Mgomo wa daladala jiji la mwanza

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Habari za kuaminika zinasadikisha kuwa leo Jumatatu kutakuwa na mgomo wa Madereva wa hiace (daladala). Chanzo cha mmgomo ni kuwa wamechoshwa na faini zinazotozwa na jeshi la polisi, pamoja na maadili mabovu ya polisi. Polisi wanalaumiwa kuwa huwa wanajificha katika vichochoro vya Nyumba, au vichaka vya miti vilivyoko karibu na barabara kutegezea madereva, na gari inapokaribia hujitokeza haraka na kuanza kufokea madereva kuwa hawakuwa waangalifu kutiii amri ya kusimama iliyotolewa na polisi, madereva niliobahatika kuongea nao wanasewma kosa liko wapi kama askari wa usalama barabarani watasimama mahali pa wazi kuliko kuishi maisha ya kufumaniana na kulazimishana faini zisizo za lazima, mfano dereva kuonekana kuwa amekataa kusimama kuepusha ajali endapo trafiki amejitokeza ghafla na gari ilikuwa katika mwendo......... MNAOHUSIKA HASA RPC UTATUE TATIZO HILO MAPEMA KAMA LITATOKEA KUTOKUATHIRI MAENDELEO YETU YA KIJAMII, KISIASA, KIUCHUMI NA KIUTAMADUNI...............
 
Aah bwana we wacha wagome;!?sasa hivi kada zote zinatakiwa zigome hadi kieleweke; Subiri mgomo mkubwa wa madaktari unakuja kwa nguvu mpya this week.
 
Yani hata kama wana makosa wasikamatwe na trafic? Aaa jamani,migomo mingine feki!
 
Habari za kuaminika zinasadikisha kuwa leo Jumatatu kutakuwa na mgomo wa Madereva wa hiace (daladala). Chanzo cha mmgomo ni kuwa wamechoshwa na faini zinazotozwa na jeshi la polisi, pamoja na maadili mabovu ya polisi. Polisi wanalaumiwa kuwa huwa wanajificha katika vichochoro vya Nyumba, au vichaka vya miti vilivyoko karibu na barabara kutegezea madereva, na gari inapokaribia hujitokeza haraka na kuanza kufokea madereva kuwa hawakuwa waangalifu kutiii amri ya kusimama iliyotolewa na polisi, madereva niliobahatika kuongea nao wanasewma kosa liko wapi kama askari wa usalama barabarani watasimama mahali pa wazi kuliko kuishi maisha ya kufumaniana na kulazimishana faini zisizo za lazima, mfano dereva kuonekana kuwa amekataa kusimama kuepusha ajali endapo trafiki amejitokeza ghafla na gari ilikuwa katika mwendo......... MNAOHUSIKA HASA RPC UTATUE TATIZO HILO MAPEMA KAMA LITATOKEA KUTOKUATHIRI MAENDELEO YETU YA KIJAMII, KISIASA, KIUCHUMI NA KIUTAMADUNI...............
vichaka ndani ya jiji?
 
matrafik wamezidi simnakumbuka sakata la jerry muro?alikua akiwaanika wazi waz itv eze hizo,ndio mtindo wao na wanapata pesa nyingi sana hawa jamaa hawana haja ya mshahara kabisa.wagome tu madreva madocta manes na hata walimu Tanzania hatunaga viongozi wagome 2
 
Hata huko kuna mgomo aya bwana, ila haijahit sana kama ingetokea Bongo ingekuwa kazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom