GE2025 Mgombea Urais ADC, Wilson Elias Mulumbe aahidi Mwanza kuwa Paradiso

GE2025 Mgombea Urais ADC, Wilson Elias Mulumbe aahidi Mwanza kuwa Paradiso

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza, Jiji la Mwanza litakuwa ‘paradiso’ ya maisha bora na kitovu cha uchumi na maendeleo nchini

Kauli hiyo ameitoa Jumapili, Septemba 7, 2025, wakati akihutubia katika matawi mbalimbali ya chama hicho wilayani Ilemela. Mulumbe amesisitiza kuwa, akiwa Rais, atabadilisha hali ya maisha ya wananchi na kuboresha maendeleo ya kiuchumi katika jiji hilo

Ameahidi pia, kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa wanawake kwa masharti nafuu na kuimarisha elimu katika shule za Serikali ili wahitimu wa vyuo vikuu waweze kufundisha shule za msingi

Mwenyekiti wa ADC, Shaabani Itutu amesisitiza kuwa, chama hicho kitatumia rasilimali za nchi kuboresha huduma za jamii, ikiwamo afya na maji. Mgombea mwenza wa urais, Shoka Khamis Juma amewataka wananchi wa Ilemela kuchagua ADC ili kuleta mabadiliko ya kweli

Pia Soma: GE2025 - Mgombea Urais ADC: Nikiwa Rais amtolipa umeme wala maji


 
Back
Top Bottom