GE2025 Mgombea Urais kupitia chama cha NCCR MAGEUZI agoma kuhutubia watu 6 Sumbawanga

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,617
Reaction score
39,974
Jana 19.09.2025 kulikuwa na kampeni za Urais mjini Sumbawanga. Mgombea Urais kwa tiketi ya NCCR MAGEUZI Bw. Ambari Khamis akiambatana na Mgombea mwenza wake Dr Evelyna walitarajwa kufanya kampeni za nguvu Kuomba kura za Wana Sumbawanga.

Lakini walichokikuta siyo walichotarajia na hivyo Mgombea akagoma kushuka kuongea na Wananchi 6 waliohudhuria kampeni yake.

Huyu Mgombea ana gari la serikali, Dereva na mlinzi anayelipwa fedha za walipa kodi. Tuwe na uchungu na hela kuliko kufuja kwa watu àmbao tunajua Wazi hata uenyekiti wa kitongoji hawawezi kushinda.
IMG-20250919-WA0040.jpg
===
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia NCCR-Mageuzi, Ambari Haji Hamisi, ameshindwa kuhutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Sabato Jangwani, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, baada ya kujitokeza wananchi wachache.

Tukio hilo limetokea baada ya wananchi kutojitokeza kwa wingi kama ilivyotarajiwa. Hata hivyo, mkutano uliendelea kwa kuhutubiwa na wagombea wawili wa udiwani wa kata za Momoka na Msua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa chama hicho mkoani humo, pamoja na kuwepo kwa maandalizi ya kutosha katika eneo la tukio, idadi ndogo ya watu waliojitokeza ilisababisha uamuzi wa kuahirisha kampeni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Septemba 19, 2025, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Rukwa, Patrick Mbalamwezi, amethibitisha kutofanyika kwa mkutano huo wa kampeni, akieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa kutokana na kutokuwepo kwa mahudhurio ya kutosha kutoka kwa wananchi.

“Ni kweli mgombea wetu alikuwepo kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni, lakini kwa bahati mbaya wananchi hawakujitokeza kwa idadi iliyotarajiwa.

“Tutajipanga wakati mwingine ili kuhakikisha tunawahamasisha wananchi wajitokeze kusikiliza sera na kunadi wagombea udiwani kupitia chama chao," amesema Mbalamwezi.

Source: Mwananchi
 
Wamegoma si kwa sababu hawampendi, wamegoma kwa sababu ya kuogopa mangeu kutoka Polifisiemu, unawaza kushangaa mnambiwa mmeandamana kabla ya Oktoba 29, mkala makwenzi...
 
Jana 19.09.2025 kulikuwa na kampeni za Urais mjini Sumbawanga. Mgombea Urais kwa tiketi ya NCCR MAGEUZI Bw. Ambari Khamis akiambatana na Mgombea mwenza wake Dr Evelyna walitarajwa kufanya kampeni za nguvu Kuomba kura za Wana Sumbawanga.
Lakini walichokikuta siyo walichotarajia na hivyo Mgombea akagoma kushuka kuongea na Wananchi 6 waliohudhuria kampeni yake.
Huyu Mgombea ana gari la serikali, Dereva na mlinzi anayelipwa fedha za walipa kodi. Tuwe na uchungu na hela kuliko kufuja kwa watu àmbao tunajua Wazi hata uenyekiti wa kitongoji hawawezi kushinda.
Ni Bora kuchekwa kidogo kuliko kuchekwa Sana😂
 
Sidhani kama hii habari ni ya ukweli. Kama walitegemea kupata umati mkubwa wa watu, mbona maandalizi yao ni ya hao watu sita?
 
Jana 19.09.2025 kulikuwa na kampeni za Urais mjini Sumbawanga. Mgombea Urais kwa tiketi ya NCCR MAGEUZI Bw. Ambari Khamis akiambatana na Mgombea mwenza wake Dr Evelyna walitarajwa kufanya kampeni za nguvu Kuomba kura za Wana Sumbawanga.

Lakini walichokikuta siyo walichotarajia na hivyo Mgombea akagoma kushuka kuongea na Wananchi 6 waliohudhuria kampeni yake.

Huyu Mgombea ana gari la serikali, Dereva na mlinzi anayelipwa fedha za walipa kodi. Tuwe na uchungu na hela kuliko kufuja kwa watu àmbao tunajua Wazi hata uenyekiti wa kitongoji hawawezi kushinda.
View attachment 3476283
Hata mimi ningegoma hizo ni dharau saana🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom