Mgogoro wa madaktari, RAIS yupo wapi?

consigliori

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
392
89
Ndugu wanajanvi,

Binafsi sijelewi kwa nini rais wetu hajasema chochote kuhusu mgogoro huu. Mimi nilidhani hili ni jambo kubwa ambalo lilitakiwa kushughulikiwa kwa haraka, lakini inaonekana sivyo analvyoliona rais wetu. Hii inanifanya nishindwe kumuelewa huyu raisi ambaye huonekana kwenye misiba, hutembelea wagonjwa hospitali, lakini katika hili yupo kimya kabis!
 
Mkuu kifupi huyu mzee inaonekana amesha chemka, sio hili la mgomo wa madaktari tu, yapo mengi sana kayanyamazia. Ukweli ni kwamba mkuu hana hoja. Kama kungekuwa na mashine ya ku-detect mawazo ya watu katika ubongo, nadhani kwa huyu bwana ingekuwa inasomeka "natamani kipindi cha utawala wangu kiishe hata leo...!". Ngoma iko maji ya shingo hii...
 
Ndugu wanajanvi,

Binafsi sijelewi kwa nini rais wetu hajasema chochote kuhusu mgogoro huu. Mimi nilidhani hili ni jambo kubwa ambalo lilitakiwa kushughulikiwa kwa haraka, lakini inaonekana sivyo analvyoliona rais wetu. Hii inanifanya nishindwe kumuelewa huyu raisi ambaye huonekana kwenye misiba, hutembelea wagonjwa hospitali, lakini katika hili yupo kimya kabis!
Usiulize rais yuko wapi ... uliza wananchi wa Tanzania wapo wapi? Inatakiwa wa-mvurumishe kwa sababu yeye anaoneka haguswi na vifo vinavyotokea kwa sababu sio watoto au ndugu zake wanakufa. Wa kulaumu kabisa na wananchi.. wapo wapi?
 
Watanzania tulivyo! Na 2015 tutampa u rais mtu wa kutoka chama hichohicho
 
Back
Top Bottom