Mgomo baridi Tanzania.

TEGEMEA

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
369
56
Nimegundua kuwa wafanyakazi wa Tanzania wako katika mgomo baridi(hawafanyi kazi ipasavyo).eg.walimu,wauguzi,na idara mbalimbali za serikali.mungu epushia mbali janga hili.Tafakari chukua hatua.
 
watafanyaje kazi wakati wana njaa...mshahara haukidhi mahitaji....mm mwalimu nikipokea mshahara tar 25 mpaka tar 1 sina hata nauli ya kwenda kwa ofisi nashukuru Mkuu anaelewa unaenda siku ukiwa na nauli........angalien tatizo afu ndo tuombe Mungu atunusuru na sio outcomes.
 
Viashiria vyake ni hivi: Aina ya majibu kutoka kwa baadhi ya wauguzi au watumishi katika taasisi za umma mara unapotembelea tasisi hizo kuhitaji huduma, matokeo ya mitihani ya Kitaifa katika ngazi ya shule za Msingi na Upili, wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kufahamu kusoma katika lugha ya Kiswahili achilia mbali lugha ya Mtawala kabla ya uhuru, wanafaulu kwenda sekondari; wakifika sekondari wanaendelea na masomo mpaka kidato cha IV bila kujua kusoma; na walimu hawakutoa taarifa kuwa wameletewa/waliletewa wanafunzi wasiojua kusoma !!!!! Hebu chukua huo mshahara wao linganisha na hali ya maisha ukianza na mahitaji muhimu, halafu angali kama anabaki na pesa ya nauli achilia mbali michango ya harusi !!! Huyu mtu lazima atalazimika kuiba, kama sio mali ya mwajri wake basi ataiba muda wa mwajiri wake.
 
Iliwahi kusemwa; Serikali inajidai kulipa watumishi wake...na watumishi wanajidai kutenda kazi!!!! Mwisho wa siku utaona hakuna lililofanyika. Naililia Tanzania bora wanajeshi wa Mali waje na hapa.
 
Back
Top Bottom