Mgombea huyu analindwa na nani jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea huyu analindwa na nani jamani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by asha ngedere, Oct 16, 2010.

 1. a

  asha ngedere Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ‘Uchafu' wa mgombea Sumbawanga watua kwa Makamba


  * Apelekewa barua, picha za Mhindi akifanyiwa unyama
  * AFORD, asasi za kiraia zataka CCM ichukue hatua

  Na Waandishi Wetu, Dar na Sumbawanga

  PICHA za mtu anayedaiwa kutekwa na mgombea Ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sumbawanga Mjini, Bw. Aeshi Khalfan Hilaly na kisha kuingiliwa na kundi la watu kinyume na maumbile zinadaiwa kutua mezani kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yussuf Makamba, imefahamika.

  Habari za kuaminika zimeeleza kwamba, taasisi ya AFORD inayoongozwa na Seneta Julius Misellya iliwasilisha picha hizo pamoja na barua yenye kumbukumbu namba AFORD/1/10/2010 ya Oktoba 5, mwaka huu ikilaani vitendo vilivyofanywa na mgombea huyo miaka miwili iliyopita.

  Katika barua hiyo, Bw. Misellya anasema kwamba wamepokea malalamiko kutoka kwa wazee waandamizi wa CCM pamoja na Umoja wa Wanawake Jimbo la Sumbawanga Mjini kuhusu tuhuma za mgombea huyo.

  "…Tunapenda kukujulisha kwamba, baada yakuona suala hili ni nyeti na linahatarisha amani na kuleta machafuko kisiasa, taasisi hii iliamua kutuma watafiti wetu ili kupata ukweli wa tuhuma hizo.

  "Watafiti wetu waliwahoji watu mbalimbali wakiwemo mapadri, wachungaji, viongozi wa misikiti, viongozi wa kimila, wazee wa CCM na jumuiya zake pamoja na watu wa kawaida," ilisema sehemu ya barua hiyo iliyonakiliwa kwa viongozi wa dini, wazee wa CCM Sumbawanga, Vyama vya siasa na taasisi za haki za binadamu.

  Misellya anasema katika barua hiyo kwamba, watu wote waliohojiwa walimlalamikia Bw. Aeshi kutokana na vitendo vyake vya ukatili, udhalilishaji unaokiuka haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kumpa mimba mwanafunzi (jina linahifadhiwa) na kumkatisha masomo.

  "…Mbaya zaidi, watafiti wetu walifanikiwa kupata picha za tukio la ulawiti aliofanyiwa (jina linahifadhiwa) mnamo Novemba 12, 2008 kwenye nyumba yake Block N eneo la Jangwani.

  "Kwa kuzingatia maadili ya viongozi wa kitaifa wakiwemo Wabunge, tunapenda kusema kwamba Bw. Aeshi hana sifa za kusimama na kuwakilisha Watanzania na hivyo taasisi inakuagiza kumuengua haraka na kumfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake… pamoja na barua hii tunaambatanisha hizo picha za aibu kwa ushahidi na utekelezaji," imeongeza barua hiyo.

  Taasisi zilizopewa nakala za barua hiyo ni Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste (PCT), Legal and Human Rights Centre (LHR), Mtume na Nabii Josephat Mwingira, Josephat Gwajima, Mchungaji Anthony Lusekelo, Sheikh Ali Basaleh pamoja na mwanasheria Mabere Marando anayetarajiwa kupelekewa wakati wowote.

  Seneta Misellya mwenyewe amelieleza gazeti hili kwamba taasisi yake bado inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la kumpachika mimba mwanafunzi na ikibainika basi watachukua hatua za kumfikisha mahakamani, kwani ni kosa la jinai

  "Tunataka mabadiliko yatakayoleta maendeleo, lakini hatuwezi kuchagua viongozi wasio waadilifu kushika nafasi nyeti kama hizi za ubunge, ni aibu na kwa hakika CCM wanapaswa kuchukua hatua za haraka, kinyume chake tutasimama majukwaani na kuhubiri machafu haya," alisema Misellya.

  Wachunguzi wengine wa mambo ya siasa wamekumbusha namna Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyofikia hatua ya kuwanadi wagombea ubunge wa upinzani mwaka 1995 baada ya wale wa CCM kuwa na mapungufu.

  "Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere aliwaambia wananchi wa mkoa wa Mara kutowachagua wagombea wa CCM waliokuwa wakituhumiwa kwa rushwa na kuua chama cha ushirika Mara, badala yake akawashauri bora wachague wagombea wa upinzani (NCCR-Mageuzi)," walisema.

  Naye Mchungaji Christopher Mtikila, amesema kitendo cha CCM kuendelea kumkumbatia mgombea huyo licha ya kashfa zinazomkabili kimeendelea kuishushia hadhi na kudhihirisha namna maovu yanavyofichuka ndani ya chama hicho.

  "Tunalaani vikali vitendo vya mgombea huyo, na nimemtumia ujumbe (Abdulrahman) Kinana mwenyekiti wa kampeni wa Kikwete kumwondoa mgombea huyo na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mara moja," alisema.

  Aidha, taasisi nyingine iliyojitokeza kulaani vitendo vya mgombea huyo ni ya Mbeya Regional Environmental Conservation Association (Mreca) ambayo nayo imevitaka vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa.

  Akizungumza na gazeti hili, ofisa wa taasisi hiyo Ambwene Mwamakula aliyefanya utafiti hivi karibuni mkoani humo, alisema kwamba pamoja na matukio hayo kufanyika siku za nyuma lakini kuna haja ya vyombo husika kuchukua hatua huku akishauri Chama cha Mapinduzi kutoa tamko badala ya kuendelea kumnadi kwenye kampeni.

  Alisema kwamba, anashangazwa ni kwa vipi vyombo vya dola, ikiwemo Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) havijamchukulia hatua licha ya kubainika kwa maovu aliyofanya mgombea huyo.

  "Suala hapa ni maadili na makosa aliyoyafanya. Kama kulikuwa na mazingira ya rushwa huko nyuma yanapaswa yasiangaliwe kwa sasa, bali tuangalie mtu huyu anataka kuwa kiongozi wa kitaifa atakayekuja kutunga na kusimamia sheria za nchi, ni sheria gani ikiwa zilizopo tayari amekwishazivunja?" alihoji Mwamakula.

  Mwamakula amesema, suala la kumpa mimba mwanafunzi ni kosa la jinai ambalo halipaswi kufumbiwa macho na mtu awaye yeyote huku akisema serikali imekuwa mstari wa mbele kusimamia Sheria ya Makosa ya Kujamiina ya mwaka 1998.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, kumekuwepo na mijadala mingi hata Bungeni kuhusu suala la watoto washule kupewa ujauzito ambapo Julai 11, 2007 baadhi ya Wabunge waliiomba Serikali kuwahasi wanaume wanaowapachika mimba wanafunzi ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea kushamiri nchini.

  Mbunge wa Lulindi, Bw. Suleiman Kumchaya (CCM), aliongea kwa uchungu Bungeni kutokana na mjukuu wake wa darasa la tano kupachikwa mamba ambapo alisema kwa vile maagizo mbali mbali ya serikali ya kuwachukulia hatua kali yanashindwa kutekelezeka kutokana na sheria iliyopo kutokidhi haja, njia ya kukomesha vitendo hivyo ni kuwahasi wanaume hao.

  "Mheshimwa Naibu Spika, mimi nikiwa ni mmoja wa waathirika wa vitendo hivyo, kutokana na mjukuu wangu wa darasa la tano kupachikwa mimba, nina uchungu sana na hasira na wanaume hao wanaofanya vitendo vya kinyama kiasi hicho," alisema.

  Alisema watu hao hawatakiwi katika jamii, hivyo suala la kuwahasi itakuwa ni njia pekee ya kuwakomesha watu wenye vitendo kama hivyo.

  Mbunge wa Kiteto, Bw. Benedict Kiroya Losurutia (CCM – sasa marehemu) alisema, serikali haina budi kubadili mtazamo juu ya watu wanaowapa mimba wanafunzi, na badala yake iwahasi ili vitendo hivyo viweze kuisha katika jamii.

  "Mheshimwa Naibu Spika, mimi na nafikiri dawa pekee ya kukomesha vitendo hivyo, ni kuwahasi watu hao kwa maana wanarudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike na wazazi wao," alisema.

  Wabunge wengine waliojadili mjadala huo ni pamoja na Jenister Mhagama Mbunge wa Peramiho (CCM), alisema maagizo mbali mbali yanayotolewa na serikali katika kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanaowapa mimba wanafunzi, yamekuwa kama wimbo wa taifa, na watu kuyadharau huku vitendo hivyo vikiongezeka siku hadi siku, hatua inayowarudisha nyuma wanafunzi wa kike kwa kukosa elimu.

  Bi. Susan Lyimo, Viti Maalumu (Chadema) alisema, wanafunzi wengi wanapewa mimba na wanaume wenye uwezo, wengi wao ni viongozi, wanasiasa wakiwemo madiwani na baadaye kuwatelekeza.

  Awali, Mbunge wa Ziwani (CUF) Ali Saidi Salum alikuwa ameshauri wale wanaowapa mimba wanafunzi wanyongwe hadharani na kisha maiti zao ziwekwe kwenye kioo maalum na kuandikwa: "Hawa ni wahalifu wabaya sana."

  Mbunge huyo alishangaa watu wazima kuamua kizini na watoto wa shule badala ya kuwasaidia, wakati kila mahala siku hizi kuna watu wazima waliokubuhu kwa shughuli hiyo.

  Naye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipata kusema Bungeni wakati akijibu maswali ya papo kwa papo Julai 10, 2008 kwamba serikali inatarajia kufanya sensa nchi nzima kuangalia ukubwa wa tatizo la mimba kwa watoto wa shule, tatizo ambalo alikiri kuwa ni kubwa.

  "Baada ya kukaa pamoja na kujadili tutaangalia kama sheria zetu ni legelege basi nazo tutazisawazisha, ili kukabiliana na tatizo hilo," alisema Pinda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema), aliyetaka kujua nini mikakati ya serikali juu ya watoto wanaopata mimba wakiwa shuleni.

  Aidha, Alhamisi Agosti 13, 2009, Waziri Mkuu Pinda alimwagiza Mkuu wa Mkoa Manyara, Bw. Henry Shekifu na Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo kuhakikisha kuwa wanasimamia suala la kusaka wanaume wanaowapa mimba watoto wa shule na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wakuu wa Serikali na Chama kutoka wilaya zote tano za mkoa huo, wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Hanang'.

  "Kuna tatizo kubwa la mimba katika shule za sekondari ambalo limeongezeka kutoka wanafunzi 42 mwaka 2005 hadi 170 mwaka 2008. Hili ni suala la kukemea sana. RC na Ma-DC nimeagiza muwafuatilie wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, akikamatwa baba mmoja akafungwa jela miaka 30, itakuwa fundisho kwa wengine," alisema.

  Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa alipata kusema Novemba 21, 2007 kwamba serikali ingewasilisha pendekezo ili watu wanaowapa mimba wanafunzi wakifungwa magerezani wachapwe pia viboko.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo baada ya kukerwa na ukubwa wa tatizo la mimba wilayani Mpanda mkoani Rukwa na kulizungumzia suala hilo kwa uchungu baada ya kuelezwa kuwa tangu mwaka 2007 uanze wanafunzi 246 wa shule za msingi na 82 wa shule za sekondari walikuwa wamepewa mimba.

  "Kuna watu hapa sijui wamelogwa, wakiona watoto wa shule yanatoka sijui manini," alisema Lowassa wakati akizungumza na wakazi wa tarafa ya Karema katika mkutano wa hadhara. "Jamani waacheni watoto wadogo wamalize shule, nawaagiza viongozi wa wilaya kuwakamata wote wanaowapa mimba wanafunzi, wafungwe kwa kuwa wanawakatili watoto haki yao ya kupata elimu."

  Wananchi wengi waliohojiwa mjini Sumbawanga wameonya kwamba tabia za kuchukua uamuzi wa kienyeji kwenye kesi za wasichana wanaopata mimba mashuleni zinapaswa kuachwa na kuitaka jamii kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwatia hatiani watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi hao na kuwafanya wasimame masomo yao.

  "Wapo wazazi ambao hupenda kufanya mazungumzo na watu wanaowapa mimba binti zao na hivyo kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika. Jamii tunapaswa kusimama imara kukemea mambo haya, na kwa hakika hata suala hili na huyu mgombea tunapaswa kulikemea na vyombo husika vichukue hatua, havijachelewa bado kwa vile yule binti yupo na hana mwelekeo wowote kwa sasa wa maisha yake kielimu," alisema Josephat Mwambije.

  SOURCE: DIRA YA MTANZANIA, OKTOBA 11, 2010.
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  duuuh kazi ipo
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  wasiwasi wangu hapa, wako wapi polisi kwenye sakata hili ambalo ni kesi ya jinai.........si kazi ya akina makamba kushughulikia kesi za jinai...........................
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nashangaa! hayo ni mambo ya kihalifu hao mitume na manabii :biggrin1: wanahusika vipi katika kuwashughulikia wahalifu?.kama nikweli hizo tuhuma basi hayo sio mambo ya kichama wala kadini, huo ushahidi upelekwe polisi.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni Tanzania hii hii tunayoishi?
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Crap!
  Hivi mtu wa aina ya Makamba kweli unaweza kumpelekea kesi ya kusikiliza? Hata hiyo CCM bado mna imania nayo? amatu kama huyu ni kumnyima kura...
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hiyo ishu ukiwapelekea polisi ni kuwapatia ulaji bila mtuhumiwa kuchukuliwa hatua. kwanza vinajulishwa vyombo vya kijamii kisha anakabidhiwa polisi ili wafanye kazi yao.
  polisi yenyewe ndo hiyo inawabambikizia watu kesi na madawa ya kulevya.
  kama kungekuwepo na vutuo vya UwT watuhumiwa kama hao wanapelekwa kule wakatahiriwe
   
Loading...