Mgombea wa CCM Tarime akataa matokeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea wa CCM Tarime akataa matokeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Oct 13, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Habari zinazotangazwa na TBC1 hivi sasa zinaeleza kuwa mgombea wa ubunge wa CCM huko tarime, Bwana Kangoye amekataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa Ubunge yaliyompa ushindi mgombea wa Chademe, bwana Mwera.
  Anasema hakubaliani na matokeo hayo kwa sababu kuna kasoro nyingi zilizojitokeza katika uchguzi ambazo hazikurekebishwa hadi siku ya upigaji kura.
  Ameitaja moja ya kasoro hiyo ni matokeo kutangazwa bila ya wao kupewa nafasi ya kulinganisha matokeo ambayo wao waliyapata kutoka vituoni na yale yaliyotangazwa na Msimamizi.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mfa maji huyo......
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wanalalamika nini sasa hawa CCM!! wakubali kushindwa tu..
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kubali matokeo na songa mbele na kujiandaa na 2010. CCM ndio chama tawala, kama umeshindwa naamini ni kwa hakika kabisa. Ni ngumu kuamini mtu wa CCM akisema ameonewa.

  Kasoro haziwezi kukosekana katika chaguzi za Tanzania, lakini kwa chama tawala kulalamikia kasoro tena kwa Tanzania naona haiingii kichwani.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  amechanganyikiwa huyo, polisi wao, msimamiwa wa uchaguzi wao, tume ya uchaguzi yao halafu anakataa matokeo! CCM ilishatangaza kwamba itakubali matokeo ya aina yeyote, sasa nini tena?. Huyu hata angepata Ubunge asingewatumikia wananchi bali tumbo lake.

  Kwanza polisi walipaswa wawe wameshamchukua na kumweka ndani kwa kuhusika kwake katika vurugu zilizotokea Tarime. Hata hivyo sheria ipo wazi akate rufaa mahakamani.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Duh huyu fisadi kuna siku atakuja kumkataa hata baba yake.Ukishindwa unakubali siyo kuleta visingizio vya kijinga.Bwana Kangoye inamaana wapiga debe wako Makamba,Msekwa,Tambwe Hiza na Ustadhi Ngeleja hawakuona hizo kasoro. Kama ungeshinda ungeongea hizo pumba au kwasababu umeshindwa unaanza longolongo.
   
 7. m

  mgirima Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani hajui sheria za uchaguzi?

  Msimamizi akishatangaza, hayo ndiyo matokeo halali. Kilichobakia ni yeye J3 awahi Mwanza, Mahakama Kuu, kwa minajili ya kufungua kesi kupinga matokeo!
   
 8. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  anatia aibu sasa huyu...akae kimya tu!!!
   
 9. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Halafu kwa taarifa tu ni kuwa huyu jamaa naye inawezekana KIHIYO. Taarifa tulizonazo ni kuwa amesaini matokeo sasa ngebe za nini. Ajipange aache blabla hapa. Umashuhuri hauji kwa kelele. Hata sisiemu walilielewa hilo. Pia tunataka tukufungulie kesi ya kusababisha kuvunjika kwa AMANI. Kaka mahakama Kuu Mwanza inakuhusu kama uko tayari. Walikupelekea askari wa miavuli lakini haikusaidia kitu.
  To win and to loose is part of game. You have lost brother!!!! Tchao,,, Ha ha haaaaaaaaaaa
   
 10. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,261
  Trophy Points: 280
  Yes ni kweli uchaguzi haukuwa wa haki kama ungekuwa wa haki CHADEMA wangepata 80% CCM 19%
   
 11. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kubali yaishe,Pamoja na dola nzima iliyokuwa TARIME Bado anaona hakukuwa na demokrasia?pole sana
   
 12. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hela alizotoa usiku ule zinamuuma; amesahau kuwa kwanza kwa kutoa hela alifanya kosa/dhambi mbaya kwa watanzania; pia akiwa Mwana-CCM kulalamika ni kashfa nyingine; Amebaki Nape naye aone kuwa si lazima uwe CCM ndio ufanikiwe; Vijana sasa wasimamie rasilimali zao maana wazee waliojaa zaidi CCM wameshindwa kutunza mali zetu za kesho; tushike hatamu sasa kupitie vyama vingine; ndani ya CCM hupati kitu
   
 13. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sio mfa maji, bali ni haki yake.

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi

  Kidumu Chama Tawala
   
 14. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Belo, naona umetoa kali ya mwaka hii.

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi

  Kidumu Chama Tawala
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,679
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  ....haishi kutapatapa :)
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ananikimumbusha gazeti lauhuru limeandika kuwa ccm ilikuwa inaongoza kata 11 kati ya 20, huenda alikuwa najumlisha hizo data za gazeti la uhuru akakuta msimamizi ameshatangaza matokeo mengine.

  pia anakumbuka tshs 600m alizotoa kama alivyodai kuhimiza maendeleo tarime. amesahau kuwa tarime si kama sehemu nyingine za tz

  nimemwona makamba kwenye star tv akiwa mwanza akikiri kushindwa! hawakuwasiliana na kangoye? au baada ya kupata fununu za kushindwa na kuambiwa na jk waondoke tarime haraka, walisambaratika bila kuagana?
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kuna mtu aliwaonya wagombea hapa nadhani ni mwita aliyehamia chadema, kuwa wasichochea vurugu kwa kushawishiwa na wapiga debe wa toka dsm, kangoye amebaki mkiwa tarime, makamba, hiza tambwe na akina msekwa wamelala mbele baadaya kubwaga! hawakuthubutu kulala tarime baada ya kupata fununu za kushindwa, sasa wengine wako mwanza, dsm, sijui mtikila, mbatia na mvungi mko wapi, ila nina uhakika ngawaiya amewasili moshi jioni hii kwa kudandia lifti
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni sawa kabisa! hakuna namna nzuri ya kukata rufaa zaidi ya kukata rufaa kwa wananchi wenyewe kama anaona kaonewa 2010 is just round the corner asubiri akate rufaa kwa wananchi.

  The way huyu jamaa anavyopayuka ovyo sadly i have to congratulate Tarime people for electing Chadema MP
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,679
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  Nafurahi sana kusikia maneno kama haya toka kwako. Hongera sana kwa hilo.
   
 20. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa Tarime CCM kushinda ni kazi, manake hata kama sehemu nyingine huiba pale si rahisi. Wale jamaa wako Ngangari kinoma. Sasa Mtikila alienda Tarime kuambulia jeraha na kushonwa, kapata kura chache vibaya mno. Viongozi wa upinzani shikamaneni, raia chini wameshashikamana, onesheni njia.
   
Loading...