Mgombea wa ACT Wazalendo Bariadi, aliyetoweka apatikana

Mgombea wa ACT Wazalendo Bariadi, aliyetoweka apatikana

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,778
Reaction score
12,577
Bariadi. Mgombea ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Bariadi Magharibi, Masunga Nghezo ametoweka kusikojulikana na hajapatikana hadi sasa akiwa katika harakati za kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.

Mbali na kutoonekana kwa Nghezo, simu yake aliyokuwa akiitumia, ndiyo inatumika kutuma ujumbe wa vitisho kwenda kwa mzazi wa mgombea huyo ikimtaka amkanye mwanae kuachana na siasa vinginevyo familia nzima itadhurika.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Afisa Habari wake, Abdallah Khamis, imesema kuwa Nghezo alitoweka siku ya Jumatatu ya wiki hii akijiandaa kwenda katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Baneni. Taarifa hiyo inaeleza kuwa kabla ya kutoweka kwake, Nghezo, alienda kumtafuta dereva mwingine wa kumuendesha baada ya yule wa siku zote kwenda msibani na kwamba aliporudi na dereva mwingine aliliacha gari likiwa katika maandalizi ya kufungwa vipaza sauti.

Taarifa imeongeza kuwa baada ya dereva na viongozi wengine wa chama kumaliza kazi ya kufunga vipaza sauti walianza kumtafuta mgombea wao bila mafanikio huku simu yake ikiwa haipatikani hadi jana mzee wake alipopokea ujumbe mfupi wa simu kupitia simu ya mwanae ikimtaka kumkanya mwanae
aachane na siasa za Bariadi.

Pia taarifa ya Khamis inaeleza kuwa mzazi wa mgombea, Mzee Nghezo, anazidi kutumiwa ujumbe wenye masharti wakimpa muda wa saa sita kutekeleza masharti yao vinginevyo watamdhuru kijana wake na kisha kuitafuta familia nzima, Hata hivyo Mwananchi Digital imezungumza na mzazi wa mgombea huyo, Joseph Nghezo ambaye amethibitisha kupotea kwa mtoto wake tangu siku ya Jumatatu.

Mzee Nghezo amesema kuwa siku ya Jumatatu viongozi wa chama cha ACT- Wazalendo walimpigia simu wakitaka kujua kama mtoto wake yupo nyumbani, ndipo alishtuka kwakuwa alijua mwanawe yuko kwenye kampeni. Ameongeza kuwa baada ya kuulizwa sana juu ya mtoto wake, majirani walimshauri aende akatoe taarifa katika kituo cha polisi.

Tumeenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi hapa mjini Bariadi na polisi wamechukua maelezo hivyo wanafanya kazi’’ aliongeza Nghezo.
Mwananchi Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi ili kuthibtisha tukio hilo lakini hakuweza kuzungumza lolote kwakuwa alipopokea simu alisema yuko kwenye kikao.

==================================

Updates: 16: 45 02 Oct 2015

Mgombea Ubunge wa ACT Wazalendo, amepatikana leo Bariadi Mjini. Watu waliomteka, walimtupa akiwa na Majeraha Mwilini. Uchunguzi wa Polisi bado unaendelea.
 
Acheni kick zisizokuwa na kichwa wala miguu, Baneni ndio mtaa gani huko Bariadi? Mnadhani humu wote ni vilaza kama nyie Wahuni na Wasaliti wa Mabadiliko?!
 
bariadi napo kuna vimafia vya kuiga kutoka kwenye novel za chase,balaa
 
Zitto kwa kutafuta kick bwana!! Yaani wamteke mgombea wa ACT ana MADHARA gani kwa siasa za Bariadi huyo?
 
He ha ha ha umemtosa tena Magufuri na kurudi nyumbani ACT ambayo imefutwa rasmi jana Kigoma mjini.
Haiwezi kani kufutwa ni porojo tusha zoea, mimi ni ACT na kauliyetu ni TAIFA KWANZA, hivyo basi nauhuru wa kuangalia taifa kuliko kuwa NYUMBU, DIWANI-ACT,MBUNGE-ACT, RAIS MAGUFULI sio ccm namchagua MAGUFULI Sichagui CCM
 
Ha ha ha nimecheka sana kusema unatumia mchuzi (Magufuri ) lakini nyama ( CCM ) huli Loh........!!!!!?
 
Haiwezi kani kufutwa ni porojo tusha zoea, mimi ni ACT na kauliyetu ni TAIFA KWANZA, hivyo basi nauhuru wa kuangalia taifa kuliko kuwa NYUMBU, DIWANI-ACT,MBUNGE-ACT, RAIS MAGUFULI sio ccm namchagua MAGUFULI Sichagui CCM

Sasa ndugu yangu unavyama vingapi wewe si ni gamba!
 
Haiwezi kani kufutwa ni porojo tusha zoea, mimi ni ACT na kauliyetu ni TAIFA KWANZA, hivyo basi nauhuru wa kuangalia taifa kuliko kuwa NYUMBU, DIWANI-ACT,MBUNGE-ACT, RAIS MAGUFULI sio ccm namchagua MAGUFULI Sichagui CCM
Hicho ni chama kimoja usishangae nyingine ni Head Office nyingine ni branch tu. Wafanyakazi ni walewale leo kituo hiki kesho waweza kuwa HQ
 
wewe tumbo liko CCM, kiwiliwili kipo ACT.
Ndugu yangu mbona umekazania CCM! rafikiangu mm nampigania MAGUFULI si ccm, ACT ni chama changu ila namchukia Lowassa toka angali ccm na ntamchukia hadi mbinguni
 
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariad kwa tiketi ya ACT Wazalendo, ndugu Masunga ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajapatikana.Pia wapo wagombea wengine wa ACT ambao wanapokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana. Mfano mgombea Chilonwa ndugu Eva pia amekuwa akipokea vitisho.

Nasikitika kunoa siasa zimetufikisha hapa, ACT kama chama tulitaraji upinzani mkubwa toka kwa vyama vingine, lakini huu si upinzani ambao tulioutaraji, tukumbuke kuna maisha baada ya oct 25. Binafsi naomba jeshi la Polisi lisidharau hili jambo, hawa wahusika wakamatwe na washughulikwe kwa wajibu wa sheria.

geita.jpggeita.jpg
 
Ndugu yangu mbona umekazania CCM! rafikiangu mm nampigania MAGUFULI si ccm, ACT ni chama changu ila namchukia Lowassa toka angali ccm na ntamchukia hadi mbinguni

usitufanye sisi watoto wadogo.
Magufuli ni mgombea binafsi?
wewe tumbo liko CCM na masikio yako ACT.
 
usitufanye sisi watoto wadogo.
Magufuli ni mgombea binafsi?
wewe tumbo liko CCM na masikio yako ACT.

Teteeeeer......mkuu uko sahihi kabisa. Ccm wanatafuta watoke vipi kwa kumtumia magufuri....hatudaganyiki, magufuri ni ccm kama alivyo Chenge, jk na familia yake.

Tutapindua meza mwaka huu..
 
Hila zina mwisho na ukweli huchelewa tu ila mwisho hufika.
 
Tunapenda kumwona picha zake na majeraha! Kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa na kila mmoja wetu
 
Ndugu yangu mbona umekazania CCM! rafikiangu mm nampigania MAGUFULI si ccm, ACT ni chama changu ila namchukia Lowassa toka angali ccm na ntamchukia hadi mbinguni

Hapo penye red nani atakupa fursa hiyo ya kumpenda au kutompenda.
 
Back
Top Bottom