Mgogoro wa CUF wazidi kusambaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa CUF wazidi kusambaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Dec 26, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad


  Mgogoro unaofukuta ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), umeingia sura mpya baada ya baadhi ya wanachama na waasisi wa chama hicho Wilaya ya Tanga, kutoa tamko la kuunga mkono kauli ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid na kuutaka uongozi wao wa Taifa kutoa maelezo na kuzifanyia kazi dosari zote zilizojitokeza.

  Hayo yalielezwa na waasisi hao katika kikao chao na waandishi wa habari jana wakidai kukerwa na malumbano yanayotengenezwa na viongozi waandamizi kupitia vyombo vya habari na hivyo kulazimika kutoa tamko kwa niaba ya baadhi ya wanachama wa Wilaya ya Tanga.

  Akizungumza kwa niaba ya wanachama na waasisi wenzake, Salim Daiyah Daiyah, alisema kwanza wanampongeza Katibu Mkuu wa CUF Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwataka viongozi kuacha kulumbana katika vyombo vya habari.

  Hata hivyo, walisema wanasikitika pia kuona wahusika hao bado wanaendeleza malumbano hayo, jambo walilolieleza kuwa ni hatari kwa mustakabali wa Chama hicho.

  Muasisi huyo na ambaye alishawahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya Wilaya ya Tanga, alisema kimsingi hawaridhishwi na malumbano hayo kwa kuwa hayana tija kwa Chama hicho na wanachama kwa ujumla na badala yake wanautaka uongozi huo kujibu madai ya

  Mbunge Hamad Rashid Mohamed waliyoyaeleza kuwa ni ya msingi.
  “Tunasikitika kuendelea kuwasikia viongozi hao wakiendelea kutoa tambo mbalimbali mfano kipindi cha baragumu kilichorushwa na televisheni ya Chanel Ten Desemba 19, mwaka huu masjira ya asubuhi. Sasa haya hatukutarajia yatokee tena baada ya kauli ile ya Katibu Mkuu,” alieleza Daiyah Daiyah

  Kwa upande wake, yeye alishauri viongozi hao kuyafanyia kazi aliyoyasema Mbunge wa Wawi Hamad Rashid kwani ni mambo ya msingi ambayo yanalenga kujenga chama ambacho alidai kuwa suala la kuzorota kwa chama hicho ni la wazi na halina ubishi.

  Naye Abdul Alqarney, ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Wilaya na Juma Mafita, Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Makorola, walieleza kushangazwa kwao na viongozi hao waandamizi kwa kile walichodai kupanga mikakati ya kumhukumu Mbunge Hamad Rashid badala ya kujadili jinsi ya kurekebisha dosari alizozieleza.

  “Sisi tunaona kuwa mambo aliyoyaeleza Mbunge wa Wawi, Mheshimiwa Hamad Rashd, ni ya msingi na tunaona si haki na vyema kujadili jinsi ya kumhukumu, badala yake wajibu na watekeleze yale aliyoyaeleza ambayo ni kuitisha vikao vya chama, kusimamia vizuri fedha na mali za

  chama hicho…..huu ndiyo msingi tunaoutaka ufuatwe kwa mujibu wa katiba yetu ya chama,” alisema Abdul.
  Naye Mafita alisema ufike wakati viongozi kukubali kukosolewa na kukumbuka lengo la chama hicho la kutaka kukiimarisha kuanzia bara na

  visiwani na hatimaye kushika dola pande zote mbili za Muungano.
  Hata hivyo, katika tamko la wanachama hao walisisitiza umuhimu wa viongozi kutumia vikao halali vya kikatiba vya Chama kutatua matatizo na kujibu madai yaliyotolewa na wa Wawi na kwamba vikao visivyo rasmi vinaweza kuchochea zaidi vurugu ndani ya chama hicho.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  CUF kwishney
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  ...Sumu ya magamba imeingia kwa Magamba B. Tatizo kubwa kwa maoni yangu ni huyu SSH. Sijui kama wataweza kumtimua maana yeye kisharidhika sasa hivyo kasahau kabisa malengo ya chama chake.
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wameongea mambo ya msingi sana CUF inatakiwa kumsikiliza Hamad na kuyafanyia kazi madai yake..
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hawa ndio wanachama hizi habari za kumtafuta mtu uchawi wakati anachosema ni kweli ni Ujinga mtupu..sina mapenzi na CUF lakini sintopenda kuona chama kinakufa kabisa kwa sababu naaamini ipo siku vyama vya Upinzani watajitazama kama hivi na watafikia muafaka wa kuunda nguvu moja dhidi ya chama tawala..Kwanza fanya usafi nyumbani kwako mengine yooote yatajipanga.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe Vyama vya Upinzani lazima viwe kitu kimoja dhidi ya chama Tawala, ndio hivyo vyama vya upinzani vinaweza kukizidi nguvu Chama Tawala. Pasipo na kuwa na Umoja hivyo vyama vya Upinzani haitakuwa sio Rahisi kuking'owa Chama Tawala katika uchaguzi wa aina yoyote ile Waswahili husema Umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu kazi kwao vyama vya upinzani...
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Hao wana CUF Wakiamuwa kumuondowa huyo Mzee Madevu SSH, basi na hicho chama kitakuwa nio mwisho wake hakita pata hata kura moja kwenye Uchaguzi mkuu unaokuja miaka ya mbele na sio Rahisi kumuondowa Mzee Madevu SSH.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  CUF hajakwisha Mkuu kila chama hakikosi migogoro ndio maana kikaitwa chama Mkuu uko pamoja na mimi? Wanajipanga Upya cUF kwa ajili ya Uchaguzi mkuu unaokuja miaka ya mbele mkuu.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  CUF itabidi Wamsikilize Katibu mkuu Sheikh Hamadi ili mambo yatulie tunangojea mwisho wake nafikiri mambo yatakuwa shwari.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Hatima ya Hamad Rashid wa CUF leo


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed​
  Kizitto Noya
  HATIMA ya uanachama ya Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed inatarajiwa kujulikana leo atakapojieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho.

  Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kuvuliwa uanachama na chama chake hicho kwa madai ya kukiuka maadili na katiba ya chama ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana na yale yanayomkabili Hamad.

  Hamad hivi karibuni amejikuta katika mgogoro na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya CUF baada ya kutangaza kuwania nafasi ya katibu mkuu wa chama inayoshikiliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na kuanza kupita kwenye matawi akigawa misaada, hatua ambayo ilisababisha vurugu katika matawi aliyopita huku tukio katika Tawi la Chechnya lililopo Manzese, likisababisha umwagaji damu baada ya wanachama wanaomuunga mkono kupambana na walinzi wa Blue Guard.

  Baada ya vurugu hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Hamad angeitwa mbele ya kamati hiyo na jana, taarifa ya CUF ilisema mbunge huyo leo atahojiwa na kamati hiyo kwa tuhuma za kuvunja katiba ya chama hicho.

  Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, adhabu ya kosa la kuvunja Katiba ya chama ni kupewa onyo kali, kusimamishwa au kufukuzwa uanachama.Hamad Rashid mwenyewe, alithibitisha kuitwa kwenye kikao hicho na wanachama wenzake 13 wanaomuunga mkono.“Ni kweli nimeitwa lakini tuko wengi kidogo. Wameniandikia barua kuniita kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili kesho (leo), ila nasikitika kwamba walianza kunihukumu kabla ya kunisikiliza,” alisema Hamad.

  Kuhusu alichoitiwa Hamad alisema: “Wanasema nimevunja Katiba ya chama,” huku akirejea adhabu zilizoanishwa kikatiba juu ya kosa hilo.Lakini, akionekana kujua kitakachomtokea kwenye kikao hicho, Hamad alisema kuwa atakata rufaa kupinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama.“Mimi kuitwa nilitarajia lakini hofu yangu ni kwamba wameshanihukumu kabla ya kunisikiliza. Ila msimamo wangu bado uko palepale, nitakata rufaa kupinga adhabu ya kufukuzwa uanachama,” alisema.

  Awali, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkuu wa Idara ya Nidhamu na Maadili ya CUF, Abdul Kambaya alisema Hamad na wenzake hao 12 wanaitwa kwenye kikao hicho ili kusomewa tuhuma zinazowakabili na kuwapa fursa ya kujieleza.
  “Tayari tumeshawapa barua za kuwaita kwenye Kamati ya Nidhamu ya Chama kuanzia 27 na 29 kwa mahojiano zaidi,” alisema Kambaya na kuongeza kuwa kuhojiwa kwa viongozi hao kuna baraka zote za chama.

  Mbali na Hamad, Kambaya aliwataja watuhumiwa wengine walioitwa kwenye kamati hiyo kuwa ni Juma Saidi Saanan (Mjumbe wa Baraza Kuu Unguja) na Shoka Khamis Juma (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Pemba).
  Wengine ni Doyo Hassan Doyo (Mjumbe wa Baraza Kuu Tanga), Yasini Mrotwa (Mjumbe wa Baraza Kuu Mbeya), Doni Waziri (Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala) na Mohamedi Massaga (Katibu wa Wilaya ya Ilala).

  Wanachama wengine Albadawi (Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke), Amir Kilungi, Yusufu Mbungilo (Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Wilaya ya Temeke) na Nanjase ambaye ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Nachingwea.

  Pia wamo Tamimu Omari (Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkunduge, Kata ya Tandale) na Ahmed Issah kutoka Wilaya ya Morogoro Mjini.“Tumeamua kuwaita kwa malengo ya kujadiliana na kuangalia mustakabali wa chama kwa mujibu wa katiba ya chama chetu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

  "Tunawomba wanachama kuendeleza amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho chama kinakaa katika vikao vya uamuzi.”
  Baadaye Kambaya alisema kwa simu kuwa kamati hiyo, haina mamlaka ya kuwapa adhabu watuhumiwa hao hata kama watabainika kuwa na makosa.
  “Sisi kazi yetu ni kuwasomea tuhuma zao na watapewa muda wa kujieleza kisha tutapendekeza adhabu kwenye vikao vya uamuzi ambavyo ni Kamati ya Utendaji na Baraza Kuu la Uongozi.”

  Alipoulizwa vikao hivyo vitakaa lini alisema: “Kamati ya Utendaji itaketi Desemba 30 na Baraza Kuu la Uongozi Desemba 31, mwaka huu.”
  Hata hivyo, alieleza kuwa mtuhumiwa asiyekubaliana na uamuzi wa vikao hivyo anaweza kukata rufaa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa ambao katika suala hilo, utapangwa na Baraza la Uongozi.

  Ingawa haijathibitika kama Hamad na wenzake hao watafukuzwa uanachama, CUF ina historia ya kufanya hivyo kwa wanachama wake. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa waliowahi kukumbuwa na masahibu hayo ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mapalala na aliyekuwa Mbunge, Naila Jidawi na Salum Msabaha.

  Lakini Kambaya alisema katika taarifa hiyo kuwa: “Tunawaahidi wanachama na Watanzania kuwa hatutamuonea yeyote katika uamuzi utakaotolewa na vikao vyote.”

  Mgogoro wa Hamad na Maalim Seif ulianza kuibuka baada ya Hamad kutangaza nia yake ya kuwania ukatibu mkuu wa CUF kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2014.

  Mgororo huo ulipambana moto mwishoni mwa Novemba katika mkutano wa Hamad uliofanyika Manzese, Dar es Salaam ambako mabaunsa wa chama hicho walivamia mkutano huo na kusababisha mapigano baina yao na wanachama waliokuwa wamehudhuria.

  Tangu hapo, Seif na Hamad wamekuwa wakizunguka kwa nyakati tofauti mikoani mbalimbali nchini na kutoa matamko kadhaa kuhusu ugomvi huo.Mara ya mwisho Seif akiwa Mwanza, alisema mgogoro huo utamalizwa katika vikao vya ndani vya chama hicho.

  Kwa upande wake, Rashid akiwa mkoani Singida alisema hana hofu na vikao hivyo na kwamba anavisubiri kwa hamu ili akaseme kile alichokiita ukweli juu ya hatima ya chama hicho chini ya uongozi wa Maalim Seif.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo. Hatima ya Hamad Rashid wa CUF leo
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CUF ni wakomavu watamaliza haya yote kistaraabu
   
 13. m

  mzalendo2 Senior Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa kweli tunasubiri nn kitajiri.

  tusiwe watabiri zaidi wakati mambo yatawekwa hadharani
   
Loading...