Raia Mwema
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 535
- 79
Namfahamu sana Elisha, atakuwa amejimaliza kwa kufanya hivyo. Alikuwa na mtaji mzuri wa kushinda baada ya NGO yake kufanya vizuri katika masuala ya maendeleo jimboni humo. Kukosa msimamo ni hatari.
.Nilisema hapa CHADEMA wasichukue makapi ya CCM, yatawatokea puani. Watu wakasema ooooh, aaaah.
Sasa mnayaona. Na bora hata huyu karudi CCM kabla ya uchaguzi, kuna wengine watabaki upinzani na kuuhujumu upinzani huu huu bungeni.
Kapata alichokuwa anatafuta,hapa TZ wanaogombea ubunge wanatafuta ngawira na sio kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,ndio maana kwa sisi wengine siasa ni "taaluma ya kihuni''abadani siwezi nikawa mwanasiasa hasa wa pande hii ya TZ
Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema Elisha Nkhambaku amerudi tena CCM baada ya kufatwa na uongozi wa juu wa CCM ukimsihi arudi CCM ambako alijiengua baada ya kushinda kwenye kura za maoni na NEC kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.Elisha ambaye alikuwa amejiunga na Chadema ili kugombea kwenye Jimbo hilo la Singida Magharibi amejitoa Chadema baada ya kupewa million 60 na kuahidiwa u-DC kwenye jimbo jipya...
Source: Zimetoka kwa mtu wakaribu sana ambaye alikuwa ni mmoja ya watu waliomfuata Elisha.
We subiria utakuja kuniambia....Japo kuwa wanaweza kufanya kinyume chake, Kama alivyo fanyiwa na Muhamed Missanga.Hiyo kwenye nyekundu ngoja niiweke kwenye "reminder" ya simu yangu kujua kitakachojiri hapo baadae
Mkuu, Hizo unazo sema wewe ndizo propaganda zenyewe. Unijui sikujui hivyo usidhani unavyo fikiri wewe na wezako ni hivyo hivyo... Swala la mimi kupata hizi habari lisikupe taabu kabisa. hii ni post yangu ya kwanza hapa JF inayohusu maswala ya siasa,source wako ni mtu aliyefuata Elisha na kumpa kiasi hicho cha fedha kisha akatoa siri kwako..... imekaa kama propaganda ya kisiasa vile