Mgombea CCM kutojipigia kura Arumeru Mashariki

mi mwenyewe lazima nikampe kura yangu jembe NASARI,nimejiandikishia USA RIVER
!VIVA CHAMA MAKINI
 
Sijui kama kuna upendeleo maalimu labda anaweza ruhususiwa ajipigie kura kwani mshkaji ganda lake linasoma mbezi,dogo kazi anayo kwakweli,haya bwana mdogo hebu tuthibitishie kweli meru ulikuja kwa ajili ya maziko tu?na sio home kama unavyotaka tuamini.nipo tayari kwa safari ya kwenda arusha kumpa nasari tiki,bonge la kampani tupo post graduate kama wanne wa makumira na wengine kibao kutoka dar moro na mbeya.

Hapo ndo nachoka kabisa kama watu watampigia kura maana yy mwenyewe hawezi kujipigia kura ss ww unampigia ya nn?
 
Ni kwamba wapiga kura wakiwa watatu (3) tu Siyoi, Pamela, na Joshua, bado Jo atashinda manake Pamela kajiandikisha kwingine Siyoi naye ndo hivo, hapo mwenye shahada ni Joshua peke yake, parua magamba.
 
Ni kwamba wapiga kura wakiwa watatu (3) tu Siyoi, Pamela, na Joshua, bado Jo atashinda manake Pamela kajiandikisha kwingine Siyoi naye ndo hivo, hapo mwenye shahada ni Joshua peke yake, Parua Magamba.

Eroo umenikumbusha. Huyu paramagamba kabudi miaka ya 1980 alikuwa mwandishi wa habari wa UHURU na MZALENDO! Siku ya mahafali ya CKD, Prof. Haroub Othman alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya sheria,na kuwa Mtanzania wa kwanza kuifikia ngazi hiyo. Basi PK,akiwa mwandishi wa habari, aliongoza kundi dogo la wapambe kunengua kumshangilia Haroub!
 
Sijui kama kuna upendeleo maalimu labda anaweza ruhususiwa ajipigie kura kwani mshkaji ganda lake linasoma mbezi,dogo kazi anayo kwakweli,haya bwana mdogo hebu tuthibitishie kweli meru ulikuja kwa ajili ya maziko tu?na sio home kama unavyotaka tuamini.nipo tayari kwa safari ya kwenda arusha kumpa nasari tiki,bonge la kampani tupo post graduate kama wanne wa makumira na wengine kibao kutoka dar moro na mbeya.

Masai ni kweli sioi akujiandikisha meru na wala aishi meru huku alikuja kwenye maziko tu.
 
tofautisha mambo; kumbuka katika siasa za Arumeru uenyeji unahusika pakubwa kuwaaminisha wapiga kura kuwa mgombea ni mwenzao sio mgeni mwenye maslahi binafsi
 
Waandishi Wetu, Arumeru
MGOMBEA wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Sioi Sumari ni miongoni mwa wagombea watatu ambao hawatajipigia kura katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumapili ijayo kutokana na kwamba hawakuandikishwa kupiga kura katika jimbo hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba mbali na Sioi wengine ambao hawatajipigia kura ni Abraham Chipaka wa TLP na Muhammada Abdallah wa DP ambao pia wamejiandikisha nje ya jimbo la Arumeru Mashariki.

Kwa mujibu wa taratibu za upigaji kura za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wagombea wanaweza kupiga kura ikiwa tu wamejiandikisha katika jimbo husika. Hata hivyo taratibu hizo hazimfungi mtu kugombea uongozi katika jimbo asikoandikishwa.

Taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambazo Mwananchi limeziona zinathibitisha kuwa Sioi, amejiandikisha kupiga kura katika kutuo namba 00007247 Mbezi Beach, Kata na Jimbo la Kawe, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

Hata hivyo mgombea huyo wa CCM alipoulizwa juzi na mmoja wa waandishi wa gazeti hili kuhusu mahali atakapopigia kura alijibu kwamba yeye (Sioi) atapiga kura katika kituo cha Akheri Shule ya Msingi, kata ya Akheri wilayani Meru.

Jana Sioi alifuatwa tena kuulizwa kuhusu suala hilo na alisisitiza kwamba; “Nitapiga kura Arumeru Mashariki”.

Taarifa za NEC katika daftari la kudumu la wapigakura lililotumika mwaka 2010, jina la Sioi siyo miongoni mwa walioandikishwa kupiga kura katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kwa kuwa hakuna marekebisho yoyote ambayo yamekwishakufanyika kwenye daftari hilo, basi mgombea huyo hawezi kupiga kura.

Kwa upande wake, Chipaka alipopigiwa simu na kuulizwa ni wapi atapigia kura alisema: “Kwa kweli sifahamu hadi sasa, ngoja kwanza niwasiliane na viongozi wangu ili tufahamu kuhusu suala hilo, nadhani baadaye nitakuarifu”.

Hata hivyo baadaye Katibu wa TLP wilaya ya Arumeru, Jumanne Zuberi, aliliambia gazeri hili kuwa, mgombea wao huyo hawezi kupiga kura kwakuwa alijiandikisha nje ya jimbo hilo.

“Nadhani mgombea wetu alipitiwa tu, hawezi kupiga kura hapa maana yeye alijiandikisha Arusha mjini ambako ndiko makazi yake yaliko licha ya kwanza ni mzaliwa wa Arumeru,” alisema Zuberi.

Naye Abdallah wa DP alithibitisha kwamba hataweza kujipigia kura kutokana na kwamba amejiandikisha Arusha mjini. “Mimi sitapiga kura, kwa sheria zilizopo ni kwamba siwezi kupiga kura nimejiandikisha mjini (Arusha) ndugu yangu, kwahiyo ndiyo hivyo,” alisema Abdallah.

Msimamizi wa uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi kwa upande wake alisema: “Siyo rahisi kufahamu wagombea wamejiandikisha wapi, sheria ziko wazi, kama mtu awe ni mgombea au mwingine yeyote hajaadikishwa katika jimbo hili, hawezi kupiga kura. Watakaopiga kura Jumapili ni wale tu waliojiandikisha katika Jimbo la Arumeru Mashariki”.

Wagombea wa vyama vingine vitano katika uchaguzi huo mdogo wamesemakwa nyakati tofauti kuwa watajipigia kura katika uchaguzi huo.

Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari alisema amejiandikisha katika Kijiji cha Kilinga kata ya Songoro na kwamba huko ndiko atakapopigia kura, huku mgombea kupitia AFP, Mzengo Adam akisema kuwa atapiga kura katika kituo cha Kisambale, Usa River.

Wengine ni mgombea wa SAU, Kirita Shaaban Moyo ambaye atapiga kura katika kituo cha Valeska, kata ya Makiba, mgombea wa UPDP, Charles Msuya atakayepiga kura kituo cha Consumers, Makumira kata ya Poli na Hamisi Kiemi wa NRA ambaye alisema kuwa atapiga kura katika Kituo cha Nsitony, Darajani kata ya Sing’isi.
:hand:
 
Walivowahuni weza Sioi akapiga kura, wakadai walifanya marekebisho binafsi kutokana na umuhim au uzito wa Sioi.

Maajab yataendelea
 
Kwasababu NEc ni mali yao atapiga kura.ukifuatilia vizuri unaweza kwenye familia ya marehemu Sumari ni yeye peke yake alijiandikisha meru.
 
Jana gazeti la Mwanachi liliripoti ya kuwa mgombea wa Magamba ya kuwa hata jipigia kura kwa kile kinachosemwa kuwa hakujiandikisha, Je ikiwa hali ni hiyo je hii si saini kuonesha ya kuwa mtu huyu hana uzalendo na Arumeru? Je hii haioneshi kuwa uchaguzi wa mtu huyu ulifanywa kibabe kutokana na nguvu za fedha walizonazo mafisadi kuliko uwezo wa mgombea?
 
Siku zote mkapa akionekana kwenye kampeni kama ilivyotokea kule igunga mtarajie uchakachuaji mkubwa sana..kulinda heshima ya mzee huyu kipara, ccm haiwezi kuacha upinzani ushinde.
 
Back
Top Bottom