GE2025 Mgombea ubunge CHAUMMA amnadi Samia jukwaani akipiga kampeni

GE2025 Mgombea ubunge CHAUMMA amnadi Samia jukwaani akipiga kampeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,777
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma Agnesta Lambert Kaiza amemsifia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anatenga fedha za kutosha kwenye mikopo kwa ajili ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

"Mama Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani akasema Marais Wenzangu walikuwa wanatoa mikopo inayoitwa mikopo ya riba nafuu, alipowaangalia wanawake wa Kitanzania alipowaangalia vijana na walemavu akawaona akina mama. Mama yetu Samia Suluhu Hassan akasema nakwenda kushusha fedha katika kila Halmashauri hiyo fedha akina mama vijana na wenye ulemavu wakopeshwe fedha bila riba" amesema Agnesta

Aidha ameongeza kuwa pamoja na Dkt. Samia kutoa fedha hizo ambazo ni kodi za Watanzania, kutokana na tafiti zake amebaini kuwa wanawake hawapati mikopo hiyo na sababu ni viongozi wa chini kutosimamia fedha hizo.

Agnesta amezungumza haya alipokuwa katika mkutano wake wa kwanza wa kampeni katika uwanja wa Msikate Tamaa, Vingunguti jijini Dar Es Salaam.


 
Back
Top Bottom