GE2025 Mgombea Urais NLD, Doyo Hassan aahidi kuondoa mfumo wa Kikokotoo

GE2025 Mgombea Urais NLD, Doyo Hassan aahidi kuondoa mfumo wa Kikokotoo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo,alieleza mfumo wa sasa unaotumika kuwapangia wastaafu na watumishi wa umma matumizi ya fedha zao baada ya kustaafu ni dharau na unaowafanyia wastaafu uonevu

Akizungumza Oktoba 22,2025 na wananchi wa Wilaya ya Kigamboni kwenye mkutano wa kampeni amesema serikali ya sasa imeweka utaratibu wa kikokotoo kwenye fedha za wastaafu zilizokusanywa kwa ajili ya akiba baada ya kustaafu, kisha inawapangia matumizi kwa awamu kupitia mfumo wa mahesabu

Amesema hali hiyo ni kinyume na heshima inayostahili kwa wastaafu ambao wamejitolea kwa muda mrefu katika huduma za umma

“Wastaafu hawana sababu ya kupangiwa matumizi ya fedha zao. Baada ya kustaafu, mtu anatakiwa kupewa fedha zake moja kwa moja ili aweze kuanza maisha mapya kwa uhuru, kuwekeza au kutimiza malengo yake binafsi,” alisema Doyo

Doyo alisema kutokana na hali hiyo wananchi wakimpa ridhaa ya kuwa rais mfumo huu wa kupanga matumizi kwa wastaafu serikali yake itauondoa

Amesema kila mstaafu atapewa fedha zake kwa ukamilifu, akiwa na uhuru wa kuamua jinsi anavyotaka kuzitumia hali hii itawawezesha wastaafu kupanga maisha yao, kuwekeza katika biashara au kilimo, na kuchangia maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla

Aidha, Doyo alisisitiza umuhimu wa kuwaandaa watumishi wa umma waliokaribia kustaafu kupitia elimu ya kifedha. Amefafanua kuwa mpango huu utahusisha mafunzo ya kupanga bajeti binafsi, fursa za uwekezaji salama na zinazozalisha faida, ushauri wa kifedha, na mbinu za kuepuka matumizi yasiyo na tija

Alisema lengo ni kuhakikisha kila mstaafu anatumia fedha zake kwa hekima, bila kulazimishwa na vizuizi vya serikali, na kufanikisha ustawi wake pamoja na wa familia yake

1761287311613.png


Chanzo: Nipashe Digital
 
Back
Top Bottom