Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Kwa kuwa mama alishakuonyesha baba yako nakushauri wasiliana na shangazi (dada wa baba halisi )Zifanyike taratibu za kukupokea rasmi.
 
Mama ana kosa gani?

Hivi mkuu ukikutana na mwanamke ambaye tayari ana mtoto ukakubali kumwoa na kuahidi kulea mtoto, halafu ukajenga chuki na huyo mtoto, nani atakuwa na makosa?
duh kumbe alimkuta mama ana mtoto tayari mie nilijua alichapiwa wakati yuko na mama yako kwenye ndoa samahani sana naondoa comment yangu hapo juu. Ukutoa maelezo ya kutosha
 
Mama ana kosa gani?

Hivi mkuu ukikutana na mwanamke ambaye tayari ana mtoto ukakubali kumwoa na kuahidi kulea mtoto, halafu ukajenga chuki na huyo mtoto, nani atakuwa na makosa?
Msome vizuri huyo ngoma ilibambikiwa juu kwa juu mpira ukaitwa kati kwa goli la mkono
 
Umejieleza vizuri sana kwa kiswahili fasaha... mpaka ulipokuja kukosea ulipoweka kimombo...

Wakati nakupa pole kwa yaliyokusibu na kukushauri utumie busara kwenye maamuzi yako, napenda kukushauri siku nyingine usiandike "he do not appreciate" bali "he does not appreciate"
 
Msome vizuri huyo ngoma ilibambikiwa juu kwa juu mpira ukaitwa kati kwa goli la mkono

Hajawa wazi juu ya hilo mkuu, ila on normal circumstances first born akiwa siyo wa kwenye ndoa anakuwa ni wa kuja naye.
 
Achana nae live ur life broo!

Ana hasira na hvyo we only wa kiume halafu sio wake!
Tena muache tu
 
lizee ni mzee mpuuzi mwenye chuki za kijinga,ni mzee anayejiona yeye ndo mwenye nguvu sana. Kifupi ni mzee asiyejielewa
Wewe unaweza leo Mtoto ambaye Mke wako amezaa nje ndani ya Ndoa? Sema ukweli usiwe mnafiki......
 
you the best.....mheshimu, mpelekee zawadi ikiwezekana......msamehe... wapende wadogo zako......songa mbele maisha matamu sana......jipendekeze pia kwa babako halisi....uwajue nduguzo....huko ndo kwenu
 
Wewe unaweza leo Mtoto ambaye Mke wako amezaa nje ndani ya Ndoa? Sema ukweli usiwe mnafiki......

Hili swali ni moja ya maswali ambayo jibu utakalolitoa kabla hujakutana na hilo swala ni tofauti na utakachofanya ukikutana nalo.

Ni sawa na kuulizwa, ukijua mke wako anachepuka utamwacha?
 
Pambana usepe ukaandae maisha yako.
 
Msimlaumu huyo mama kuchepuka pengine alikuwa single mother akaolewa btw tanzania wengi wetu uzao wa kwanza ni wa nje ya ndoa na sababu hiyo madhara tunayapata watoto km hivyo kunyanyasika na kutokupata upendo unaostahili kwa wazazi mwisho wa siku ndo hivyo kisaikolojia huwi vizuri bro hauko peke yako wengi tupo km wewe ni vile mambo mengine huwezi sema tunaumia ndani kwa ndani pole sana ila ishi maisha yako potezea km huna baba maana yaelekea akikuona anapata hasira na chuki juu yako shukuru mungu upo hai
 
Wewe unaweza leo Mtoto ambaye Mke wako amezaa nje ndani ya Ndoa? Sema ukweli usiwe mnafiki......
waswahili wanasema kitanda hakizai haramu. Kama utagundua mtoto si wako na amezaliwa ndani ya ndoa Una chaguo moja Kati ya mawili KUMKUBALI au KUMKATAA yote sahihi. Lakini kumtesa,kumpiga na kumchukia huyo mtoto sio sahihi na ni dhambi maana yeye hana kosa.
kwanza Hilo lizee kinaonekana lioga na limeshikwa na mkewe Kama alijua si mwanae kwa nini asingempa talaka mkewe?

Binasfi Mimi ningechukua uamuzi huu. Ningempa talaka mke wangu na kubaki na wanangu akiwemo na huyo ambaye si mwanangu. Ningewalea kwa upendo wote wawili na Kama angefikisha umri wa kujitegemea basi ningemweleza ukweli wote Ili aamue la kufanya.
Mungu ana makusudi yake huyo mtoto kuzaliwa kwenye familia hiyo.
 
Mkuu umeoa au Unatarajia Kuoa? Ulishawahi kufanyiwa mwanamke wako Kwenye mahusiano na ukajua????
 
Asante sana mkuu
 
Mkuu umeoa au Unatarajia Kuoa? Ulishawahi kufanyiwa mwanamke wako Kwenye mahusiano na ukajua????
ndio nimeoa mkuu,sijajua kama nimewahi kusalitiwa na mke wangu au la lakini muhimu nimeshamwambia wazi kuwa SIKU NIKIGUNDUA ANANISALITI AU ALINISALITI BASI HAPO HAPO NDIO MWISHO WETU HAIJALISHI ALINISALITI LINI AU NA NANI. Ukitaka kuishi na mwanamke ishi nae kwa msimamo ajue kuwa muda wowote akienda wrong (akikusaliti) basi ndio mwisho wenu.
Tumeshuhudia wanaume wenzetu wakijiua kwa sumu na kujinyonga kisa usaliti. Usaliti unauma ndugu na hamna wa kuadhibiwa kwa usaliti zaidi ya yule aliyekusaliti(mwanamke) usimuadhibu mwingine yeyote wala usijiadhibu wewe. Kumbuka mwanamke sio ndugu Ni rafiki tu na kama ujuavyo undugu haufi ila urafiki unakwisha kwa hiyo ukioa ujue kuna kuacha.
 
Aisee pole sana,nikiyafikiria haya huwa nafikiri kubaki mwenyewe mpaka mwanangu atapokua mtu mzma na kujitambua inauma sana mtoto kufanyiwa vtendo kama hivo kama kosa n la mama kuzaa kabla ya ndoa na bas mtto hayastahili hayo, daah pole mkuu and msamehe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…