MGOMBEA MWENZA KUREJEA CUF
Kutokana na mivutano inayoendelea ndani ya viongozi wa upinzani, taarifa zinasema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi wa CUF upande wa Tanzania bara kulalamikia kutotimizwa kwa makubaliano yaliyofikiwa wakati wanaungana katika umoja na kupinga namna Chadema wanavyoendesha umoja huo. Aidha kutokana na hali hiyo,taarifa zinadai kunauwezekano mkubwa mudawowote kuanzia sasa mgombea mwenza wa Chadema Juma Duni kutangaza kujitoa kwenye chama hicho na kurejea CUF.