Mgombea wa CCM Arusha atembelea vituo vya kujiandikisha

Mgombea wa CCM Arusha atembelea vituo vya kujiandikisha

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
183
Katika hali isiyo ya kawaida mgombea aliyetangaza kuwania ubunge katika jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya CCM,Thomas Munisi amefanya ziara ya kushtukiza katika vituo mbalimbali vya kupigia kura hali ambayo imempa nafasi kubwa ya kuungwa mkono na wakazi wa Arusha.

Itakumbukwa ya kwamba ni mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwa sasa GODBLESS LEMA pekee ndiye aliyekuwa akizunguka kutembelea vituo hivyo peke yake hapo awali.

Hatahivyo juzi Munisi ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya KILIMANJARO MILLENIUM PRINTERS LTD(KPML) aliamua kutumia usafiri wake kutembelea vituo vya kujiandikisha vilivyopo kata ya UNGA LTD NA SEKEI ambao leo anaendelea na ziara yake katika vituo vilivyopo kata ya ELERAI.

Hatua ya Munisi kufanya ziara ya kutembelea vituo hivyo imeungwa mkono na makada wa CCM arusha ambapo baadhi yao wamesikika wakisema kuwa ni ujasisri mkubwa sana alioufanya kwani amekuwa ni mgombea pekee wa CCM kuzungukia vituo hivyo.

Munisi mwenyewe amehojiwa mara kwa mara na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu hatua hiyo lakini yeye amesema kuwa ameona ya kuwa hakuna hajan ya kusubiri hadi viongozi wa chama watembelee vituo hivyo na yeye kamamgombea ameamua kuzunguka ili kutoa hamasa kwa vijana kujiandikisha zaidi.

Kwa upepo ulivyo kwa sasa Arusha Munisi anatajwa kuleta ushindani mkubwa ndani ya chama cha CCM ambapo hadi sasa ni mkada watatu tu ambao ni MONABAN,NYARI NA KIM ndio wanatajwa kuwa na mvuto ndani ya CCM kwa sasa ambao wanatajwa kuchuana na LEMA hapa Arusha.

Makada na baadhi ya viongozi wa CCM Arusha wamefurahishwa na hatua ya MUNISI kuzungukia vituo vya kujiandikisha na hiin huenda ikampa karata ya kisiasa kupitishwa ndani ya chama chake cha CCM kwani amekuwa akifanya mambo tofauti na wagombea wenzake.

source-mimi buswelu moja hapa Arusha.

(pichani chini ni mgombea anayewania kuteuliwa na CCM Arusha kuwania jimbo la ARUSHA MJINI,THOMAS MUNISI ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya TOM GEMS)
.
 

Attachments

  • tomgem.jpg
    tomgem.jpg
    39.7 KB · Views: 862
Arusha hawako tayari kuiludisha madarakani ccm tena mwabieni anapoteza rasilimali zake bure

Umeona! yaani apo umesema ukweli wanaarusha hawako tiyali kuirudisha ccm madarakan ilo wasahau kabisa mwambie ahache kujiangaisha bure.
 
Ndoto za mchana nani anawajua wagombea hao Arusha mjini?
 
Arusha hawako tayari kuiludisha madarakani ccm tena mwabieni anapoteza rasilimali zake bure

Hata angezunguka mara laki ni ndoto za alinacha kupata arusha wanamsimamo wakisema wamesema ajipumzikie tuu asichoke asubir wakat wa kampeni
 
mkuu nihakikishie kama bado arusha wanajiandikisha ili nimjazie Mh Lema muda wa maongezi kwenye simu yake .
 
Arusha ukisamamisha JIWE kwa nembo ya CDM na mgombea wa CCM, jiwe CDM litamshinda mgombea wa CCM
 
Huyo jamaa kwa arusha akifanya mchezo atafunga hako kakampuni kake ka kilimanjaro printers bora akomae tu na hako kakampuni kake.
 
Arusha hawako tayari kuiludisha madarakani ccm tena mwabieni anapoteza rasilimali zake bure

huyu mleta habari siyo mzima .yaani tumpe Munisi ccm .ubunge arusha haswaa !!.sio bure ccm imeharibu ubongo wa wanachama wake kiasi wanaamini kupata uongozi kwa pesa .apeleke njaa zake
 
Hela zinamuwasha?

Amuulize masamaki wa kirumba mwanza aliuza hadi nyumba zake na udiwani hakupata....ccm sio chama cha kuaminika
 
Huyu jamaa namfahamu sana tangu akiwa mererani kabla hajafungua ofisi ya kununulia mawe pale arusha kwenye jengo la kanungaa. Ila kikubwa huyu ni mgumu sidhani kama anaweza kutoa hela kama watia nia wenzake maana kwa ccm lazima umwage pesa ndo upitishwe. Pia huyu tom ana kashfa ya kuwanyanyasa wafanyakazi wake na kuwarusha mishahara yao alipopewa tenda ya kukusanya ushuru wa parking kabla ya kunyang'anywa na nyari.
 
Bora msingeandika hiyo kilimanjaro millenium printers hii kampuni ilitusumbua wakati akiwa ana tenda ya parking arusha mjini
 
anajisumbua bureeeeeeeeeeeee arusha hata agombe sr Edo cdm wanashinda
 
mkuu nihakikishie kama bado arusha wanajiandikisha ili nimjazie Mh Lema muda wa maongezi kwenye simu yake .
Kumbe ni kweli jamaa kaishiwa hivyo? Ndio maana ma red brigade wa chama chake hawakumkawiza pale alipowarusha fedha zao
 
Arusha hata akipelekwa Mkapa CDM haitoki pale ..kwa ufupi CCM waachane na Arusha
 
Back
Top Bottom