Nakubaliana na mapendekezo ya Balozi Mpungwe kwamba ndugu zetu wa Znz wanahitaji mpatanishi ili kuwasuluhisha kutokana na mgogoro wao wa kihistoria na kisiasa.
Kama kuna watu wanaopaswa kusikilizwa basi ni Balozi Mpungwe. Huyu alikuwa kati wa washiriki wakuu wa mazungumzo ya amani ya Rwanda yaliyozaa mkataba unaoitwa Arusha accord. Kwa hiyo ni mtu mwenye uzoefu.
Lakini sikubaliani na Balozi Mpungwe anaposema tuwatumie wazee wastaafu wa hapa Tanzania. Wastaafu tulio nao wenye hadhi ya kutatua mgogoro huo wote ni wanachama wa CCM. Hiyo inawaondolea sifa kuu kwamba msuluhishi wa mgogoro wowote ule ni lazima aaminike na pande zote na asiwe na historia ya mahusiano ya karibu na upande mmoja ktk mgogoro anaotarajiwa kuusuluhisha.
Kwa kuangalia hapa Afrika na hata nje ya Afrika, nadhani Koffi Annan na Luis Moreno-Ocampo wanaweza kuwasaidia ndugu zetu wa Zanzibar kuondoka ktk mkwamo wa kisiasa na kijamii unaondelea nchini kwao.