Mgogoro wanukia NMB, NBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wanukia NMB, NBC

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PayGod, Jun 20, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mgogoro wanukia NMB, NBC Boniface Meena

  MGOGORO mkubwa wa wafanyakazi na manejimenti unafukuta chinichini katika benki mbili kubwa nchini NBC na NMB kuhusu mfumo wa malipo ambao wafanyakazi wanaulalamikia kwamba hauwanufaishi.Katibu Mtendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Fedha, Viwanda vya Uzalishaji na Biashara (Fibuca), Alquin Senga alibainisha hayo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano baina yake na wafanyakazi wa NMB na baadhi ya wafanyakazi wa NBC uliofanyika jana Dar es Salaam.

  Senga alisema hivi sasa wako katika majadiliano na menejimenti ya NMB na kwamba kuna mambo ambayo wameafikiana, lakini wafanyakazi wanadai mfumo wa malipo haueleweki."Suala la mshahara hatujaafikiana, lakini wafanyakazi wanacholalamikia ni suala la mfumo na siyo kiwango cha mshahara, kwa kuwa ni lazima kuwe na mfumo ambao utawasaidia wafanyakazi. Tukizalisha zaidi tulipwe zaidi," alisema Senga.Katibu huyo alisema wafanyakazi wanataka suala la mfumuko wa bei liwe sehemu ya mfumo wa malipo na suala la wageni kulipwa zaidi ya wazalendo liangaliwe upya."Wageni wanalipwa kuliko wazawa na wana elimu sawa na uwezo vile vile, lakini inashangaza analetwa mgeni afanye kazi ambayo ingefanywa na mzawa, hatukubaliani na hilo," alisema.

  Kwa upande wa NBC, Senga alisema katika benki hiyo kuna mgogoro mkubwa, hasa katika mfumo wa malipo ya mishahara, bonasi na ushirikishwaji wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi katika kufanya maamuzi."Viongozi wa chama wananyanyaswa na hili lisipotatuliwa mapema kutaibuka mgogoro mkubwa sana kwa kuwa kuna mgogoro wa chinichini tangu Desemba 2010," alisema.Alisema majadilano na menejimenti ya NBC yamekwama hivyo mgogoro unaweza kulipuka muda wowote kuanzia sasa."Hali ni mbaya NBC, na uongozi umefikia hatua ya kumsimamisha Rais wa wafanyakazi ndani ya benki hiyo,"alisema.

  Meneja uhusiano wa NMB, Shyrose Bhanji alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa malalamiko hayo alisema hana la kusema."Sasa hivi sina chochote cha kusema,"alisema.Mshauri wa mawasiliano wa Benki ya NBC, Robi Matiko akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, ghafla simu ilikatika na hakupatikana tena mpaka tunakwenda mitamboni.
   
Loading...