Mgogoro waitikisa CHADEMA!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,611
Reaction score
6,720
MGOGORO mkubwa unakinyemelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuelezwa kuwa sekretarieti yake imekayakataa mapendekezo ya Tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo, ukiwamo wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu), ambayo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji unaelezwa kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Karatu uliko mradi huo walihojiwa jana, lakini akasema hapakuwa na mpango wowote wa kufukuzana.

"Ninachoelewa ni kwamba waliitwa wakahojiwa na kitakachofuata ni kupewa maagizo ambayo lazima wayafuate na atakayekiuka ndiye atakayefukuzwa," alisema Mwigamba.

Baadhi ya viongozi wa Chadema Karatu waliotarajiwa kuhojiwa jana ili kupata suluhu ya mgogoro huo ni pamoja na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu, Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini, Jubiless Mnyenye.

Viongozi wakuu wa Chadema hawakupatikana jana kwa kuwa muda mwingi walikuwa katika kikao hicho ambacho kilimalizika jana, huku ikielezwa kuwa taarifa rasmi kuhusu yaliyojadiliwa itatolewa leo.

Alipoulizwa kuhusu mgogoro huo, Msemaji wa Chadema Tumaini Makene alisema agenda za kikao hicho zilikuwa wazi na ziliainishwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi.

"Hakuna zaidi ya hizo na leo (jana), ni masuala ya Katiba Mpya. Kwenye yatonakayo, masuala mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya nchi yanajadiliwa nchi nzima kwa sababu yanatokana na vikao vilivyopita si Karatu pekee. Angalia usije ukalishwa matangopori," alisema.

Kumshinikiza Rais
Habari zaidi kutoka katika kikao hicho zinaeleza kuwa kamati hiyo imeazimia kuchukua hatua ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusimamia utekelezaji wa masuala ambayo yapo katika mamlaka yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.

Wengine ambao kimesema kinataka wawajibishwe ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.

Kamati hiyo pia imeazimia kuanzia Januari kuwa na operesheni kubwa ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), nchi nzima kushinikiza utekelezaji hatua za kinidhamu kwa watendaji hao na watuhumiwa wa ufisadi wa Fedha za Madeni ya Nje (EPA).

CHANZO: Mwananchi | Disemba 17, 2012

***************************

 
Sijui ni umbumbumbu wa mwandishi wa taarifa hii, sijui ni mtazamo wake wa kisiasa ama pengine ni udhaifu wake wa maadili na ithibati ya uandishi.

Ajabu kabisa kwa mhariri wa mwananchi kuruhusu kuchapwa kwa habari hii ambayo yaliyomo hayarandani na kichwa cha habari. sijaona huo mgogoro unaotishia kuigawa chadema, wala sijaona namna viongozi wanaotuhumiwa kufisadi mradi wanavyolindwa na viongozi wa kitaifa.

Napata mashaka sana na uandishi wa namna hii. msifikiri Tanzania inamilikiwa na waandishi peke yenu, wala msifikiri Tanzania ni nchi ya kufikirika. Tafadhali acheni ujinga wa kutoa taarifa skewed namna hii. Jitendeeni haki kwa kuandika taarifa zinazozingatia maadili badala ya kulazimisha fikra zenu kwenye mambo yasiyokuwapo.

Kuna ugumu gani kuandika habari kama zilivyo kama walivyofanya Mwanahalisi na Raia Mwema ama the Guardian?
 
Wanabodi.

Chama cha CHADEMA kimefanya ufisadi mkubwa na kukwamisha miradi mingi ikiwemo Mradi wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu) tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi hiyo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.

Mradi huo wa maji umeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambayo wanatajwa kufanya ufisadi ni Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa viti maalumu Cicilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini Jubiless Mnyenye.

SOURCE: MWANANCHI DESEMBA 17, 2012.
 
Mkuu kajipange upya, mimi niko huku karatu hakuna kitu cha aina hiyo, mgogoro uliopo ni wa viongozi na wala si wakutafuna pesa, kwani wao ndo Mkurugenzi wa halimashauri? kmauulize mkurugenzi yeye ndo mwenye pesa,
 
wamekusikia Ritz
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenye Red, naona unatafuta kuingiza siku mkuu, hivi kwa akili yako Mbunge anawezaje kula pesa? yeye ni mhasibu?
 
Naona bado unaandamwa na jinamizi la degree ya kubebwa pale Mlimani na Prof. Ibrahim Juma. Hili jinamizi litakutesa hadi kaburini!
 
Nilidhani wamekula fedha za umma kumbe ni kukwamisha mradi!
Ulipouliza wanasema sababu ya kukwamisha ninini, maana usilete habari zenye kiwiliwili bila kichwa!
 
hapo kwenye red, naona unatafuta kuingiza siku mkuu, hivi kwa akili yako mbunge anawezaje kula pesa? Yeye ni mhasibu?

cdm si ndo wanaongoza halmashauri na ndio wenye maamuzi mana katika halmashauri madiwani ndio wenye mamlaka ya mwisho....sasa hao wamekula fedha za miradi.....
Tulitegemea cdm mtakuwa mfano wa kuungwa katika halmashauri za wilaya mnazoziongoza lakini mumeonhyesha uzaifu mkubwa kuwa hakuna kitu ni maneno maneno tu ..... Halmashauri tu inawshinda je mtaweza ongoza nchi??????.......
 
teh teh teh...unajua akili za baadhi ya great thinkers wetu zimepata dege dege, lol! Ufisadi ni tatizo kubwa kuliko linavyoelezwa hapa. Sisi tusio wapambe wa chama chochote ila nchi yetu ufisadi si kitu cha kuletea mizaha mizaha maana kinachelewesha maendeleo.
 
Hapo kwenye Red, naona unatafuta kuingiza siku mkuu, hivi kwa akili yako Mbunge anawezaje kula pesa? yeye ni mhasibu?

chasha,
Kwa hiyo unataka kutuambia uwezi kufanya ufisadi mpaka uwe mhuasibu?
 
Last edited by a moderator:
Uwakili unakushinda,kazi kudandiadandia hoja zisizo zako.Una kesi hata moja uliyowahi kumwakilisha mteja wako Mahakama yoyote tangu uwe Wakili? Kutwa kushinda JF kupiga porojo.Kazi anshindwa mdingi ndio uweze wewe...mwangalie kwanza na ukilaza wake!
 
Nenda kamwambie nape tayari umeshaandika kwenye jf.Utumwa mbaya sana!!
 

ww bado unaliamini gazeti la Mwananchi, hili nalo siku hizi nadhani limenunuliwa na magamba, haliaminiki tena. tafadhali waambie wlete ushahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…