Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
CCM inapeta kwa wabunge sita na kigezo cha idadi hiyo ni uwiano wa wabunge ndani ya bunge la jmt.
Inapokuja upinzani wanarundikwa kundi moja bila kuzingatia uwiano wa wabunge wa kila chama kwenye hilo bunge.
Hoja ya kuwa sheria inatamka watakuwepo wabunge kutoka chama tawala na upinzani siyo mlenda wa kutelezea na kukwepa kuwatendea sawa wapinzani kama walivyoitendea CCM kwa kubeza kuvitambua vyama kuwa ni tofauti na uhalali wao kuwepo bungeni hivyo basi kutoangalia uwiano wa kila chama kama walivyoitendea ccm ni ubaguzi wa waziwazi unaopaswa kukemewa na mahakama ya Africa mashariki.
Mfano tu chama kikuu cha upinzani nchini kikikosa wawakilishi wawili kwenye bunge la Afrika mashariki basi huo uwakilishi ni haramu.
Kama bunge litawabagua wapinzani na kutotumia utaratibu uleule uliotumika kuwapata idadi ya wawakilishi sita wa CCM na kupata idadi ya kila chama cha upinzani huo ni ubaguzi na mahakama ya afrika mashariki ikiombwa kukemea ukiukwaji wa EAST AFRICAN TREATY utakaofanywa na bunge la Tanzania itachukua hatua ya kutangaza zoezi zima lilikuwa batili.
Aina yoyote ya kutotendeana sawa ni ubaguzi na ubaguzi ni ukiukwaji wa katiba zote mbili na ya shirikisho la Africa Mashariki