Mgombea kujengea mafisadi gereza la ghorofa

Mgombea kujengea mafisadi gereza la ghorofa

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
mgombea+pic.jpg


Moshi. Mgombea udiwani ameomba kuchaguliwa ili ajenge gereza la ghorofa la mafisadi litakalokuwa na bwawa la kuogelea na wafungwa wataruhusiwa kukutana na wake zao. Hizo ni ahadi za mgombea wa chama cha Sauti ya Umma (Sau), Issack Kireti alizozitoa juzi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ofisi ya zamani ya Kata ya Mawenzi.

Kireti ambaye unaweza kusema ni mgombea ambaye hachoshi kumsikiliza kutokana na ahadi zake, namna alivyovaa na kipaza sauti anachotumia. Juzi jioni kwenye mkutano wake kampeni akionekana kama anahutubia wapita njia zaidi, aliahidi kujenga magereza yenye jengo la ghorofa maalumu kwa ajili ya wafungwa wa makosa ya rushwa na ufisadi.

Akihutubia huku akiwa amevalia aproni yenye nembo ya chama chake, Kireti alisema gereza hilo litakuwa na bwawa la kuogelea na wafungwa wataruhusiwa kukutana na wake zao. “Nilipokuwa nagombea ubunge 2015 nililiahidi hili na leo nataka niwaahidi tena mkinichagua kuwa diwani nitapigania kujengwa kwa gereza la ghorofa kwa ajili ya mafisadi na wala rushwa,” alisema. Lakini, hakuishia hapo, kwani alikuja na ahadi nyingine kubwa zaidi ambapo aliahidi kujenga madaraja ya kupita juu (flyovers) kwa ajili ya kuwaepusha watembea kwa miguu na ajali za bodaboda. “Kumekuwa na ajali nyingi za bodaboda wakati watembea kwa miguu wakivuka barabara. Nitakomesha hili kwa kujenga flyovers barabara muhimu ili tuondoe alama za pundamilia,” adai

Katika mkutano huo ambao hapakuwepo msemaji mwingine yeyote zaidi yake, mgombea huyo aliahidi kupanda miti katika hospitali ya Mawenzi ili wagonjwa wawe wanakula matunda bila kununua.
 
Kujenga hilo ghorofa tu ni ufisadi tosha, akimaliza na yeye anawekwa ndani.
 
Hawa huwa tunasema "wafurahisha msafala"

Wanasindikiza uchaguzi na ndio maana huwa hawachukuliwagi serious ni kama Hashim Rungwe alivyosema "mkinichagua nitatumia helicopter kumwagilia mashamba"
 
Back
Top Bottom