Mgombea urais 2015 atinga Vatican

Mgombea urais 2015 atinga Vatican

Bernard Camilius Membe hafai kuwa Rais wa Tanzania kwa sasa! Labda baada ya miaka 30 ijayo!!!
 
Magazet mengine ni ya udaku tu mbona hawataji jina lake au ni mbinu ya kuuza zageti ...uongo mtupu.

Sure... Hata mie naona Mtanzania la Rosti Tamu l'Azizi linataka soko tu. Nawashangaa wanalolisoma! Na ukiona hivyo, waziri huyo aliyesemwa bila kutajwa jina, ni mpinzania wa Lowassa katika safari hiyo ya Ikulu!
 
Mmeanza siasa zenu chafu​ zakupakana matope kisa kwenda ikulu inajulikana hayo magazeti yalinunuliwa kwa nia moja yakuwachafua wapinzani wa JK na mlifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwandama na kuwachafua Salim na Sumaye.

Sio lazima mbinu hiyo ifanikiwe na safari hii,mambo yanabadirika na wakati, hizo ni propaganda za Bashe dhidi ya Membe kama alivyodhihirisha kule Dodoma kwa kumpiga vita lakini mwisho wa siku Membe akashinda.

Hiyo safari ya Vatican uenda kweli ilikuwepo lakini isiwe na uhusiano wowote na mambo ya uchaguzi ujao,ila kwa vile Lowasa kila akilala na kuamka anaota urais,tafsiri ya chochote anachokisikia anahisi ni cha kuhatarisha dhamira yake hofu yakuusarandia urais.

Kwa usongo mliokuwa nao dhidi ya Membe hamgekosa picha za safari na vielelezo vya magari 24 yanayodaiwa kutoka Uarabuni.

Inaonekana kama vile TB Joshua alishamhapisha Lowasa kuwa rais wa Tanzania.
 
WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 likiendelea kupanda miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaohusishwa na harakati za kuwania urais, mmoja wa makada hao amekwenda Vatican kwa nia ya kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki duniani, MTANZANIA Jumapili limedokezwa.

Habari za uhakika kutoka katika chanzo cha karibu na kada huyo ambaye pia ni waziri kwenye moja ya wizara nyeti nchini, kimedai kuwa waziri huyo amezuru jijini Vatican hivi karibuni.

Mtoa habari wetu huyo alilidokeza gazeti hili kuwa licha ya ziara ya waziri huyo jijini Vatican kuonyesha kuwa ni ya kikazi, lakini lengo kuu la kuelekea huko lilikuwa ni kutambulisha dhamira yake ya kuwania urais 2015.

Alisema kuwa waziri huyo, ambaye katika
historia ya elimu inaonyesha amepata kusoma shule ya seminari, alipofika mjini Vatican alikutana kwa faragha na maofisa kadhaa wa Kanisa Katoliki duniani, ambapo alitumia nafasi hiyo kupenyeza lengo lake kuhusu dhamira ya kugombea urais mwakani.

“Alikwenda Vatican akiwa na lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki na tangu amerudi amekuwa akijinadi kwamba Vatican itamuunga mkono Rais wa Tanzania mwaka 2015,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Awali gazeti hili lilidokezwa na chanzo kingine cha habari ambacho kipo naye karibu katika wizara anayoiongoza kuwa waziri huyo alisafiri kwenda Vatican mwishoni mwa Julai na akarejea nchini mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu.

Mbali na ziara ya Vatican, waziri huyo amedaiwa kuwa na mpango wa kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini, Kardinali Polycarp Pengo, kwa lengo la kumdokezea juu ya dhamira yake hiyo, hasa baada ya kuwa amerudi kutoka makao makuu ya kanisa hilo.

Katika hatua nyingine, gazeti hili lilimkariri mmoja wa vijana anayeunda kundi linalompigia kampeni waziri huyo akisema: “Tayari tupo vijana ndani ya CCM ambao tumeanza kuzunguka nchi nzima kueneza habari hii ya mavuno kwetu”.

Pia kijana huyo alidokeza kwamba hivi karibuni waziri huyo ameingiza nchini magari 24 aina ya VX Land Cruiser kutoka katika nchi za Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuendesha mkakati wa kundi lake wa kuzunguka nchi nzima kutafua ushawishi ndani na nje ya chama.

Kijana huyo alidai kwamba moja ya magari hayo analitumia mmoja wa viongozi wa juu wa CCM ambaye hivi karibuni alikwenda nalo mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Kamati Kuu ya chama (CC).

Waziri huyo anayetajwa katika mikakati ya sasa ni mmoja kati ya makada sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanatumikia kifungo cha mwaka mmoja cha kutojihusisha na masuala ya siasa kwa kosa la kuanza kampeni za urais mapema kinyume cha kanuni za chama.

Wanaotumikia adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani,
Edward, Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira.

Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Chanzo: Mtazania

Sasa kaficha kitu gani hapo hata mtoto mdogo anafahamu!
 
Kama amekwenda vatikani kupata upako ni haki yake ushauri wangu kwa wapinzani wake ni kwamba nao waende ili wakapimwe kama wana sifa njema ya kutuvusha hapa tulipo jikwaa.

Wengi wanenda kwa TB Joshua na kupewa maji!

Huyu waziri atakuwa anatoka mikoa ya kusini.

WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 likiendelea kupanda miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaohusishwa na harakati za kuwania urais, mmoja wa makada hao amekwenda Vatican kwa nia ya kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki duniani, MTANZANIA Jumapili limedokezwa.

Habari za uhakika kutoka katika chanzo cha karibu na kada huyo ambaye pia ni waziri kwenye moja ya wizara nyeti nchini, kimedai kuwa waziri huyo amezuru jijini Vatican hivi karibuni.

Mtoa habari wetu huyo alilidokeza gazeti hili kuwa licha ya ziara ya waziri huyo jijini Vatican kuonyesha kuwa ni ya kikazi, lakini lengo kuu la kuelekea huko lilikuwa ni kutambulisha dhamira yake ya kuwania urais 2015.

Alisema kuwa waziri huyo, ambaye katika historia ya elimu inaonyesha amepata kusoma shule ya seminari, alipofika mjini Vatican alikutana kwa faragha na maofisa kadhaa wa Kanisa Katoliki duniani, ambapo alitumia nafasi hiyo kupenyeza lengo lake kuhusu dhamira ya kugombea urais mwakani.

“Alikwenda Vatican akiwa na lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki na tangu amerudi amekuwa akijinadi kwamba Vatican itamuunga mkono Rais wa Tanzania mwaka 2015,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Awali gazeti hili lilidokezwa na chanzo kingine cha habari ambacho kipo naye karibu katika wizara anayoiongoza kuwa waziri huyo alisafiri kwenda Vatican mwishoni mwa Julai na akarejea nchini mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu.

Mbali na ziara ya Vatican, waziri huyo amedaiwa kuwa na mpango wa kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini, Kardinali Polycarp Pengo, kwa lengo la kumdokezea juu ya dhamira yake hiyo, hasa baada ya kuwa amerudi kutoka makao makuu ya kanisa hilo.

Katika hatua nyingine, gazeti hili lilimkariri mmoja wa vijana anayeunda kundi linalompigia kampeni waziri huyo akisema: “Tayari tupo vijana ndani ya CCM ambao tumeanza kuzunguka nchi nzima kueneza habari hii ya mavuno kwetu”.

Pia kijana huyo alidokeza kwamba hivi karibuni waziri huyo ameingiza nchini magari 24 aina ya VX Land Cruiser kutoka katika nchi za Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuendesha mkakati wa kundi lake wa kuzunguka nchi nzima kutafua ushawishi ndani na nje ya chama.

Kijana huyo alidai kwamba moja ya magari hayo analitumia mmoja wa viongozi wa juu wa CCM ambaye hivi karibuni alikwenda nalo mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Kamati Kuu ya chama (CC).

Waziri huyo anayetajwa katika mikakati ya sasa ni mmoja kati ya makada sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanatumikia kifungo cha mwaka mmoja cha kutojihusisha na masuala ya siasa kwa kosa la kuanza kampeni za urais mapema kinyume cha kanuni za chama.

Wanaotumikia adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward, Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira.

Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Chanzo: Mtazania
 
Hivi kati ya hawa wafungwa Wa kisiasa ndani ya CMM, Lowassa na Membe nani mwenye mvuto na uwezo Wa kuongoza nchi?
 
WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 likiendelea kupanda miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaohusishwa na harakati za kuwania urais, mmoja wa makada hao amekwenda Vatican kwa nia ya kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki duniani, MTANZANIA Jumapili limedokezwa.

Chanzo: Mtazania

Wengine walienda kwa TB Joshua kama picha hapa chini inavyoonyesha

tb-joshua-viewers.jpg
 
  • Thanks
Reactions: jme
Back
Top Bottom