Mgomo: Dodoma, Ruvuma, Songea, Morogoro, Mwanza, Mbeya wawapokea wafanyabiashara wa Dar

mtanzania mwenye akili tuimamu hawezi kusapoti watu ambao wamezoea kuwahonga maafisa wa TRA na kukwepa kulipa kodi.

mashine hizi ni mkombozi kwa namna moja maana zinaondoa nafasi ya maafisa wa TRA kupokea rushwa na kutoa makadirio ya chini ya kodi.

tuliyoyasikia wakati wa escrow kwa mtu kuuza shea kwa dola milioni ishirini alafu TRA ikaandikwa laki tatu ndiyo hayo wafanyabiashara hawa wanafanya kila siku na watendaji wa tra.

migomo hii inaweza kuwa inasapotiwa na watumishi ndani ya TRA ambao mianya yao inazibwa.

mimi namuuliza raisi wetu maana yeye ndiye mtendaji mkuu, hivi tume ya maadili au takukuru wako wapi unakuta afisa wa tra anayekusanya kodi mshahara wake mdogo lakini tajiri mkubwa.

jamani umasikini sisi nchi za watu wajinga tunajitakia.

asiyetaka kulipa kodi aache biashara,

labda kama ni swala la urasimu hilo tuzungumze ili kuondoa urasimu anayeweza kuagiza mashine aagize
 
Iyo ela ni ndogo sana ukilinganisha na PAYE.
Lipeni kodi acheni kutafuta visingizio.

Mzigo wa kodi VAT unakutafuna wewe pia. Pigana ulipyngizwe PAYE lkn pia pigana upunguziwe VAT. So far hzo kodi zote zinaishia kunufaisha wachache.
 
Kama haufanyi biashara hautakiwi kuchangia kwa kuonyesha shida za PAYE.

Kamahaufanyi biashara funga domo lako. Juzi ni wakulima na wafugaji jana wafanyabiashara na wafuasi wa Cuf. Kwahaya yote yanayotokea ni elimu kwa wapigakura mwezi wakumi hakunatena haja ya kampeni matukio yanayotokea mitaani yanadhirisha kuwa CCM haifayiiiiiiiiiiiii. Ukawa hoyeeeeeeeeeeee
 
Hii sasa inaonyesha kuwa kuna state failure kwasababu viongozi wameamua kuishi kwa upendeleo na kuangalia zaidi maslahi ya wakubwa.

Huu mgomo wa wafanyabishara ni moja ya mapigo ya mwisho kuelekea anguko la Magamba mwaka huu
 
jamani serikali imuachie huyo m/kiti, huku mbeya idadi kubwa ya watu wanapata mahitaji yao hapo sido
 
Baada ya jana kukamatwa kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo jijini Dar es Salaam, Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinaeleza kuwa leo wafanyabiashara Mkoani humo nao wamegoma kushinikiza kuachiliwa na kujua hatima ya kiongozi wao.

Waliopo Dodoma au maeneo mengine lakini mnataarifa hizi tunaomba mtusaidie katika hili.
 
Siku zote hakuna anayependa kulipa kodi, isitarajiwe mfanyabiashara atakubaliana kirahisi kudhibitiwa asiibe kodi anayolipa mlaji wa mwisho.

Kwa maendeleo ya nchi kodi ni muhimu sana. Lazima tubadilike tuenende kisasa, matumizi ya machine ni moja ya hatua nzuri. Wafanyabiashara wengi Tz hawasafiri nje ya mchi, na waende huko waone kama unaweza nunua pipi usipewe risiti ya kisasa. Watz tujenge utamaduni wa kutoa na kupokea risiti.

Mfanyabiashara sio anayelipa kodi, kodi hulipwa na mtumiaji wa mwisho yeye anasaidia kuikusanya. Tatizo anataka akiikusanya iwe ni nyongeza ya faida yake wakati mlipaji anahitaji huduma na maendeleo mbalimbali kutoka kwa serikali yake.

Tatizo nilionalo mimi ni matumizi ya hizo kodi, mabadiliko tunayosisi, tuchague viongozi watakaoweza kuzitendea haki kodi zetu na si watakaotupa vijizawadi wakati wa uchaguzi. Wananchi tusibabaishwe na wachache kwa maslahi yao. Na tukidai risiti kodi itawakilishwa sehemu husika na tutaweza kuibana serikali yetu itutekelezee huduma zetu kwa kodi zetu wenyewe.

Fikiria wewe mfanyakazi unayelipa kodi yako ya mshahara bila hata kuiona zaidi ya kuiona kwenye salary slip, na bidhaa unazokwenda kutumia zina kodi ndani yake anayeichukua imsaidie yeye wakati kwako ni double taxation.

TUBADILIKE TUACHE MIKUMBO.

Jana huyo mwenyekiti alituma ujumbe kwa wenzake kuwa yupo dodoma kwenye kikao kwa mujibu wa ITV. sasa wao wanagoma nn? Au ushakuwa mchezo na utamaduni?
 
Wabunge tusaidieni jamani. Hizi mashine ni biashara ya wakubwa. Mimi niliinunua 1.5m mashine ambayo leo inapatikana kwa chini ya 800k. Mbaya zaidi, kabla tulipewa semina na maofisa wa TRA pamoja na suppliers wa mashine hizo na tukaahidiwa kuwa suppliers wangekuwa wanazifanyia regular service. Tangu 2010 niliponunua mashine hiyo sijamuona mtu wa kuja kuifanyia service, na imenigharimu mara mbili kuipeleka Mwanza toka Musoma niliko kwa vitu vidogo eti software updates, kwanini mfanyabiashara abebeshwe mizigo hii? Tusaidieni wabunge tafadhalini.

tena ni ajabu anaitisha migomo kuhusu hizo mashine ndio mawakala wa tra
 
Iyo ela ni ndogo sana ukilinganisha na PAYE.
Lipeni kodi acheni kutafuta visingizio.
Kodi tunalipa, ninachoongelea hapa ni hizi mashine na gharama zake zisizo na maslahi kwa mfanyabiashara. Jaribu kuutumikisha ubongo wako kufikiri.
 
Mbeya napo wanawaunga mkono wenzao wa Dar, leo wanakutana saa nne asubuhi mkapa hall soko matola
 
Watatuelewa tuuu wamezoea kumnyonya mfanyabiashara kwa njia za ajabu
 
Back
Top Bottom