Mgogoro Wa Darfur "Sudan" Una Mkono Wa Magharibi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro Wa Darfur "Sudan" Una Mkono Wa Magharibi?

Discussion in 'International Forum' started by X-PASTER, Jan 26, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mgogoro Wa Darfur "Sudan" Una Mkono Wa Magharibi?

  Sudan inakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu kwa mapana na marefu ya nchi yake. Nadharia ya fitina, kwa vyovyote vile, ndiyo inayoichimba nchi hiyo. Ni ukweli ambao mtu hapaswi kuukataa kuwa Taifa la Sudan linakabiliana na awamu mbaya mno ya historia yake katika Jimbo la Magharibi la Darfur ambako, hadi sasa zaidi ya watu 50,000 wameripotiwa kufa kutokana na vita na maradhi.

  Kwa mujibu wa makadirio ya Umoja wa Mataifa, vita hivyo vimewatimua kwenye makazi yao zaidi ya watu 600,000 tangu mwezi Februari, mwaka 2003 wakiwemo watu 200,000 waliokimbilia nchi jirani ya Chad.

  Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Mustafa Uthman Ismail amezipinga vikali takwimu hizo za Umoja wa Mataifa, akisema kuwa zimezidishwa mno, mara kumi ya takwimu halisi. Alisema kuwa mgogoro huo wa muda mrefu katika eneo la Darfur umesababisha maafa ya takriban watu 5000. Kati yao 456 walikuwa ni askari Polisi.​
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Vita mjini Darfur

  Vita hii, kwa kifupi, inawahusisha Waarabu na Waafrika, wafugaji na wakulima, Kaskazini na Kusini na kwa undani wake, hivi ni vita vya ardhi na maji. Tatizo, kwa ujumla, ni la kijamii na kiuchumi. Tatizo hili, kwa kiasi fulani, limechochewa na baadhi ya vyombo vya habari, vikiliezea kama ni tatizo la ubaguzi.
  Huenda lengo la vyombo hivyo ni kuitikisa serikali ya Bashir na kusababisha hamkani nchini humo. Jambo hili laweza kuonekana katika mazingira ambayo rasilimali ya mafuta imegundulika katika mkoa wa Darfur ambao hivi sasa ni kitimoto kwa kile kinachoangazwa kwetu na mitandao ya Magharibi yaani mgogoro mkubwa wa wanadamu.

  Hakuna hata mtu mmoja anayezungumzia chimbuko la chuki ya ubaguzi ambayo ilianza tangu enzi za ukoloni. Waingereza, kwa hila yao ya kupoteza hamasa ya utaifa, walitumia mbinu yao kongwe ya ‘wagawanye-uwatawale’ baina ya Kaskazini na Kusini kama vilevile walivyofanya kati ya Wahindu na Waislamu nchini India kabla ya uhuru, mbinu ambayo imeleta athari kubwa hadi leo.

  Isitoshe, Sudan ni nchi inayopakana na nchi tisa jambo ambalo pia linailetea tatizo. Nchi zinazoizingira Sudan ni Misri, Libya, Chad, Congo, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia na Eritrea. Jamii nyingi za kikabila zimesambaa katika pande zote mbili za mpaka ambapo tatizo lolote la nchi mojawapo husambaa kutokana na maingiliano ya kikabila.

  Mathalani ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe nchini Chad katika miaka ya themanini, ulileta mtikisiko katika eneo la Darfur Magharibi, ukazidisha mivutano kati ya makundi ya makabila ya wa-fur na wa-Zaghawa.

  Takribani asilimia 40 ya Waislamu weusi, kijamii, walijihisi kuwa na udugu wa nasaba na makundi fulani ya nchini Chad kuliko hata yale ya mjini Khartoum. Kosa alilolifanya Rais Umar Bashir na wenziwe waliomtangulia ni lile la kushindwa kuutafiti mgogoro huo, jambo ambalo, kinyume chake, limewafanya weusi waitilie shaka dhamira ya serikali yake.

  Na kwa hivyo, palipotokea janga la ukame miaka ya karibuni sanjari na ufinyu wa maeneo ya malisho ya mifugo kutokana na kupanuka kwa Jangwa la Sahara, uhasama ukazidi kuongezeka ambapo wafugaji, wengi wao wakiwa Waarabu, na wakulima ambao takribani wote ni Weusi, wakavutana kunyang’anyana rasilimali hizo zilizopungua.

  Hata kama serikali ya Bashir haikuchochea mvutano huo bado, kwa kweli, ilishindwa kubaini wapi ulikokuwa ukivumia upepo. Lakini Rais Bashir kakiri kuwa, huu, kimsingi, ni mgogoro wa kikabila kutokana na mvutano wa ardhi na maji kati ya wafugaji na wakulima.

  Hata hivyo, vyombo vya habari vya Magharibi vinaupa mvutano huo sura tofauti kwa kuonesha kuwa ni mvutano kati ya Kaskazini ya Waarabu na Kusini ya Weusi.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mfumo wa Makabila.

  Ikiwa na idadi ya watu milioni 34, Sudan ina asilimia 70 ya Waislamu na aslimia 5 ya Wakristo. Waliobaki ni wapagani. Kuna makabila 500, kati yao, makabila 85 yana nasaba yao ndani ya Darfur ambayo ina takribani watu milioni 4.

  Makabila yenye nguvu ni Fur, Zagawa na Masaliyt. Waarabu ndio wengi wakiunda takribani asilimia 49 ya idadi ya watu, na wengi wanakaa Sudan Kaskazini. Eneo la Kusini, kwa kiasi kikubwa, linakaliwa na Waafrika weusi na jamii za watu wachache wakiwemo Wanubi.

  Dafur iko upande wa Magharibi wa Sudan. Takriban asilimia 60 ya wakaazi wake ni wakulima. Kabila kubwa ni Fur. Wa-fur ambao ni wakulima, wanakalia ukanda wa kati wa eneo hilo, ikiwa ni pamoja na eneo la Jebel Marra Massif.

  Vilevile katika kanda hii ya kati wapo wapo watu wasio Waarabu, nao ni wa-Masaliit, wa-Berti, wa-Bargu, wa-Bergid, wa-Tama na wa-Tunjur. Wote hawa ni wakulima wa kudumu.

  Mgogoro wa Darfur, inayopakana na Chad, ulianza Mwezi Aprili, mwaka 2003, pale makundi ya waasi weusi yaliposhambulia jeshi katika eneo la El Fasher, ambao ni mji mkubwa wa Dafur Kaskazini, yakikifikisha kileleni kile kipindi cha mvutano.

  Makundi mawili ya waasi JEM (The Justice and Equality Movement) na SPLA (Sudanese People’s Liberation Army) ambayo ndiyo yaliyoendesha mashambulizi hayo, yakajinadi kuwawakilisha wa-Dafur weusi, yakiishutumu serikali kwa kuwakandamiza Weusi na kuwapendelea Waarabu.

  Ili kudhibiti uasi huo, serikali ya Sudan imeripotiwa kuwasaidia wanamgambo wanaoitwa Janjawiyd, jina ambalo maana yake halisi ni askari wa farasi, ingawaje wanamgambo hawa wamefanya mambo kuwa mabaya mno kwa serikali ya Sudan kwani wamekwenda mbali zaidi ya kudhibiti uasi na kujiingiza katika kampeni ya vitendo vya uhalifu dhidi ya raia.

  Serikali ya Sudan inakanusha kuwapa silaha wanamgambo hao. Badala yake, inashikilia kuwa imepeleka idadi kubwa ya askari polisi kuwalinda raia wa Darfur dhidi ya Janjawiyd. Lakini hii haikutosha kuwaridhisha viongozi wa Magharibi wanaoitaka serikali kuwadhibiti Janjawiyd.

  Hii pia iliweza kuonekana katika mlipuko mwingine wa vita katika eneo la Kusini linalopakana na Uganda ambako vita kati ya serikali na SPLA iliweza kusitishwa mwaka 2003 lakini hiyo ni baada ya kugharimu maisha ya watu milioni 2 kwa kipindi cha miongo miwili.

  Picha ni ya kutia shaka katika eneo hili. Ambako takribani watu milioni saba ni Wakristo. Joseph Kony, Mkristo mwenye msimamo mkali, aliendesha vita dhidi ya Museven akitokea Sudan. Nayo Uganda ikaisaidia SPLA kuishughulisha kijeshi serikali ya Sudan.

  Hadi katikati ya miaka ya 1990, SPLA iliyokuwa ikiongozwa na John Garang, Afisa wa zamani wa Jeshi la Sudan, ilidhibiti sehemu kubwa ya eneo la kusini na ikadhibiti miji mingi muhimu.

  Inahofiwa kuwa Mgogoro wa Darfur unaweza kuyumbisha amani inayolegalega katika eneo la Kusini ambako amani hiyo ilirejeshwa Mwezi Mei mwaka 2004 baada ya mpango wa kugawana madaraka kuafikiwa baina ya serikali na kundi kuu la wanamgambo, na kumaliza vita kati ya kaskazini na kusini ambayo ilidumu kwa takriban nusu karne. Iwapo machafuko yataendelea Darfur, basi yanaweza kabisa kuuvunjilia mbali mpango huo unaolegalega.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mazungumzo ya Amani

  Ingawaje makundi kadhaa madogo-madogo ya waasi yamesaini mikataba ya amani na serikali, bado SPLA ilisema kuwa isingekubaliana na chochote isipokuwa uhuru kamili wa Sudan Kusini. Serikali ya Sudan ilizishutumu nchi za Ethiopia, Eritrea, Uganda na Tanzania kwa kuwasaidia waasi lakini nchi hizo zimekanusha madai hayo.
  Katika mazungumzo ya amani ya Katikati ya mwaka 1998, SPLA na serikali ziliafiki kura ya uhuru wa kujiamulia mambo wa Sudan Kusini chini ya usimamizi wa Kimataifa.

  Mikutano kadhaa ya kukomesha vita iliitishwa katika kipindi hiki ili kuunga mkono jitihada za kuleta amani na kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na chakula na chanjo katika eneo la kusini lililokubwa na vita.

  Mazungumzo ya amani ya Darfur yalianza tena Desemba 10, 2004, mjini Abeche, Kusini mwa Chad. Mnamo Aprili 9, 2004, serikali ya Sudan na makundi mawili ya waasi ya Darfur wakaukubali mpango wa kusitisha mapigano kwa siku 45 ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikia mamia kwa maelfu ya watu walioathiriwa na mapigano.

  Umoja wa Afrika (AU) ndio unaoyasimamia mazungumzo hayo ya amani baina ya serikali na waasi. Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya taarifa, waasi waliripotiwa kuuwa zaidi ya watu 1,500 tangu mpango wa kukomesha vita uliposainiwa.

  Mpango huo wa amani ulionekana kama njia ya kumuimarisha hayati John Garang. Alikuwa mmoja wa makamo wawili wa Rais wa Sudan lakini serikali iliamini kuwa Garang alikuwa na tamaa ya kupata kikubwa zaidi ya umakamu wa Rais, nacho ni kuimega Sudan apate nchi yake au kuchukua nafasi ya utawala.

  Marekani, kwa upande wake, badala ya kusaidia kumaliza mgogoro huo, yenyewe inazidi kuchochea hali ya mambo kwa kuuita kuwa ni mgogoro huo mkubwa kabisa wa wanadamu.

  Tangu mwanzo, Wachunguzi wa Kimataifa walionesha wasiwasi kuwa, kwa kauli kama hizo, wanamgambo katika mazungumzo ya amani wangekuwa wakaidi kwa matumaini kuwa mamlaka za Kimataifa zingelazimishwa kupeleka majeshi katika eneo hilo.

  Mnamo Septemba 17, 2004, Umoja wa Afrika katika mkutano wake wa duru la pili la Mazungumzo ya Amani ya Darfur Sudan, ulisisitiza haja ya Umoja wa Afrika (AU) kuendelea na jukumu la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Darfur.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hali ngumu inayoikabili serikali.

  Serikali ya Rais Bashir imeshindwa kurejesha utulivu katika nchi. Nchi hii kubwa Barani Afrika ipo katika tafrani kubwa ambapo mgogoro uliopo si mdogo kama Rais wa Sudan anavyotaka dunia ielewe.

  Umar Hassan Al-Bashir, Brigedia wa Jeshi la Sudan, aliingia madarakani akiendeleza kadhia zilezile za uhaba mkubwa wa chakula, vita vya msituni, machafuko na deni kubwa linalozidi kuongezeka pamoja na matatizo mengine ya Rais aliyepita, Sadiq Al-Mahdi.

  Mnamo Juni 1989, akiwa pamoja na Hasan At-Turabi, wakati huo akiwa Mwenyekiti Chama cha Umma wa Waislamu, The National Islamic Front, na ambaye pia ni Mwanasheria, Bashir aliipindua serikali ya Mahdi katika mapinduzi baridi.

  Miaka minne baadae, alipiga hatua kuuendea mfumo wa demokrasia ya vyama vingi akiondosha serikali ya kijeshi. Mnamo mwezi Machi, mwaka 1996. Katiba mpya ambayo serikali ya Bashir iliipitisha, ikaruhusu siasa ya vyama vingi na kulinda uhuru wa maoni na dini. Lakini Turabi na Bashir wakafarakana mwaka 1998.
  Bashir baada ya kujiweka karibu na ulimwengu wa Magharibi, akamtupa Turabi jela. Mfarakano wao ukaonekana kuleta mshituko kwa Waislamu wote waliokuwa wakiitazama Sudan kama kigezo kipya cha Dola ya Kiislamu.

  Rais Bashir, siku zote, ameshikilia msimamo mkali dhidi ya SPLA ambayo iliamua kutumia mbinu ya vita vya msituni ili kuitia msukosuko serikali. Lawama za Kimataifa juu ya hali ya Darfur zinailenga hasahasa serikali ya Sudan. Rais Bashir amezionya Uingereza na Marekani kutoingilia mambo ya ndani ya nchi yake.

  “Kila janga duniani lina muktadha wake. Sudan nayo haikukosa,” alisema mwandishi mashuhuri wa habari Said Naqvi katika gazeti la Indian Express la India. Naye Dkt. William Bowles, mtaalamu wa mafuta na mahusiano ya Kimataifa, anafafanua kwa upana zaidi ‘muktadha huo’ pale anaposema katika moja ya maandiko yake juu ya Sudan:

  “Kusema kuwa mafuta ndiyo chanzo kikuu cha hali ya mambo nchini Sudan ndiyo uwazi hasa japo vyombo vya habari vinataka tuamini kuwa huu ni uzushi mwingine kutoka kwenye genge la fitina.”

  Kwa kweli sababu ya China kulikanyaga kwa mguu wake azimio lolote la Umoja wa Mataifa la kuweka vikwazo ni kwamba inauona mchezo mkubwa wa mafuta ambapo Marekani ndiyo mchezaji mkuu.

  Mbali ya hivyo, China yenye dau la asilimia 40 pamoja na nchi nyingine zinazoendelea yaani Petronas ya Malaysia (asilimia 30), ONGC ya India (asilimia 25) na Sudapet ya Sudan (asilimia 5) zina dau kubwa katika sekta ya mafuta. Kwa hali hiyo, haishangazi pale Balozi wa China Umoja wa Mataifa alipoonesha ishara ya nchi yake kuzuia azimio jingine lolote la kuweka vikwazo.

  China ni moja ya nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama zenye kura ya veto na ilikuwa moja ya nchi nne zilizojitenga na kura (ikiwa pamoja na Urusi, Pakistan na Algeria). Makampuni ya China yana nafasi muhimu nchini Sudan.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nafasi ya Marekani.

  Ulimwengu unafahamu kuwa Marekani iliipiga vita Iraq kwa ajili ya mafuta. Na nchini Afghanistan Marekani iliiendea serikali ya Taliban, kuomba njia ya kupitisha mabomba yake ya mafuta hadi Asia ya Kati. Taliban ilipokataa, Marekani ilikuwa ikitafuta njia tu za kuwahilikisha ambayo waliipata kwa kisingizio cha Mkasa wa Septemba 11.

  Sudan ni nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa wa mafuta duniani, na kwa misukosuko ni nchi ya tatu baada ya Iraq na Afghanistan, ambapo inasusuikwa kama ni kadhia ya Kimataifa kwa sababu ya ule ambao Marekani inauita ‘mgogoro mkubwa wa kibinadamu ulimwenguni.

  Vyombo vya habari, haraka-haraka vikafuata nyayo za Marekani na kuanza kusambaza vijineno kama vile ‘mauaji ya kiimbari’ (genocide) na ‘Safisha-safisha ya Kikabila (Ethnic cleansing) nchini Sudan.

  Ikiwa hicho ndicho Marekani ilichotaka dunia ikiamini basi hapa kuna kingine: Mnamo Agosti 9, 2004, Umoja wa Ulaya ulitoa tamko ukisema “hakuna mauaji ya halaiki” nchini Sudan.

  “Hatuko katika katika mazingira ya Mauaji ya kiimbari hapa”, alisema Pieter Feith, Mshauri wa Msimamizi Mkuu wa Sera ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya na ambaye pia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Kutafuta Ukweli, aliyasema haya baada ya kutoka ziarani nchini Sudan.

  Hili pia limethibitishwa na Shirika la Misaada ya Kibinadamu Ulimwenguni, Shirika la Tiba Mipakani (MSF) lenye makao yake nchini Ubelgiji, ambalo lilifanya harakati za kuwezesha misaada ya kibinadamu kufika inakokokusudiwa. Shirika hili limepinga kuwepo kwa mauaji yoyote ya Halaiki nchini Sudan.

  Mnamo mwezi Mei, mwaka 2004, pale Sudan ilipochaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Mjumbe mmoja wa Marekani akatoka nje kupinga.

  Juni 29, 2004, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell aliitembelea Sudan kuyataka mamlaka ya nchi hiyo kuwadhibiti wanamgambo wa Kiarabu na kuitishia nchi hiyo juu ya hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama vurugu zisingedhibitiwa.

  Baadae Marekani ikaweka sharti la kuwa na ‘Mahusiano ya Kawaida na Sudan endapo tu kungekuwa na haki na amani kamili” nchini Sudan. Jambo hili linaibua swali la kuirudi Marekani kama iko tayari kutumia fimbo hiyo hiyo kujichapa yenyewe katika kujenga mahusiano ya kawaida na nchi nyingine iwapo tu kuna “haki na amani kamili” katika nchi ya Iraq inayoendeshwa na Marekani.
  Na kwa nini SPLA iliyokuwa ikipigana vita vya msituni kwa miongo miwili haikuwekwa kwenye mabano na Marekani kwa ugaidi? Ulimwengu umeshuhudia kuwa kutokana na ndimi mbili, Marekani inazidi kujishushia heshima katika kila jambo inalofunua mdomo kulizungumzia.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jawabu la Waarabu

  Nchi za Kiarabu zilitoa jawabu kuhusiana na kile kinachoendelea nchini Sudan na kuhusiana ba msimamo wa dunia juu ya kadhia hiyo. Nchi za Kiarabu ziliiunga Mkono Sudan juu ya suala la vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuhusiana na Darfur.

  Mnamo Agosti 9, 2004, Katika mkutano usiokuwa wa kawaida Mjini Cairo, nchi hizo zilitoa mwito wa kusogezwa mbele muda wa mwisho wa siku 30 wa kulitatua tatizo hilo. Tamko hilo likapokewa na Naibu Waziri Mkuu wa Saudia na Mrithi wa Mfalme, Abdullah wakati alipoendesha kikao cha Baraza lake la Mawaziri siku iliyofuata.

  Mrithi huyo wa Mfalme aliunga mkono hatua iliyochukuliwa na Sudan katika kulitatua tatizo hilo kwa msingi wa mkataba uliosainiwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa. Saudi Arabia ilisisitiza kuwa mamlaka ya Sudan na heshima ya nchi yake lazima viheshimiwe.

  Baraza hilo la Mawaziri lilikataa hatua yoyote ya kuingia Darfur Kijeshi au kuiwekea vikwazo vya uchumi Sudan na kuiomba jumuiya ya Kimataifa kuipa serikali ya Sudan muda wa kutosha kutekeleza ahadi zake kwa kuzingatia mkataba wake na Umoja wa Mataifa.

  Kweli Sudan inahitaji uangalizi wa dunia lakini si kwa misingi ya kile kinachoonekana kama mgogoro mkubwa wa kibinadamu bali mtazamo uelekezwe katika chimbuko la mgogoro na uchumi wake. Ukweli unapaswa kuwa wazi lakini katika ulimwengu wa leo wa muwamba ngoma, nani atasimamia hilo?
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pamoja na historia nzuri, ni kweli kwamba rasilimali ni sababu ya wamerakani kuifuata sana nchi hiyo, lakini Bashir ni kibaraka na dicteta laiti angekuwa anafuata misingi ya kiislam jambo hili angelimaliza bila kusubiri pressure kutoka nje

  Hata wamerakani hawana uhakika na atakayeshika madaraka baada ya dicteta ndio maana wana delay..kumtoa wana wasiwasi uchaguzi huru sudan itakuwa mikononi viongozi wa kiislam haswa kuliko u-dicteta wa bashir...wakishapata puppet wao wataivamia ..na kuna uwezekano mkubwa wa kuweka africom hapo
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,056
  Likes Received: 3,980
  Trophy Points: 280
  Acheni chokochoko zisizo na miguu wala kichwa kama Sudan ni 5% Christians basi kusingekuwa na haja ya kujitenga southern Sudan! hiyo vita ni ya kibaguzi kila mtu anafahamu na msubiri siku muarabu awatawale ndo mtajua chafu zake!
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mbona umekuja mbio mbio bila kujibu hoja, hii si vita ya kibaguzi watafiti wengi wameona hilo wewe source yako ni ipi?

  Hakuna chokochoko ila ni hoja kwa hoja...usikimbia leta hoja tukujibu..wewe ndio walete chokochoko bila data (tafiti) unafuata mkumbo!
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii data una uhakika nayo????????????
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Will come back with the data!
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Eh! Sasa jazba za nini tena?
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika na hizo Data mkuu, unaweza kunisaidia hapo...!
   
Loading...