Mgombea wa ACT Wazalendo kata ya Mbagala Kuu akamatwa na kupigwa na Polisi akiwa kituo cha kupigia kura

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,316
5,052
Mgombea wa Udiwani wa ACT Wazalendo Kata ya Mbagala Kuu, Shaweji Mketo amekamatwa na Polisi akiwa kituo Cha Kupigia kura ambako alikwenda kuzuia watu wasioandikishwa kupiga kura.Amejuruhiwa mguuni na Polisi akiwa mikononi mwao na sasa anapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa yaTemeke.

act.PNG


 
Uliahidi kufanya sherehe siku JK akitoka madarakani na ukamuimbia sana JPM. Kuja kushtuka CCM ni ile ile ukaanza kumnanga na kumpa all the worldly known curses na kusherehekea kifo chake. Umemuimbia mama mapambio yote lakini sahizi ndiyo unagundua kuwa naye ametokana na CCM 😀😀😀😀
 
Mgombea wa Udiwani wa ACT Wazalendo Kata ya Mbagala Kuu,Shaweji Mketo amekamatwa na Polisi akiwa kituo Cha Kupigia kura ambako alikwenda kuzuia watu wasioandikishwa kupiga kura.Amejuruhiwa mguuni na Polisi akiwa mikononi mwao na sasa anapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa yaTemeke https://t.co/90WSJZbQ3o
Hawana akili

Utashirikije uchaguzi kwa mentality hii ya meko?
Ni upumbavu . Meko alishanajisi kila kitu kawanajisi polisi wote na ccm wote
 
Mgombea wa Udiwani wa ACT Wazalendo Kata ya Mbagala Kuu,Shaweji Mketo amekamatwa na Polisi akiwa kituo Cha Kupigia kura ambako alikwenda kuzuia watu wasioandikishwa kupiga kura.Amejuruhiwa mguuni na Polisi akiwa mikononi mwao na sasa anapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa yaTemeke https://t.co/90WSJZbQ3o
Chokochoko eh, kajitwika kazi ya polisi wanataka IGP Huru
 
Upinzani ujitangaze kwa kutumia sera, badala ya kutengeneza matukio na kulalamika. Hakuna chama kinachoweza kuchaguliwa kwa sababu ya huruma.
 
Tumia lugha ya staha.
Hawa watu anaowaweka ndani ambao hawana hata hatia, ambao hata ndugu zao wakiwaletea chakula nasikia kuwa wanafukuzwa na chakula chao anawaweka ndani kwa staha?Kuweka watu ndani ambao wana-exercise haki zao za msingi kabisa za kikatiba za kutoa maoni yao ni staha?Hii mikong'oto unayoizungumzia katika huu uzi wako ina staha?

Kuna mzee wa miaka 83 jana alienda kutoa maoni yake kwenye kile kikao cha ndani cha Mwanza na amewekwa ndani hadi muda huu na polisi wamekataza kuwa asipewe dawa zake za presha,hii ni staha?

Samia kuongoza nchi bila ya kufuata katiba ambayo ameapa ni staha?
 
Back
Top Bottom