Mgombea akamatwa kwa rushwa ya Sh500 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea akamatwa kwa rushwa ya Sh500

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ambitious, Mar 7, 2012.

 1. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Gazeti la Mwananchi,

  Tuesday, 06 March 2012 20:51

  MBIO za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki zimefikia patamu, baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Democratic (DP),Mohamed Abdalah Mohamed kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akituhumiwa kutoa rushwa ya Sh500.

  Kukamatwa kwa mgombea huyo kumekuja wakati mchakato wa uchukuaji fomu za kuwania jimbo hilo ukiwa unaendelea baada ya mgombea wa sita ambaye ni Siyoi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kujitokea kuchukua fomu hizo. Wakati uchukuaji fomu ukiendelea jana,habari zilizolifikia gazeti hili zilisema mgombea huyo wa DP na Katibu wa Uenezi na Mipango Taifa wa chama hicho Abdul Mluya walikamatwa eneo la Maji ya Chai wakati akitafuta watu wa kumdhamini.

  Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba mgombea huyo alikamatwa jana mchana wakati akimpa kiasi cha fedha mmoja wa wapambe wake, ili akachukue kitambulisho nyumbani kwa ajili ya kumdhamini.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, tukio hilo lilitokea saa 7:00 mchana baada ya maofisa hao wa Takukuru waliokuwa wamevalia nguo za kiraia kufika eneo hilo, kuwakamata na kupeleka katika Kituo cha Polisi cha Wilaya kilichopo Usa River kwa mahojiano zaidi.
  Mtuhumiwa akisimulia mkasa huo Mohammed alisema, Tukio hilo liliwaathiri kisaikolojia kwa kiwango kikubwa kwani litagharimu hata harakati zao kuendelea kuwatafuta wadhamini katika mchakato huo wa uchaguzi.

  Hata hivyo, alisema baada ya mahojiano ya saa kadhaa kituoni hapo na kujieleza kuwa alikuwa katika harakati za kutafuta wadhamini.

  Mkuu Polisi wa wilaya hiyo, aliwaruhusu kuendelea na mchakato huo wa kutafuta wadhamini baada ya kuchukua maelezo yao. “Nikiwa kituoni wakiwa wameshikilia nyaraka zetu tulizokuwa tunazitumia kutafutia wadhamini, OCD aliwasiliana na
  Msimamizi wa Uchaguzi, Trasias Kagenzi kuthibitisha kama kweli mimi ni mgombea, ndipo niliporuhusiwa kuendelea kutafuta wadhamini,” alisema Mohamed.

  Msimamizi huyo wa uchaguzi alithibitisha kukamatwa kwa mgombea huyo na kueleza sababu zake kuwa ni taarifa za raia wema waliopiga simu Takukuru baada ya kuona mtu akipewa fedha. "Baada ya kuongea na mgombea,aliniambia kuwa baada ya kumpata mtu wa kumdhamini katika eneo hilo,alimwambia kadi yake ya kupigia kura iko nyumbani, hivyo mgombea alitoa Sh500 ya Bodaboda ili aifuate ndipo alipokamatwa na Takukuru,” alisema Kagenzi.

  Hata hivyo, kwa upande wake Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Arumeru,Zawadi Ngailo alisema hakuwa amepata taarifa za kukamatwa kwa mgombea huyo hadi tunaenda mitamboni.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Rushwa ya shilingi mia tano ndiyo waliyoiona tu na kumkamata mtuhumiwa? Mbona tulizosikia awali ni nyingi tu sijui zimeishia wapi?
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah hawa jamaa wameanza tena na makashfa yao
   
 4. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kwamba sheria ni msumeno lakini hapa nchini kwetu kosa dogo ndio lenye kutiliwa maanani sana lakini kosa likiwa kubwa sana na linalohusu untouchables(vigogo) basi sio kosa tena.Takukuru wanatafuta kuonekana wachapa kazi hapo.
   
 5. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hilo linaitwa zengwe la kipindi cha uchaguzi.
   
 6. S

  Saas JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kuona taasisi ya kipumbavu kama hii...
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kiini macho tu hiki
   
 8. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Taasisi ni ya uma lakini watendaji ndani yake wako mikononi mwa watu binafsi.
   
 9. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kuna ule mchezo wa mitaani unaitwa karata tatu una viini macho na utapeli mwingi,hautofautiani sana na huu.
   
 10. W

  We know next JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi Hakimu akipelekewa kesi mbili za rushwa, moja ni ya sh. 500 na nyingine ya million 700. Hawa watu watapata adhabu sawa? Ikiwa kama ni hivyo, basi mahakama zetu zina uwalakini.
   
 11. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kwa wale wenye uelewa wa ndani kidogo kuhusu Sheria inayohusu suala la rushwa tunaomba watusaidie kuhusu hili swali muhimu.I've tried to do my homework lakini sipati maelezo yaliyo wazi kuhusu hili.
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ka ndo hivo kuna ambao wamepewa hadi rushwa ya sh 100 na wamekubali.
   
 13. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kuna corruption with na corruption without theft of public finances.
  Wakitaka kumaliza corruption wawe wakali kwa wale mafisadi wanao iba pesa ya Watanzania
  halafu ndio waje kumaliza hizi za honga. This culture is copied from the top!
   
 14. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sasa mtu anayepokea rushwa ya fedha taslimu Tsh 100 anaenda kununua andazi au ni mazoea ya kupenda kitu kidogo?
  Ila nimeona sahani za wali zikitolewa kama kichocheo kwa wapiga kura,lolote linawezekana Tanzania.
   
 15. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Kwa kuanzia, wale WATOA RUSHWA wa CCM walioripotiwa kwenye vikao vya Chama,wamechukuliwa hatua GANI? TAKUKURU wafunguke watwambie!
   
 16. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Asante kwa hiyo classification.Rushwa inayoathiri masilahi ya taifa inaamuathiri kila mtanzania kwa ujumla wake lakini kwa ufuatiliaji wangu wa kesi na tuhuma dhidi ya wala rushwa kama ulivyoonyesha awali wale wa corruption with theft of public finances are likely to get away with it.
  Ni ajabu kuona 'loopholes' ziko mahali ambapo ni sensitive sana kuliko mahali ambapo ni less sensitive as far as public welfare is concerned..
   
 17. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Corruption with theft ni rahisi kukagua sababu inachakachuliwa kwenye vitabu. Pia ni rahisi kumaliza kwa kupitia tume, sheriha, mahakama, body of ethics etc. Inatumia network ya watu wa karibu. you dismantle the network, strengthen independence of the accounting bodies and punish severily the culprits (of course hapa naongea haraka, kila case ina context ya kuzingatia kwa makini)

  Corruption without theft is harder to tackle sababu haitokei in offices, haiachi traces, na inategemea culture of impunity. Perpetrators perceive their actions as legitimate sababu wanaona the elite class is getting away with it.
  Ndio maana nilipendekeza hiyo ya kwanza iwe tackled first, na hii ingine itashindwa kuendelea sababu culture ya corruption itaanza kupungua na the general public will be willing to participate.

  Mfano: huyu mtu kahonga 500, ila watu wanaona sio mbaya sana sababu wale wanao iba more get away with it. Ila ingekua wanafungwa na kua prosecuted wote tungepiga kelele za 'zero tolerance'.
   
 18. 1

  19don JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  matumizi ya rasilimali za taifa kwa kukamata rushwa ya shilingi 500 huu ni wehu:bange::mvutaji:
   
 19. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Baada ya ku-digest hizo technical terms na huo mfano nimeipata perspective yako. Nafikiri kuna umuhimu wa kuingalia vizuri Anti-corruptio policy ya Tanzania kwa sababu naona kama inakosa uwiano wa moja kwa moja na Global Anti-corruption Policies ambazo ziko makini zaidi.
  Kwa mfano katika pekuapekua yangu nimekutana na kipengele cha 'Bribe Payers Index' ambayo inabainisha kitakwimu makampuni,wanasiasa na watu binafsi wanaotoa rushwa kwenye baadhi ya nchi kama vile Pakistan,India,France,Nigeria etc.
  Kuna global shift ya kubaini watoaji rushwa kwa sababu wao ndio chanzo halisi cha kuenea kwa janga la rushwa.Sisi bado tuko kwenye kuitegemea sheria yenye mapungufu ifanye kazi ya kuwakamata wapokea rushwa huku ikishindwa kuwafikia vizuri watoa rushwa.
  Halafu vile vimetego vya TAKUKURU hukamata samaki wadogo tu wale wazee wa wizi na rushwa ya kalamu kama ulivyoeleza mwanzoni wameteka system yote kuanzia Anti corruption agencies mpaka Judicial system.
   
 20. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Una haki ya kuita wehu kutokana na system ilivyoshindwa kutambua wapi pa kuanzia.
   
Loading...