Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi
Hii ni Makala ya Jumapili ya Leo
Screen Shot 2022-06-26 at 1.08.26 PM.png
Screen Shot 2022-06-26 at 1.08.42 PM.png

Leo naendelea na ile mada ya kuhusu Haki za Kikatiba, zilizotolewa na Ibara moja ya Katiba, halafu zikaja kuporwa kwa kuchomekewa vifungu vinavyopora haki hiyo na ibara nyingine.

Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili. Mahakama Kuu ndio mamlaka pekee ndani ya JMT, inayoweza kutamka sheria fulani ni batili. Hili ninalozungumza hapa, Mahakama Kuu iliishalitamka ni Batili.

Bunge limetunga sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya mwaka 1977.
. Mahakama Kuu Ikatamka Sheria hiyo ni batili kwasababu inakwenda kinyume katiba!. Serikali yetu, kupitia Bunge, letu, ikafanya marekebisho ya katiba yetu na kuvichomekea hivyo vipengele batili, ndani ya katiba yetu!.

Mahakama Kuu chini ya Half Bench (Majaji 3) ikatamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Mahakama ya Rufani chini ya Full Bench (Majaji 7) wakaubariki ubatili huo not expressly but impliedly kwa kusema "the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Yaani Mahakama Kuu imesema jambo hili ni batili!,
Serikali ikaichukua batili hiyo ikaipitisha Bungeni kwa hati ya dharura, ikafanya marekebisho ya katiba, ikachomekea batili hiyo ndani ya katiba yetu.
Mahakama Kuu ikasema tena, hata uchomemekeaji huo uliofanywa na Bunge letu, kuichomekea hiyo batili ndani ya katiba yetu, nayo ni batili!.

Jambo la ajabu likafanywa na Mahakama ya Rufani, haizungumzi lolote kuhusu hiyo batili, wala ubatili uliofanyika wa kuichomeka batili ndani ya katiba yetu!, bali ikasema Mahakama sio custodian wa the will of the people, bali ni Bunge lenye wawakilishi wa wananchi, hivyo kulirudisha hilo jambo kwa bunge ndio iliondoe!, bila hata kutamka kuwa ni batili!. Huo ubatili mpaka ninavyoandika hapa sasa, bado ukingali upo ndani ya katiba yetu, Jee Turuhusu Ubatili Huu Uendelee Kuwepo Ndani ya Katiba Yetu Mpaka Lini?. Tunaomba Jicho la Haki la Mama, liuangazie ubatili huu, mimi kama mimi nasema "Tusiruhusu!", Jee vipi wewe mwenzangu?.

Haki ninayoizungumza hapa ni haki ya kila Mtanzania kuwa huru kuchagua kiongozi wake kwa kupiga kura kama ilivyotolewa na Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT ambayo ilipaswa kwenda sambamba na haki ya kila Mtanzania kuchaguliwa iliyotolewa na Ibara 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, jinsi ilivyokuja kuporwa na shurti la mgombea uongozi wa umma, kudhaminiwa na chama cha siasa hivyo kuipora kabisa ile haki iliyotolewa na ibara ya 21.

Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi

Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya kwanza ilikata rufaa kuipinga hukumu ya Jaji Lukakingira!. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!.

Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali katiba yetu ichezewe, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu

(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.

(b) Kutamka wazi kuwa kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!.

Lakini serikali yetu ya wakati huo, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench chini ya majaji 7, wakiongozwa na Jaji Mkuu mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu.

Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabingwa wabobezi watatu wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, (baadae akawa Mwanasheria Mkuu Zanzibar, sasa ni Makamo wa kwanza wa rais Zanziibar), Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa (Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua ifuatavyo, hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Hapa Mahakama ya Rufani Tanzania, ilijivua jukumu la kuilinda katiba. Kama ubatili unafanywa kwenye katiba yetu, halafu Mahakama yenye jukumu la kutafsiri katiba inajivua jukumu hili!, who is the custodian of the will of the people?.

Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, halafu Bunge likatunga sheria kuifuta haki hiyo, ilitegemewa mahakama kutumia mamlaka yake ya “checks and balance” kulia,nia Bunge haliwezi kutunga sheria inayokwenda kinyume cha katiba!. Mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?.

Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!. Yaani Bunge litunge sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kisha kipengele cha sheria hiyo batili kikachomekewa ndani ya katiba kwa mabadiliko yakatiba kwa hati ya dharura!. Mahakama Kuu inasema huu ni ubatili, Mahakama ya Rufaa inasema “hatuwezi kuliingilia Bunge!.

Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ukatufungua macho kuhusu political silent status za baadhi ya majaji wetu!. Kumbe baadhi ya majaji wetu nao ni makada wa vyama vya siasa!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama wakuu wa mhimili wa mahakama mara tuu baada ya kustaafu wanageuka makada!.

Tunamuomba Rais Samia, atuondolee ubatili huu ndani ya katiba yetu!

Wasalaam

Paskali
Uli kulielewa vema banndiko hili, lisomwe na Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
 
Kati ya vitu vya kufanyia kazi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025, ni pamoja na uwepo wa Tume Huru ya uchaguzi, lakini pia kuruhusiwa kwa Mgombea binafsi.

Haya mambo ya kulazimishana kugombea kupitia vyama vya siasa, hayakubaliki. Ifikie wakati yale maamuzi ya mahakama ya kuruhusu Mgombea binafsi, yaheshimiwe.

NB: Mkuu, isije tu ikawa umekuja na hili wazo kwa sababu ya wale Wajumbe wako wa Kawe.
 
Mkuu Tate Mkuu haya sasa ndio maslahi ya taifa.
Haya mambo ya kulazimishana kugombea kupitia vyama vya siasa, hayakubaliki. Ifikie wakati yale maamuzi ya mahakama ya kuruhusu Mgombea binafsi, yaheshimiwe.
Naunga mkono hoja
NB: Mkuu, isije tu ikawa umekuja na hili wazo kwa sababu ya wale Wajumbe wako wa Kawe.
No sio hasira za wajumbe wa Kawe, ni utetezi tuu huru wa haki.
P
 
Kwa hiyo wajumbe wa CCM hawakusimamia haki?
Wajumbe wa chama chetu, wanatoa kura zao sio kwa hoja za mtu, hebu sikiliza hoja za mtu huyu, alitaka kwenda kufanya nini bungeni

Linganisha na aliyepo
P
 
Mtikil hakuishia hapo alifungua kesi Mahakama ya Africa na kushinda hiyo kesi.
Ilipokuja Mahakama kuu ili kuthibitishwa utetezi was serikali ilikuwa kuna mchakato was katiba na mgombea binafsi ilikuwa moja ya mapendekezo ya katiba mpya. Lakini mchakato ulivurugika sababu kupata katiba mpya ni kama hisani.
Bado inaweza kufunguliwa kesi ya kubadili katiba kuruhusu mgombea binafsi.
 
Hivi wewe Paskali wa JF ni muumini wa Katiba Mpya? if yes, since when? isije kuwa juzi baada ya maazimio ya KK yenu.
 
Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ukatufungua macho kuhusu political silent status za baadhi ya majaji wetu!. Kumbe baadhi ya majaji wetu nao ni makada wa vyama vya siasa!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama wakuu wa mhimili wa mahakama mara tuu baada ya kustaafu wanageuka makada!.
Mhimili wa mahakama una Uhuru wa kwenye karatasi tu (rejea kesi ya ugaidi ya Mbowe), huu mhimili upo kwa ajili ya kulinda hatamu za chama dola tu
 
Wanabodi
Hii ni Makala ya Jumapili ya Leo
View attachment 2272777View attachment 2272779

Leo naendelea na ile mada ya kuhusu Haki za Kikatiba, zilizotolewa na Ibara moja ya Katiba, halafu zikaja kuporwa kwa kuchomekewa vifungu vinavyopora haki hiyo na ibara nyingine.

Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili. Mahakama Kuu ndio mamlaka pekee ndani ya JMT, inayoweza kutamka sheria fulani ni batili. Hili ninalozungumza hapa, Mahakama Kuu iliishalitamka ni Batili.

Bunge limetunga sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya mwaka 1977.
. Mahakama Kuu Ikatamka Sheria hiyo ni batili kwasababu inakwenda kinyume katiba!. Serikali yetu, kupitia Bunge, letu, ikafanya marekebisho ya katiba yetu na kuvichomekea hivyo vipengele batili, ndani ya katiba yetu!.

Mahakama Kuu chini ya Half Bench (Majaji 3) ikatamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Mahakama ya Rufani chini ya Full Bench (Majaji 7) wakaubariki ubatili huo not expressly but impliedly kwa kusema "the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Yaani Mahakama Kuu imesema jambo hili ni batili!,
Serikali ikaichukua batili hiyo ikaipitisha Bungeni kwa hati ya dharura, ikafanya marekebisho ya katiba, ikachomekea batili hiyo ndani ya katiba yetu.
Mahakama Kuu ikasema tena, hata uchomemekeaji huo uliofanywa na Bunge letu, kuichomekea hiyo batili ndani ya katiba yetu, nayo ni batili!.

Jambo la ajabu likafanywa na Mahakama ya Rufani, haizungumzi lolote kuhusu hiyo batili, wala ubatili uliofanyika wa kuichomeka batili ndani ya katiba yetu!, bali ikasema Mahakama sio custodian wa the will of the people, bali ni Bunge lenye wawakilishi wa wananchi, hivyo kulirudisha hilo jambo kwa bunge ndio iliondoe!, bila hata kutamka kuwa ni batili!. Huo ubatili mpaka ninavyoandika hapa sasa, bado ukingali upo ndani ya katiba yetu, Jee Turuhusu Ubatili Huu Uendelee Kuwepo Ndani ya Katiba Yetu Mpaka Lini?. Tunaomba Jicho la Haki la Mama, liuangazie ubatili huu, mimi kama mimi nasema "Tusiruhusu!", Jee vipi wewe mwenzangu?.

Haki ninayoizungumza hapa ni haki ya kila Mtanzania kuwa huru kuchagua kiongozi wake kwa kupiga kura kama ilivyotolewa na Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT ambayo ilipaswa kwenda sambamba na haki ya kila Mtanzania kuchaguliwa iliyotolewa na Ibara 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, jinsi ilivyokuja kuporwa na shurti la mgombea uongozi wa umma, kudhaminiwa na chama cha siasa hivyo kuipora kabisa ile haki iliyotolewa na ibara ya 21.

Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi

Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya kwanza ilikata rufaa kuipinga hukumu ya Jaji Lukakingira!. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!.

Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali katiba yetu ichezewe, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu

(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.

(b) Kutamka wazi kuwa kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!.

Lakini serikali yetu ya wakati huo, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench chini ya majaji 7, wakiongozwa na Jaji Mkuu mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu.

Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabingwa wabobezi watatu wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, (baadae akawa Mwanasheria Mkuu Zanzibar, sasa ni Makamo wa kwanza wa rais Zanziibar), Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa (Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua ifuatavyo, hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Hapa Mahakama ya Rufani Tanzania, ilijivua jukumu la kuilinda katiba. Kama ubatili unafanywa kwenye katiba yetu, halafu Mahakama yenye jukumu la kutafsiri katiba inajivua jukumu hili!, who is the custodian of the will of the people?.

Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, halafu Bunge likatunga sheria kuifuta haki hiyo, ilitegemewa mahakama kutumia mamlaka yake ya “checks and balance” kulia,nia Bunge haliwezi kutunga sheria inayokwenda kinyume cha katiba!. Mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?.

Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!. Yaani Bunge litunge sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kisha kipengele cha sheria hiyo batili kikachomekewa ndani ya katiba kwa mabadiliko yakatiba kwa hati ya dharura!. Mahakama Kuu inasema huu ni ubatili, Mahakama ya Rufaa inasema “hatuwezi kuliingilia Bunge!.

Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ukatufungua macho kuhusu political silent status za baadhi ya majaji wetu!. Kumbe baadhi ya majaji wetu nao ni makada wa vyama vya siasa!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama wakuu wa mhimili wa mahakama mara tuu baada ya kustaafu wanageuka makada!.

Wasalaam

Paskali
Uli kulielewa vema banndiko hili, lisomwe na Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
Kwa wale msiojua, kile kilichonikuta kwenye lile jambo langu, kinatikana na ubatili huu niliuzungumza hapa!. Kuna uwezekana mtu una jambo lako unalitaka, unalipania sana la Mungu anakunyima, unalikosa, unakubali matokeo kwasababu waliochaguliwa wamekupita sifa, ila kuumia kulikosa jambo lako unakuwa umeumia!. Kumbe kuna uwezekano, majanga mengine sio majanga, ni mapito!. Unapitishwa kwenye mapito ya majanga huku unachapwa mijeledi, kumbe ni kwa kupigwa kwako, unapigwa ili wengine waponywe, hivyo majanga hayo yakawa ni a blessing in disguise!.

Mungu Nisaidie Niyaweze yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
P.
 
Kwa wale msiojua, kile kilichonikuta kwenye lile jambo langu, kinatokana na ubatili huu niliuzungumza hapa!. Kuna uwezekana mtu una jambo lako unalitaka, unalipania sana la Mungu anakunyima, unalikosa, unakubali matokeo kwasababu waliochaguliwa wamekupita sifa, ila kuumia kulikosa jambo lako unakuwa umeumia!. Kumbe kuna uwezekano, majanga mengine sio majanga, ni mapito!. Unapitishwa kwenye mapito ya majanga huku unachapwa mijeledi, kumbe ni kwa kupigwa kwako, unapigwa ili wengine waponywe, hivyo majanga hayo yakawa ni a blessing in disguise!.

Mungu Nisaidie Niyaweze yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
P.
 
Kwa wale msiojua, kile kilichonikuta kwenye lile jambo langu, kinatikana na ubatili huu niliuzungumza hapa!. Kuna uwezekana mtu una jambo lako unalitaka, unalipania sana la Mungu anakunyima, unalikosa, unakubali matokeo kwasababu waliochaguliwa wamekupita sifa, ila kuumia kulikosa jambo lako unakuwa umeumia!. Kumbe kuna uwezekano, majanga mengine sio majanga, ni mapito!. Unapitishwa kwenye mapito ya majanga huku unachapwa mijeledi, kumbe ni kwa kupigwa kwako, unapigwa ili wengine waponywe, hivyo majanga hayo yakawa ni a blessing in disguise!.

Mungu Nisaidie Niyaweze yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
P.
Pole sana ndugu, hayo yote yatapita tu
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom