Mgomo chuo cha Mandela Arusha!

Mgomo chuo cha Mandela Arusha!

nsami

Senior Member
Joined
Jun 11, 2010
Posts
175
Reaction score
8
Wadau.

Nimepata taarifa kuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mandela kilicho Arusha wameandaa mgomo wa kutoingia madarasani kuanzia asubuhi ya leo 4/2/2013. Wakati taarifa hizi zikiendelea kuenea, Makamu mkuu wa chuo hicho prof Mwamila ameomba kuzungumza na wanafunzi wote saa 10 jioni.

Kwa kuwa niko arusha wiki hii, nitafika eneo la tukio asubuhi kujua kama mawasiliano hayo na mkuu wao yanaweza kuathiri mwenendo mzima wa mgomo huo. Pamoja na mambo mengine, wanafunzi hao wanagomea uongozi wa chuo kutoa pesa "kiduchu" kwa wanafunzi wa mwaka wa pili ambao wanaanza tafiti zao (research fund).

Kulingana na "fee structure" ya chuo hicho, wadhamini wanatoa milioni 12.5 kwa ajili ya utafiti kwa wanafunzi wa masters na milioni 37.5 kwa ajili ya wanafunzi wanaofanya PhD. Mtoa habari hizi kanidokeza kuwa kuna watu wanafanya PhD lakini wamepewa pesa chini ya milioni kwa ajili ya research zao. Aibu!

Hata hivyo mtoa taarifa alishindwa kubainisha kuwa ni mgomo wa muda gani (duration).

Nawasilisha!

Source: Nimezungumza na wanafunzi wa Mandela.
 
Yani hiki chuo ambacho bado kinatambaa hata kutembea hakijaweza watu washaanza kukifisadi? Kweli hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Sasa hii hasara kugoma kuingia klasi wanajiharibia wenyewe afadhali wachukue hatua ,hutoingia darasani utafeli unarudi mbwinde huko.
 

Attachments

  • monkey1.jpg
    monkey1.jpg
    1.7 KB · Views: 895
Mgomo ni extreme justice aproach way!
 
Yani hiki chuo ambacho bado kinatambaa hata kutembea hakijaweza watu washaanza kukifisadi? Kweli hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo

Wabongo hata ukiwakabidhi marekani ya leo, miaka ishirini ijayo inageuka kuwa Tanzania tena of Manzese type!
Swali langu ni kuwa hao ma profesa walifanya tafiti zao kwa milioni moja? na kama milioni inatosha kufanya tafiti kwa nini wanaomba zaidi kwa wafadhili? wanataka kujineemesha kwa migongo ya wanafunzi?
 
Mhhh chuo kipya hata kutoa nyilon kwenye viti hawajamaliza tayari migogoro, kweli TZ nuksi kila mahali. Ninawasiwasi sana na mfumo wa elimu yetu hasa MASTERS NA PhD, kwani hizo research inakuwaje wanapitisha research proposal na budget yake alafu kuipata budjet inakuwa issue?. kama walikuwa hawana uwezo wangezikataa mapema.

Fanya siasa katika mambo mengine, lakini elimu na afya haiitaji siasa.
 
pole sana wanafunzi wa mandela
 
Usikute wanagoma kwa sababu hawapati taarifa ya kiafya ya Mandela chezea wabongo wewe
 
Nina wasiwasi kama umekanyaga hata kidato kimoja, itakuwa umeishia la saba wewe ambako hukuweza kugoma. Kama hufahamu hiyo ni njia ya kudai haki.
Sasa hii hasara kugoma kuingia klasi wanajiharibia wenyewe afadhali wachukue hatua ,hutoingia darasani utafeli unarudi mbwinde huko.
 
Mgomo ni moja ya hatua ya kudai haki ikiwa upande mmoja hautaki kufikia muafaka, lakini mgomo ufuate sheria ili kuepesha madhara baada ya mgomo. nawashauri wanachuo wawe na subira kwa kuwa upande wa pili wako tayari kuendelea na mazungumzo na huenda wakaafikiana.
 
Haaaah! Eti Umasikini???????? Tanzania tuwe na subira! Mnataka kunikataa kichwa changu? Hizi ni baadhi ya statements za VC wa Taasisi ya Nelson Mandela akijaribu kuzima mgomo unaoendelea ndani ya kampasi hapa A. town.

Wadau leo nikuwepo hapa hasa baada ya kupata taarifa za tukio hili. Mwanafunzi wa hapa anatakiwa kupewa hela ya utafiti sh. 12.5 milioni kwa Masters na 37.5 milioni kwa PhD.


Umekuwa hivi:
Mwezi wa 11 mwaka jana wanafunzi walipitishiwa proposal zao na bajeti inayokidhi kumaliza mahitaji yake. Baada ya kupitishwa kwa bajeti hizi kukawa na mchakato wa kamati ya Utafiti ambayo ilipitisha hela hizi.

Baada ya kupitishwa ikatokea tatizo hasa nani wa kusimamia hela za utafiti. Supervisor au DVC-Resaerch. Ikawa ni DVC. Sasa nani atanunua mahitaji kama vifaa vya maabara ya kemikali, uongozi ukajipa majukumu yote. Hii ilipingwa na wanafunzi wakiangalia mfumo wa manunuzi ya serikali.

Baada ya hapo, wanafunzi wakaanza kuomba hela. Mfano, ukiomba imprest ya sh. 2.0 milioni unakuta unapewa sh. 1.0milioni. Wanafunzi wakawawanaumia tu.

Kibaya zaidi imekuwa hivi. Wanafunzi wameingia mikataba ya hela ya kujikimu (kila mwezi na utafiti). Baada ya kuanza kutoa cheki za hela wakasema hela ya utafiti inakatwa kwenye hela ya kujikimu. Hivyo, mwanafuzi atakaye fanya utafiti kwa siku zaidi ya 90 hata pata hela tena mapaka anaondoka chuo. Hili ni tatizo.

Wanafunzi wanauliza. Kuna hela ya utafiti na kujikmu na kuna mikataba tofauti, je imekuweje?????

Tatizo ndo hilo wakuu. Na wamesema hawatafanya kazi yoyote mpaka watakapopata ufumbuzi wa tatizo hili.

Mimi ninavyo amini hapa kuna dili za MACCM. Wamepata fedha kwa migongo ya wanafunzi lakini hawataki kuitoa.

THANX GUYZ

 
Mhh... Tanzania! Kwani umelaaniwa? Hiki chuo linapigiwa upatu na vigogo wa nchi hii kila siku (kiongozi yeyote mkubwa huwa anakwenda huko mara kwa mara), bado madudu yanaanikwa hadharani. Juzi juzi nilimwona Raisi akitaka watu wajiunge. Wasomi msikubali kuburuzwa!!! Ikiwa kama tafiti hazotofanyika, nchi itaendeshwa kichawi.
 
Hapo chuoni panasemekana kuna matatizo mengi zaidi ya haya...kuna ukaguzi wa mahesabu umefanyika na Ufisadi mkubwa sanaa kuonekana kufanyika hapo!
Sio wanafunzi tuu, inasemekana hata wafanyakazi wanaweza kugoma mda wowote kutokana na Uongozi mbovu uliopo hapo! kuna profesa anaitwa Prof Dubi, yeye ndio tatizo kubwa linalolalamikiwa kwa wanafunzi na hata wafanyakazi.
 
tatizo ni Serikali dhalimu iliyopo madarakani hakuna ukaguzi maalumu unaofanywa kwani unaweza kukuta wana TEN% hapo hivyo ktoa pesa yote ni kitu kisicho wezekana.Aliye waweka hajui kama aliweka watu na wala siyo malaika ufuatiliaji haupo nawasihi hao maintellectuals wasiogope kudai haki zao.Na Watanzania sasa wasiogope wala kutuhumu kundi linalo goma .TUKIUNGANA TUNAWEZA KWANI NGUVU TUNAZO NIA TUNAYO NA SABABU TUNAZO.
 
Back
Top Bottom