Mgomo Wa Daladala Moshi Na Ma-Bus Moshi To Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo Wa Daladala Moshi Na Ma-Bus Moshi To Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Puppy, Jul 9, 2012.

 1. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Kwa Siku Mbili Au Zaidi Daladala za mji wa Moshi zimegoma kufanya kazi ya kusafirisha watu.
  Sababu yao kubwa ni Ushuru mkubwa wanaotozwa kila waingizapo magari Stand kubwa. Mfano daladala zinazo-operate Route ya Rau-Mjini nauli kubwa ni 300 ama 250 kwa abiria, na kila aingi*po gari stand analipa 2000.

  Moshi-Arusha.
  Leo Tarehe 09-07-2012 mabus yanayofanya ka- kubeba abiria Moshi kwenda Arusha na Arusha kwenda Moshi nayo yamegoma, madai yao ni Ushuru,(wanashirikiana kituo na daladala), Pili usmbufu wa Trafics na mengine.
  Katika Habari hiyohiyo leo pale Machine Tools Machame daladala ya Arusha yenye route za Ngulelo Town maarufu kama kipanki imepasuliwa kioo kwa sababu ya kubeba abiria kutoka Arusha kuleta moshi.

  Mgomo umesababisha usumbufu mkubwa kufuatia shule nyingi kufunguliwa leo na wanafunzi kukosa usafiri.


  NIONAVYO:
  Serikali fungueni macho, hawa viongozi wenu wa halmashauri wataharibu Nchi. Yule mkurugenzi wa kumuangalia mara ya pili.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Serikali haina ubunifu wa vyanzo vya mapato zaidi ya ushuru wa stendi
   
 3. m

  mangatara JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 10,055
  Likes Received: 5,642
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu, sii wewe tu umeona athari hii ya mgomo huu. umejaa siasa tupu wala hakuna pa kujificha kuhusu serikali yangu tukufu ya ccm. Hii ni serekali sikivu sana tena nasema sana. Naishukuru kwa sababu ni sikivu, tena inawajali watu wake haswa wale waendao kwa miguu. Nadhani wanadhani ni Chadema wanaandamana ndiyo maana wanakataa kumng'oa huyu mkurugenzi wao mchapakazi sana mama Kinabo. Mwacheni akae ili aweze kuisaidia serekali hii tukufu tena sikivu.
  Mimi sina chama, sina daladala wala bodoboda ila, naishukuru serekali hii sikivu ya ccm kuniwezesha kufanya mazoezi ya kutembea zaidi ya km 10 kila siku sasa. ati ni ili kusudi niwachukie chadema na meya wao.
  Huu ni wendawazimu, huu ni ukichaa. Mwenyekiti wa wasafirishaji wa mkoa huu na AR ni ccm pure bila hata kujificha. Ameamua kutuadhibu sisi masikini kwani ameshachuma vya kutosha hivyo kukosa income ya siku chache tuu, kwake si shida. Ole wako kwani Mungu anasema atasikia kilio cha mnyonge naye atajibu.
  Huenda ukadharau neno hili lakini nakuambia, Watu wa Moshi sii vipofu kama unavyodhani. ccm yako ilishapoteza mwelekeo tangu ilipoanza kuwakumbatia mafisadi kama wewe.
  ccm imeongoza halmashauri yetu hii kwa miaka mingapi lakini hatukuona hata changarawe kule Kwa Mtei mpaka siku 3 kabla ya kampeini ya uchaguzi? Tena sio changarawe bali ni "LIUDONGO" tuu lililobebwa mahali na kuja kuswekwa hapo barabarani kama kiini macho kwa wapiga kura???
  Acheni jamani. Hiyo chadema mnayotaka tuikatae, imeshika uongozi siku ngapi?? Mona tumeona changarawe ya kweli??
  Aksante Mwenyekiti kama utasikia kama serekali yako inavyo sikia.
  Myonge mnyongeni lakini....
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kama ushuru umepangwa na halmashauri ya mji, madiwani hawajapitisha? Kama wamepitisha basi hawawezi kukwepa lawama hizo!
  Kuhusu serikali kuu, nadhani wanatakiwa kutazama upya swala la ushuru wa stand. Maana gari ikitoka Arusha kwenda Moshi, inalipa ushuru Arusha, Tengeru, Bomang'ombe na Moshi. Sasa kama wamepandisha hadi elfu 2, itafika sh elfu nane kwa trip. Ni nauli ya karibu abiria wa 4 kwa trip moja. Ni hela nyingi sana hasa ukizingatia abiria sio wengi na kuna ushindani na mabasi yanayokwenda na kuingia kutoka mikoa ya jirani.
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280


  Kaka huu mgomo kuliko wanavyodhani, Arusha umenukia kidogo tayari, ukiwa ON unategemea ni nini kitafuata?
  Watu wanangoja tu Buttons ziwe pushed waingie Barabarani na kwa mambo yalivyo there will be no goin back.
  1. Waloshindwa kufika shule leo watapewa adhabu, itajenga hasira na chuki kwa wote mwanafunzi na mzazi.
  2. Biashara ngapi zimekwama na ugumu huu wa maisha? Wameshindwa kwenda memorial leo kuchukua mitumba.
  3.Watu wa boma, kibaoni , kingori na kia hawajaenda kazini, acha wa mijini.

  Ushuru huu umelalamikiwa sana lakini wapi, moshi watavurugana kama hawajui, wanadhani wanaizorotesha upinzani lakini ukweli ni wanawapa nguvu sana tu.

  Wanaleana sana
   
 6. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280

  Hapo haujazungumzia Traffic wanachukua ngapi pale Usa-River, KIA, Boma na Pale Karibu na Keep Left Changbay.

  Stand moshi wamegeuza geuza lile banda la ushuru.
  Wale watoza ushuru wamepewa nguvu kubwa sana, ni ubabe na kudhalilishana sana kama wale jamaa wa municipal.

  Hizi siasa za kuchafua upinzani zinawakomaza wananchi na zinawaweka tayari kwa lolote, Tawala hawaoni hili.

  Kwa kifupi nimeumia sana, ilikuwa rahiisi sana kutatua hili
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280

  Na ukiangalia kiundani tatizo sio ushuru tu, bali ubabe wa wakusanyaji ushuru
   
 8. m

  mangatara JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 10,055
  Likes Received: 5,642
  Trophy Points: 280
  nachukia mno ninapo ona kuwa watu wameamua tu kuathiri wengine ili wajione ati wanaongoza tu milele. laiti watu wangejifunza kwa (Matyrants) wengine akina Mubarak. Mbona waliondoka kwa aibu. Hakuna mwenye hati miliki ya Moshi hii. Tutasoteshwa lakini bado ngangari tuuuu
   
Loading...