Mgomo mwingine wa madaktari hautakubalika!


Baki hivyohivyo na maoni yako wala husibadilike na hayo maoni yako ungepeleka wizarani ingekuwa vizuri kwani sie tumejaribu imeshindikana, mgomo wetu upo pale pale hadi hapo JK atakapojua wajibu wake! Hii sio siasa na wala hakuna maandamano.
 

Hata JK,PINDA NA MPONDA WAMESOMESHWA NA KODI ZA BABA ZETU!!!


huna hoja!:biggrin:
 

Nadhani umekosea kidogo. Sidhani dakitari yupo kwa ajili ya kuua wala kusababisha kifo bali kujaribu kuokoa maisha yake..nadhani kitu kingne ni kutowekewa mazingira mazuri ya madaktar kufanya kazi kiujumla bila kusahau maslahi..Hakuna anaependa watu wafe bali tunataka kujengewa mazingira mazur ya kuwahudumia watanzania.
 
Hv Mponda na Nkya wamefanya nn hadi wajiuzuru?

Inaonesha kabisa hii ishu ni ngeni kwako..jiulize kwanza kwa nini Blandina Nyoni na mwenzake walisimamishwa kazi, ukijua hilo nadhani utajua kwa nini na hawa tunataka waondolewe.
 
Hv Mponda na Nkya wamefanya nn hadi wajiuzuru?

Asante sana Negembo. Me naona madaktari wanakua vichaa sasa. Kwani Mponda na Nkya ndio wamekula posho zao? Halafu kinachonishangaza wanampa AMRI Rais eti mpk jumatano awe kashawafukuza kazi. PM kashawaambia kuwa madai yao yako kwny mchakato kulingana na taratibu za serikali ila hawasikii. Me naona km hawataki kazi WAACHE wakalime mahindi, wawaache wenye uzalendo wafanye kazi. Hakuna aliyeshikiwa mtutu wa bunduki.
 


KAKA Umeandika mengi ila sijaona jambo la msigi, lazma ujiulize kwanini wanagoma, je haya hawakuyasema kwenye mkutano na Pindua kuwa watafanya iwapo makubaliano hayatatekelezwa?mbaya ni mkuu wenu na serikali yake!wamekuwa wakiwaignore sana wataalam na kujiona no one else, sasa wakati ndo huo tunasogea taratibu!serikali gani inatumia pesa ya walipa kodi kufanya uchunguzi wa mambo kadha wa kadha lakini yanapuuzwa ili kulinda uovu na urafiki wa kinafiki na usio na tija mbele ya maisha ya watanzania!

huu mgomo nadhani umechelewa
viva madaktari
hii nchi lazima ipelekwe hivohivo!
ukiwa na viongozi kama baba mwanaisha na pindua ni janga la kitaifa!
 

nyie wote ni vipofu, msiwe kama manumba mnakurupuka tu na kupost ishu zenu za kipuuzi
mtu makini anafanya research kwanza then ndo anaweza kuongea!unajua madai ya madaktari ni yapi?hujui hata viongozi wa kisiasa wanakuwa connected vipi kwenye hii ishu unakimbia kupost uliza kwanza kabla ya yote!else these are damn shit!
 
Acha uwe uvivu wakufikiri nadhani hata madaktari furaha yao nikuona masikini tunakufa kwa kukosa huduma, tutafute mbinu zingine tafadhali hata kwakutaka wananchi tuwasaidie kwa maandamano!

Ugumu upo wapi; je, PM Pinda alipowaahidi alitaka kuwafanya watoto wadogo kuwapa ahadi hewa??

Tatizo viongozi wetu wameshazoea kudanganya. Kila siku wanafikiria niwadanganye nini hawa, na waelewe kuwa HATA UONGO HUWA UNAISHA, JE, MANENO YA UNGO YAKIKUISHIA UTADANGANYA NINI TENA?

madr walitumia busara pale walipokubali kuendelea na kazi, na PM aliwaahidi kuwa madai yao yanashughulikiwa, sasa hadi leo hakuna kilichofanyika. TUNATEGEMEA NINI??

ACHENI NISEME HATA MKINI....... ACHENI NISEME KUWA SERIKALI NZIMA IWAJIBIKE KWA KUJIUZULU KAMA WATAWEKA MAZINGIRA YA MGOMO KUFANYIKA TENA NA KUUA WALALAHOI.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
wewe nawe ndio walewale masabuli utilizers!pm si aliahidi kuwafukuza kazi nani kamzuia?we unafikili hii ni fani ya kuuza duka sio!!??kamshauri mta maamuzi awafukuze hata leo halafu wewe na masabuli yako mkatibu mwana..wewe!hahaha eti wazalendo,huyo waziri na mwanzie ndio wanauweza uzalendo kwa kubaki madarkn hata baada ya kubolonga sio!ofcourse ikishindikana inakuja massresigniton ndio utatumia aikli badala ya masabuli.hahaha!
 
Ingawa na mimi naasirika kwa kiasi fulani ila nawaunga madaktari Mkono kwa %zote ukindoa hulka ya Dr mmoja mmoja.Kazi wanazofanya ni kubwa mno tena mno asa kwa hili swala kurinda huai wa mtu anapo kuwa katika operesheni ya aina yoyote ile.Mm bnafs nimeteseka na maumivu ya nyoga kwa muda wa miaka 4 akatoke Dr 1 pale MOI ana cheo kkubwa akanionyesha fadhla zake mpaka sasa naweza kutoka Sehemu moja kwenda nyngne ingawa bado nyonga 1.Alafu useme ma DR awana humuimu lazma ntakuwa na waswas na akl zako.
 
acha uwe uvivu wakufikiri nadhani hata madaktari furaha yao nikuona masikini tunakufa kwa kukosa huduma, tutafute mbinu zingine tafadhali hata kwakutaka wananchi tuwasaidie kwa maandamano!
heshima yako mkuu!naomba unitajie maandamano matatu ambayo yalifanyika hapa nchini na kufanikiwa!?usiwe mtu wa kulalamika bila kufanya kwa vitendo!kwa nini usiandamane leo kuitaka srkl itimize makubaliano maana sasa hivi mgomo haujaanza unangoja nini!!!?hivi mtu kujiuzuru kunachukua mda wa siku nzima!acha propaganda ni wakati wa kutimiza wajibu.una nafasi ya leo na kesho kuwashauri na kushinikiza utekelezwaji wa makubaliano na kumbuka madactari hawako kisiasa na huwezi mlazimisha afanye kazi,ni wajibu wako kujua kama utampisha mtt wako kwenye njia ya mbwa mkali au lah!na ukiamua kumpitisha usijidanganye utawaambia watu ulikuwa unampenda mtt wako wakakuamini.
Si kweli furaha ya madactari ni nikuona masikini wanakufa,ni vyema ungepita msingi wa madai yao halafu ndio uchangie.nakushauri upitie jukwaa la siasa upate walau kwa uchache ndio uje kuchangia hii mada.asante mkuu pamoja sana!
 
kama mnaona maslahi ni kidogo na hamuwezi kuvumilia serikali kutatua matatizo yenu basi ACHENI KAZI! tafuteni kazi kwingineko! nyie si ni kada muhimu zaidi ya wengine? pili wengine wanasema Serikali wanakwenda kutibiwa nje! issue hapa ni competence maana kama mtu ana wasiwasi na uwezo wako hawezi kurisk maisha yake kama uwezo anao! OPERATION YA KICHWA BADALA YA MIGUU NA hiyo inahitaji kuongezwa maslahi? diagnosis ya malaria kwa wengine ni taabu! ni watu wangapi mmewapima wana HIV mkarule out kwamba wanao wakati hawana? au kwa kuwa wananchi tupo kimya hatuwabwatukii kwa madudu mengi mnayoyafanya?! BUT BY THE WAY NYIE NDO MNATOA RECCOMENDATION MGONJWA AENDE NJE AU LAH!  naamini wapo madaktari wachache wazuri lakini wengi tumepoteza pesa za wananchi! NI VILAZA na thats why mnashindwa kuhandle issue ndogo kama hii eti mnampangia RAIS ni mtu gani awaongoze na nani asiwaongoze!! nyie watu wa wapi?! NASEMA MGOMO WENU NI WA KITOTO NA HAUKUBALIKI!
 
kwa jinsi ulivyo kilaza umeyaelezea madai ya msingi ya madaktari bila kujua halafu mwishoni unawapinga tena...madaktari siyo malaika na mara nyingi wanajitolea zaidi ya uwezo wao...kama serikali imeamua kununua utitiri wa mashangingi na kufanya upumbavu mwingi wa kufuja mali za walipa kodi huoni ni sahihi kwa madaktari kuishinikiza serikali kuboresha huduma za afya? huduma duni kama upatikanaji wa dawa na vifaa bora vya kutendea kazi ndiyo vinavyosababisha mengi uliyoyaeleza hapo juu...
bure kabisa kilaza we...!
 
I wish Kagame angepewa hii nchi japo miezi 6 ainyooshe!
 

Mimi naamini tofauti na wewe. Mtoa uhai ni Mungu pekee, na ndiyo huuchukua pia kama alivyopanga. Madaktari wanadai vyao na wapewe. Pia sioni kwa nini hawa ndugu zangu mawaziri wasijitoe wenyewe. Kunani hapo? Kama ni kulaumu then walaumiwe Mponda na mwenzie NKYA.
 

Ukoko wa kisiasa.
 
hakuna haja ya kutoka povu mdomoni mkuu, usihofu kuanzia j5 tutawaachia hospitali zenu sie tutaenda kulima mahindi
 
nendeni zenu! kwanza mnatuhujumu. Matibabu feki harafu mnafanya kazi nusunusu mara mpo hospitali za watu binafsi wakati wa kazi! ni wezi wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…