁
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom