Mgomo wa daladala Mwanza leo Machi 11, 2024

Mgomo wa daladala Mwanza leo Machi 11, 2024

Watu wa daladala wakubali tu nyakati zinabadilika. Dunia ipo kasi sana
Ndio Mana hapa mtu akiwa huko juu na biashara anapiga pin kuwa Hakuna mwingine kuingiza huo mzigo nchini anabakia yeye mwenyewe kuwa msambazaji pekee. Ama akipita pale bandarini ushuru huo hausemi. Biashara Ni ushindani . Viwanda vya sukari vinalindwa hakuna sukari ya nje Kama sio ujamaa Ni Nini. Yaani maslahi ya wakubwa yanalindwa. Ila nyumbu Hana thamani anakanaygwa na kuliwa.
 
Halafu daladala nyingi zina uhuni wa ajabu ajabu. Mfano nauli kila mtu ana bei yake, huyu atakuambia 900 yule atakuambia 800.

Jambo la pili kukatisha route. Mfano gari la airport - Nyashishi mida ya jioni wanasema wanaishia mkuyuni. Wakifika mkuyuni wanashusha wanapakiza tena mpaka buhongwa. Wakifika buhongwa wanapakiza mpaka nyashishi.

Mamlaka zipo zinawaangalia. Waache uhuni
Unajua uhuni unaofanyika kwa Kodi kuliwa huko juu ama wewe ndio wale mnaofunga mmama miaka 22 kwa nyama ya swala
 
Unajua uhuni unaofanyika kwa Kodi kuliwa huko juu ama wewe ndio wale mnaofunga mmama miaka 22 kwa nyama ya swala
Unataka kutetea nini?.. Huoni kua inawaumiza wananchi wa kawaida huu uhuni wa kwenye daladala. Yawezekana wana hoja za msingi wasikilizwe ila nao waache uhuni ili watoe fair service mambo yaende. Vinginevyo wawaache wenye bajaji nao watoe ushindani.
 
Jamani kama kero basi leo mwanza kuna kero.inasemekana fununu za mgomo zilijulikana mapema.lakini hakuna kilichosaidia mgomo kuendelea
 
Unataka kutetea nini?.. Huoni kua inawaumiza wananchi wa kawaida huu uhuni wa kwenye daladala. Yawezekana wana hoja za msingi wasikilizwe ila nao waache uhuni ili watoe fair service mambo yaende. Vinginevyo wawaache wenye bajaji nao watoe ushindani.
Sitetei kitu Ila shida iko huko juu kabisa. Watu maalumu pekee ndio wanaoweza kuagiza mafuta toka nje uelewe so anauza Bei anayojisikia. Ina Mana Hana ushindani. Yaani watu bado wako enzi za ujima. Sukari hairusiwi kutoka nje. Yaani huwa nawaza na ninajiuliza kuwa inakuwaje sukari inasafirishwa from Brazil Ila ikifika hapa nchini inauzwa kwa Bei ya chini kuliko ya hapa nyumbani.
Yaani kusafiri umbali wote huo Ila bado inauzwa Bei ya chini.

Wameshikilia dart imewashinda na bado tanesco
 
Yule bingwa Amos makala kila akienda sehemu lazm migomo ianze
 
Kwa jiji la mwanza bado sijaona bajaji za kusumbua,bado ni chache sana
 
Wakuu kuna mgomo wa daladala toka alfajiri ya leo.

Shida nasikia ni mgomo unatokana na bajaji kuingilia route zao.

Hali ni tete na ni mgomo wa njia zote za daladala. Wananchi wanatembea na bajaji , malori na vi kirukuu ndo vinapakiza abiria kwa wingi.
🙄💭
 
Mwanza si mji mkubwa zaidi hapa nchini ukiitoa Dar!? Inakuaje wagombanie Abiria!? Wabadili tu route na wao ama waje Dom tunashida ya usafiri kutoka Chamwino hadi Makole
 
Wakubali tu yaishe..haya haya yalitokea Moshi route ya KCMC ...wa haice wakakubali yaishe ikabid na wao wahamie kweny bajaji route ikafa
 
Back
Top Bottom