Mgombea ubunge CHADEMA afukuzwa Bunda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea ubunge CHADEMA afukuzwa Bunda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by elimukwanza, Feb 28, 2011.

 1. e

  elimukwanza Senior Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wadau kuna habari nimeipata jana kutoka kwenye mkutano wa CDM wilayani bunda kuwa aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la bunda kupitia CDM Ndg Elias Kajeli Maarugu amefukuzwa na wafuasi wenye hasira katika mkutano wa CDM kwa kile kinachodaiwa kuwa aliuza jimbo kwa mh Wasira katika uchaguzi mkuu 2010.kama kuna mdau aliyekuwepo atujuze zaidi nini kilitokea zaidi ya hapo.
   
 2. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hebu check gazet la mwananchi.
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hivyo vyote ni visingizio
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MFA maji ...............
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  La lini mkuu?
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Nenda hapo thread #5 juu bofya link mieweka
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbona kuna wagombea wengi wa CHADEMA,walishindwa maeneo mabalimbali,lakini hawajawahi kufukuza kwenye mikutano kama hii!hata kama upo CCM ukiona hivyo ujue kuna jambo mkuu!!
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  poa mkuu, nashukuru sana!!
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA mgombea ubunge wa ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Bunda Elias Maarugu ametimuliwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliohutubiwa na katibu mkuu Dk Wilbroad Slaa baada ya kukataliwa
  na wananchi kwa madai kuwa alihongwa na kumwachia Stephen Wasira.

  Dalili za kumkataa Maarugu zilianza mapema mara baada ya kuitwa asalimie wananchi mjini Bunda, umati mkubwa wa wananchi ulipiga kelele na kudai hawataki kumsikiliza kwa kuwa aliwasaliti na kuuza haki zao.

  Wananchi hao walipiga kelele wakisema hawako tayari kumsikiliza huku wakimtaka atoke jukwaani kwa kuwa hafai, "hatumtaki huyo mtoeni hapo aliuza kura, alihongwa msaliti hafai mtoeni hatutaki kumsikiliza."

  Kelele hizo zilisikika sauti kwa nguvu za wananchi waliojaza uwanja wa stendi ya zamani.

  Licha ya Maarugu kujikakamua na kusema Peoples, wananchi walipaza sauti na kumtaka atoke haraka sana," hatutaki kumsikiliza huyo mtoeni huyo hafai msaliti alikuwa wapi kwanini amekuja leo siku zote alikuwa
  wapi?"walihoji.

  Kutokana na kelele na wananchi kugoma kumsikiliza Dk Slaa alilazimika kuingilia kati na kusema kuwa, "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama umma wote huu unakukataa ndugu yangu Maalugu kuna kitu naomba utueleze kwa nini watu hawa wanakukataa."

  Hata hivyo katibu mkuu huyo kuwataka wananchi wawe na subira wananchi waliendelea kugoma na kusema kuwa hawako tayari kumwona wala kumsikiliza hivyo wakamtaka atoke eneo hilo.

  "Maarugu Chadema inapinga ufisadi ndani na nje ya chama kama unatuhumiwa wewe ni mtu mzima na kuheshimu sana nakuomba uamke taratibu uage uende kwako na sisi tunakuchunguza, natamka kuanzia sasa
  kuwa nakufutia ugombea wa miaka mitano ijayo kwa kuwa hufai maana nakataliwa na wananchi, nitatoa taarifa kwenye kamati tendaji ya chama,"alisema.

  Kutokana na kauli hiyo Maarugu ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Magu na Misenyi alilazimika kushuka taratibu huku akizomewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika hapo,huku Dk Slaa akiwasihi wananchi
  wasimpige,kumtukana kwa kuwa suala lake bado linachunguzwa na wananchi watapewa majibu.

  Aliagiza kamati tendaji ya chama wilaya kuketi haraka kujadili kisha kutoa taarifa kwake ndani ya wiki mbili, na kama wataridhika nayo wataifanyia kazi,vinginevyo watalazimika kuunda kamati maalumya kufuatilia kwa kuwahoji wananchi wa jimbo hilo. .........

  Source: Mwananch 28/2/2011
   
 11. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Big Up Dr.Slaa,kama mtu amekataliwa na wananchi,then wa nini?
  kuleana leana ndo ilowaponza ccm kwenye kura za maoni...
   
 12. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,110
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Kweli Dr Slaa amemfutia ugombea Maarugu kwa miaka 5 ijayo? bila kukamilika uchunguzi? sijui kama ni kweli? labda tuambieni zaidi
   
 13. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [FONT=georgia, bookman old style, palatino linotype, book antiqua, palatino, trebuchet ms, helvetica, garamond, sans-serif, arial, verdana, avante garde, century gothic, comic sans ms, times, times new roman, serif]Remember the difference between a boss and a leader; a boss says "Go!" - a leader says "Let's go!" ~E.M. Kelly[/FONT]
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na bado wengi watafukuzwa. Sasa naona Chadema wanatafuta mchawi.
   
Loading...