Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad leo Agosti 7, 2020, wamechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za NEC Jijini Dodoma.

View attachment 1529783
View attachment 1529827
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe katika Ofisi za NEC Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020, kushoto ni Mgombea Mwenza, Prof. Omar Faki Hamad . Chama hicho kinakuwa cha nane kuchukua fomu.

View attachment 1529828

====
TAARIFA KWA UMMA

MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Bernard Kamilius Membe leo tarehe 7, Agosti 2020 amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Membe amekabidhiwa fomu hiyo ya uteuzi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage Jijini Dodoma.

Katika uchukuaji huo wa fomu, Membe aliambatana na Mgombea mwenza wake, Profesa Omary Fakih Hamad.

Aidha msafara huo wa Membe uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu, Ndugu Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Mhonga Said Ruhwanya, Katibu wa Mambo ya Nje Ndugu Bonifasia Mapunda, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Ndugu Janeth Rithe, Katibu wa Ngome ya Vijana Ndugu Mwanaisha Mndeme na viongozi wengine waandamizi wa Chama.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Ndugu Bernard Membe amesema kuwa amejiandaa kufanya kampeni kabambe kila Kona ya nchi ili kuipatia ACT Wazalendo ushindi mnono na kuhakikisha ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020, utawala wa Rais Magufuli unafikia tamati.

Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.

Imetolewa leo tarehe 07 Agosti 2020.
Wapinzani naona wanapiga mark time tu
Hawa watu wanajua fika kinachowakosesha ubungwa mara nyingi ni mgawanyo wa Kura
Kwanini Membe na Lissu wagombee wakati mmoja?
 
Mtu yeyote anayeamini kuwa Membe ni mpinzani basi huyo ana ukichaa ambao hata Mirembe hawawezi kuutibu

Kiongozi wa Act wazalendo alivuruga uchaguzi wa wapinzani (UKAWA) 2015 na mwaka huu, 2020 yale yale ya 2015 yatatokea!! Ni Magufuli ushindi slop slop 90% ya kura zote!!
 
Nadhani ACT wazalendo wangetumia akili kidogo kumnadi mgombea anaekubalika na watanzania kwa sasa. Kiukweli TL ndio chaguo la watanzania mambo ya kumchagua membe tunarudia makosa tuliyofanya law lowassa mwisho wa siku anarudi ccm.
 
hili ni pandikizi kuu la ccm, kazi yake kuu ni kuhakikisha anapunguza kura za upinzani.........mtanielewa siku fulani..
Mtaacha lini siasa za kutafuta kura za huruma? Ni kosa la kiufundi kuingia kwenye uchaguzi ukitegemea msaada wa chama kingne. Hakuna chama kilichoanzishwa kwa ajili ya kukisaidia kingine kushinda.
 
Hata media coverage imeipa very minimal publicity ACT. Hakuna wa kumshinda baba leo Magufuli.
 
Mtaacha lini siasa za kutafuta kura za huruma? Ni kosa la kiufundi kuingia kwenye uchaguzi ukitegemea msaada wa chama kingne. Hakuna chama kilichoanzishwa kwa ajili ya kukisaidia kingine kushinda.
endelea na usingizi wako mkuu.
 
... yuko kazini hivyo!
Yaaani anatupotezea muda tu......... Usikute kila siku anafanya retirement kule ofisi za tiss kwa kueleza Mikakati ya act na wapinzani......

Maccm sio majitu ya kuyaamini kabisa
 
Back
Top Bottom