Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Source?!.. Hizo ni hisia, umbea au?????????????????????????????
 
Pamoja na mapungufu yake, CHADEMA wapo serious sana kumshughulikia yeyote anayekiuka miiko na taratibu za chama na taifa kwa ujumla. Hawa ndiyo wanaostahili kushika dola, maana kwa hakika hawatamvumilia fisadi. CHADEMA ni tofauti kabisa na CCM ambayo inaishi kwa kushabikia uenzetu na kulipana fadhila.

Naamini kama kampeni ya kujivua gamba ingekuwa iliendeshwa na chadema, ni dhahiri hakuna fisadi ambaye angesalia katika system. Hivi leo tusingezungumzia suala la mgao wa umeme, wala ukosefu wa maji Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi ambayo miradi yake imehujumiwa na watu wachache.

Tuiunge mkono CHADEMA. Wapo tayari kumpoteza mwanachama ili kulinda heshima na miiko ya chama chao na sheria za nchi. Hawana muda wa kumwangalia mtu usoni. Long live CHADEMA!
 
Subiri Xmas ukapate ujira wako wa pilau ya mchicha pale lumumba.
 
Results 1 to 30 of 101
 

Mkuu Mungu wangu akubariki kwa ukweli wako huo.
 

....ccm wangia karatu ...cm ..0 na ..ana Ngorongoro...Tembo ...wa...nusa....
 



..majangili yapiga hodi KARATU ....TEMBO... NA... PEMBE..... Wakibimbilia Serengeti sasa tembo........wanaongelelea ..ziwa Victoria..... kuelekea...... Nile

Source:
LUMBUMBA
 
R.B

Kuandika kuwa CHADEMA waanza kutimuana itakuwa ni umbea, unasemaje tunaanza wakati huo ndo mwendo wetu??? sisi tunauthubutu, watu wasioendana na itikadi za chama ni utaratibu wetu kuwamimina, tumeshatimua madiwani Arusha na maeneo mengine, unaposema tunaanza unamaana gani hasa????

Neno kuanza ungekaa nalo kwanza hadi ukiona CCM wametimua mtu ndo ulitumie mana wao hawana uthubutu wa kufukuza mtu anayeenda kinyume na maadili ya chama sababu chama chao hakina maadili, sisi hatuna kuremba, ukijichanganya tunakumimina uwe diwani au mbunge.

Neno waanza nadhan hukupaswa kulitumia kwa chadema sisi hizo ndo zetu mbona toka kitambo, we mean business, we need discipline???Hatujaanza leo.
 
Last edited by a moderator:
Kamwe hatuwezi kulea mafisadi na majangili kama chama cha magamba.
 
Kuna kila ulazima wa kuwashughulika wale watovu wa nidhamu ili kukiweka chama chao vzr

CDM pigeni mzigo
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI WA AWALI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, Desemba 15-16, 2012, katika Hotel ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, imemaliza kikao chake Desemba 16, usiku.

Pamoja na kwamba maazimio yote ya kikao hicho yatatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Desemba 18, 2012, huu ni ufafanuzi wa awali kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazowakanganya wanachama na Watanzania kwa ujumla, zilizoandikwa
tangu jana Jumapili na Jumatatu, katika baadhi ya vyombo vya habari.

Mbali ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea taarifa ya hatua kadhaa za utekelezaji wa maazimio yatokanayo na vikao viwili
vilivyotangulia, Kamati Kuu pia ilijadili hali ya siasa nchini, mchakato wa Katiba Mpya na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya mwenendo wa chama kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambapo ilijadili pia kasoro za utendaji wa viongozi wa chama katika Wilaya ya Karatu.

Kamati Kuu ilichukua uamuzi wa kusimamisha uongozi mzima wa Wilaya ya Karatu na kuweka shughuli za utendaji wa chama chini ya uangalizi wa Kamati Kuu mpaka hapo itakapotolewa maagizo mengine baadae.

Aidha, Kamati Kuu pia ilipokea na kujadili mwenendo wa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa taasisi za kiserikali wanaotokana na
CHADEMA, hasa katika masuala ya ardhi na maji Wilayani Karatu.

Kikao pia kilibaini kuwa taarifa zinazohusu masuala hayo ya maji na ardhi ni tofauti na namna zilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari.

Aidha kutokana na mjadala, iliazimiwa hatua kadhaa zichukuliwe, ambazo umma utaarifiwa katika tamko la Kamati Kuu litakalotolewa
kupitia waandishi wa habari.

Imetolewa leo, Desemba 17, 2012,
Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari
CHADEMA
 
heri chadema ikose jimbo au halmashauri lakini nidhamu inabaki ndani ya chama
 

Hiki ulichosema ndio hakipo CCM. Wananchi wanapenda kuona nidhani inadumishwa kwa wote wanaokengeuka, lakini serikali ya CCM imekuwa ni chaka la kutunza wahalifu, siku CCM watakapoanza kutumia fagio la chuma alilopewa raisi Mwinyi mwaka ule, CCM itarudi kwenye chati kwa haraka, bila hivyo CCM ndio basi tena
 
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, Desemba 15-16, 2012, katika Hotel ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, imemaliza kikao chake Desemba 16, usiku.

Pamoja na kwamba maazimio yote ya kikao hicho yatatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Desemba 18, 2012, huu ni ufafanuzi wa awali kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazowakanganya wanachama na Watanzania kwa ujumla, zilizoandikwa tangu jana Jumapili na Jumatatu, katika baadhi ya vyombo vya habari.

Mbali ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo kupokea taarifa ya hatua kadhaa za utekelezaji wa maazimio yatokanayo na vikao viwili vilivyotangulia, Kamati Kuu pia ilijadili hali ya siasa nchini, mchakato wa Katiba Mpya na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya mwenendo wa chama kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambapo ilijadili pia kasoro za utendaji wa viongozi wa chama katika Wilaya ya Karatu.

Kamati Kuu ilichukua uamuzi wa kusimamisha uongozi mzima wa Wilaya ya Karatu na kuweka shughuli za utendaji wa chama chini ya uangalizi wa Kamati Kuu mpaka hapo itakapotolewa maagizo mengine baadae.

Aidha, Kamati Kuu pia ilipokea na kujadili mwenendo wa utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa taasisi za kiserikali wanaotokana na CHADEMA, hasa katika masuala ya ardhi na maji Wilayani Karatu.

Kikao pia kilibaini kuwa taarifa zinazohusu masuala hayo ya maji na ardhi ni tofauti na namna zilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari. Aidha kutokana na mjadala, iliazimiwa hatua kadhaa zichukuliwe, ambazo umma utaarifiwa katika tamko la Kamati Kuu litakalotolewa kupitia waandishi wa habari.

Imetolewa leo, Desemba 17, 2012, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
 
Jana niliona uzi mmoja umeletwa na Ritz kuhusu mambo ya Karatu sikujua kama Ritz yuko ndani ya CDM!
 
Last edited by a moderator:
mkuu kajipange upya, mimi niko huku karatu hakuna kitu cha aina hiyo, mgogoro uliopo ni wa viongozi na wala si wakutafuna pesa, kwani wao ndo mkurugenzi wa halimashauri? Kmauulize mkurugenzi yeye ndo mwenye pesa,

mimi nashangazwa na nyie wanasiasa wa vyama hivi viwili ccm/cdm, ili mradi ukitetee chama chako nyote muko tayari kuiweka mhanga nchi yetu. Tusidanganyane uko mpasuko mkubwa sana katika kikao hichi cha cdm, wakubwa wengi akiwamo dr.slaa wanawapigia vifua mafisadi wa karatu. Na kuna wale majasiri ndani ya cdm wanosema, hata ikionekan harufu ya ufusadi popote au kwa mwanchama yeyote, basi ni lazima aonyeshwe mlango au achukuliwe hatua na kupelekwa mahakamani. Hamtaweza kuwatukana ccm kwa ufisadi na hali nyie muna protect mafisadi wano va ngu za kidini.
 

barida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…