Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,939
Mkuu unaongea kwa Jazba sana hakuna sehemu mleta mada ambapo amesema ameoa na anafamilia yake au ana watoto ila nilichoelewa kijana bado anasoma Chuo... Kama nimepitwa mahala nikumbushe..Kasema ana mke na watoto, hiyo ndio familia yake kwa sasa. Aachane na habari za kwao.
Sawa, nimeona. Ila km keshakuwa mtu mzima afanye yake tu yanayomhusu.Mkuu unaongea kwa Jazba sana hakuna sehemu mleta mada ambapo amesema ameoa na anafamilia yake au ana watoto ila nilichoelewa kijana bado anasoma Chuo... Kama nimepitwa mahala nikumbushe..
Nilidhani Ungemshauri akawa karibu na Baba Yake Mzazi au Kumuuliza Mama Yake kwanini Baba yake Mzazi alimtelekeza au ilikuwaje mpaka akawa chini ya huyu baba mlezi au kwa nini asiendee kutambuliwa kule kwa kuwa huku aliko hata urithi wa mali hatapewa zaidi ya hiyo elimu aliyosaidiwa na huyo Mzee unayemkashfu.Sawa, nimeona. Ila km keshakuwa mtu mzima afanye yake tu yanayomhusu.
Wadau wengine wameshamshauri hayo.Nilidhani Ungemshauri akawa karibu na Baba Yake Mzazi au Kumuuliza Mama Yake kwanini Baba yake Mzazi alimtelekeza au ilikuwaje mpaka akawa chini ya huyu baba mlezi au kwa nini asiendee kutambuliwa kule kwa kuwa huku aliko hata urithi wa mali hatapewa zaidi ya hiyo elimu aliyosaidiwa na huyo Mzee unayemkashfu.
Forgive and forgetUmenena jambo mkuu.
Yes ananipenda na muda mwingine nahisi ananipenda kwa condition fulani tu, ila sio ule upendo Wa baba na mtoto.
Nafikiri ni kwa sababu ya kuja kumsaidia tu baadae, akiishiwa nguvu, ndio maana anakuwa anawekeza kama vile anawekeza kwenye asset tu, sio father and son relationship.
Ilikuwa ni miaka hiyo kukiwa na ule utaratibu wa kuweka kishika uchumba kama ng'ombe ili binti akimaliza shule aoelewe hivyo basi wazee walikubaliana ng'ombe ikawekwa kama kishika uchumba Ila alipomaliza shule hakupenda kuolewa na baba mlezi, ndipo alichagua kuolewa na baba mzazi, kwa maana tayari ujauzito ulikuwa umeshapatikana.Mleta mada aje aeleze vizuri kuwa Mama yake alimhadithia kuwa alibeba mimba ya nje baada ya kuolewa au alikuja na mimba yake???
Nimetolea ufafanuzi kidogo kwenye post namba 92.Ila Mkuu tumuulize kwanza huyo Mtoto Je Mama yake alimwambia kuwa alibeba mimba yake ya huyo mwanaume mwingine akiwa na huyo baba mlezi au aliolewa akiwa ameshazaliwa. Usije ukatokwa Povu kumbe kosa ni Mama na kwa kosa hilo likawa limemkwaza sana au hujui kuwa alibambikiziwa pia na amekuja kujua kuwa kijana siyo mtoto wake baada ya kuwa ameshazaa hao watoto wengine... Usiwe mwepesi wa kuropoka Mkuu
Mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako, kuna comment namba 92 nafikiri majibu ya maswali uliyopata wakati unasoma yapo hapo.Kwanza pole sana kwa changamoto hizi na hongera kwa kufunguka ili uomba mawazo kwa wengine, ila sikiliza na kisha tafakari kwa 'Ya Kuwambiwa Changanya Na ya Kwako"
Kama nimeelewa vizuri ni kwamba wewe ni mtoto wa kwanza kwa mama yako, maana yake mama yako alikuzaa kabla ya kukutana na huyu baba yako mwenye tabia ya ukali, matusi na kupiga. Nisahihishe kama nimekosea. Napata shida kuelewa kosa la mama yako liko wapi hapo kama alikuzaa kabla ya kukutana na huyu baba wa sasa. Naweza kuelewa kwamba labda amekulea akijua kwamba wewe si mwanawe, labda hili ndilo linalompa hasira kwa kiasi fulani.
Katika vitu vilivyonisikitisha hapa ni tabia ya huyu baba yako kuendekeza vipigo kwako na mama yako. Siku zote nimekuwa nikisema kupiga hakusaidii bali kunajenga chuki ya kudumu na usugu wa muda mrefu. Wote wenye tabia za kupiga ni dhaifu, wajinga na washamba. Ona sasa wewe ulivyoathirika kwasbababu ya vipigi visivyokwisha.
Ushauri
1) Halijalishi amekufanya nini, pamoja na vipigo na matusi yote aliyokufanyia huyu anabaki kuwa NDIYE BABA YAKO. Pamoja na mapungufu yote aliyonayo anabaki kuwa baba yako. Huyu ndiye aliyekulea, aliyekusomesha, huyu ndiye mwenye 'bond' na wewe, hivyo ndiye baba yako. Kuwa baba ni zaidi ya kumpa mtu mimba. Kumbuka muda wote huu umekuwa ukijua kwamba huyu ndiye baba yako, kwahiyo haijalishi kwamba eti kuna baba mwingine, huyu ni baba yako.
2) Inaonekana ana hasira kutokana na mambo yaliyotokea huko nyuma au hakujua jinsi ya kukabiliana na msongo huo hivyo ikabidi atembeze vipigo, hivyo MSAMEHE, endelea kumheshimu, ila jiweke naye mbali. Kama hali yako kiuchumi iko vizuri siku moja moja muunge mkono/msaidie kwa kiasi unachoweza ila usimtupe kwa kweli msamehe bure.
3) Usibabaike kwa kumkimbilia huyu baba uliyeambiwa na mama yako kwamba (ETI) ndiye baba yako halisi. Jipe muda, utafakari na ufanye utafiti nini kilipelekea kuweza kujua/kuwa na baba yako hadi imefika huku ukubwani. Huyu ni baba lakini huna 'bond' naye, kwa hakukulelea na hujui kwa nini hakukulea!! Laiti kama huyu baba yako (mpigaji) asingikuwa mnyanyasaji/mpigaji kama alivyo leo, si ajabu usiingehangaika wala kujulishwa kwamba kuna baba yako mahali, ila hali hiyo imechangiwa na ukali wake hadi wewe kuhoji. Kaa mbali kwanza usilazimishe kumuona baba yako haraka kihivyo, hoji zaidi tafuta ukweli wa nini hasa kilichotokea.
4) Pamoja na changamoto zote hizi zilizojitokea kuna funzo kubwa sana hapa kwako na wale wote wanaoifahamu hadithi yako hii. Kwamba utakapojaaliwa kuwa na familia yako usirudie makosa waliyoyafanya 'baba zako' wote wawili, hasa usiige kabisa tabia ya kupiga, kudhalilisha na kunyanyasa watoto wako au mkeo.
Nimekupata, pole kwa changamoto MSAMEHE nadhani ana hasira za muda mrefuMkuu nashukuru sana kwa ushauri wako, kuna comment namba 92 nafikiri majibu ya maswali uliyopata wakati unasoma yapo hapo.
Kwa kifupi ni kwamba alikwenda pale na ujauzito mkubwa kabisa, ambapo hata yeye alifahamu fika sio wake.