MGOGORO WA CHADEMA Vs ZITO NA TAFAKARI YA MONJA

MONJA

Member
Apr 4, 2013
43
11
Naomba nianze kwa kusema kuwa mfumo wa vyama vingi unaoongozwa na demokrasia ya uwongouwongo ndio chanzo cha matatizo ya kiuchumi na hata migogoro mbalimbali inayopelekea kumwagika kwa damu, katika nchi zinazoendelea hasa Afrika.Sasa naweza kusema imefika wakati tukubali kuwa ni bora udikteta wenye tija kwa wananchi kuliko demokrasia isiyo na tija yeyote kwa wananchi. Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu kuwepo kwa hali ya sintofamu ndani ya chama makini chadema inayotafsiriwa na baadhi ya watu hasa maadui wakubwa wa chama kama ni mgogoro.Binafsi nikiwa kama mwanachama wa chadema siamini kabisa kuwa huo ni mgogoro bali ni changamoto tu katika kupigania kumwondoa mkoloni mweusi ccm.Kutokana na hali ilivyo ndani ya chama naomba nitoe maoni na hata ushauri pia kuhusu hali ya chama tunachokipenda na kukiamini kuwa ndio mtetezi wa wanyonge wengi na si kwa chadema pekee bali hata vyama vingine pia kwa mustakabali wa nchi yetu kama ifuatavyo; 1;Naungana mkono na kamati kuu ya chama kwa hatua walizozichukua dhidi ya Zito mwenye tuhuma ya kuhujumu chama,kwasababu hata kama Zito asingevuliwa vyeo vyake na kama kweli anamini hausiki na tuhuma hizo na kama kweli yeye ni mwanachama mtiifu wachadema na anaipenda kama anavyojinasibu katika maongezi yake mbalimbali alipaswa aachie ngazi ili kupisha uchunguzi huru dhidi yake.Lakini hali haikua hivyo badala yake amekuwa mstari wa mbele kutunishiana misuli na chama na baadhi ya viongozi wenzake tena waziwazi mbele ya halaiki ya watu ili mradi tu awadhihirishie wananchi na wanachama wa chadema kuwa kuna mgogoro ndani ya chama na yeye anaonewa. 2;Bado nashindwa kuelewa kwanini Zito anataka aonekane kuwa yeye ni bora kuliko wengine ndani ya chama,kama kuna mambo yanafanyika kinyume na sheria basi alipaswa afuate taratibu zinavyomtaka na kama anaona hasikilizwi na anataka kuwaonyesha watanzania mapungufu yachama chake alipaswa ajiondoe katika chama hicho ili apate kuyasema magungufu hayo akiwa chama kingine kama hawezi kuishi pasi na chama,sasa kwa hali kama hii kwanini viongozi au hata wananchi wasiamini kuwa zito ni msaliti kwa wenzio na chama chake? 3;Waraka wa mabadiliko 2013, unaodaiwa kuandikwa na zito na wenzike, wazi kabisa walitaka kukibomoa chama na kutaka chama kisambaratike.Kama kweli zito ni kiongozi mtiifu ndani ya chama hawezi kuwaambia wenzake kuwa hawana elimu na wanaongoza chama kilocal local,sasa kama kigezo cha kuwa kiongozi wa chama au taifa ni elimu basi viongozi wote wa chama na nchi basi maprofesa na madoctor ndio wenye haki ya kuwa viongozi tu,sasa zito atuambie anataka uongozi yeye ni profesa au doctor?.Viongozi waliopigania uhuru kama Nyerere,Mandela,nkrumah,obote na nk walikuwa na elimu gani ya maana ambayo elimu ya mbowe na wenzake anaona haifai kuongoza chama? 4;Kama waraka ule hauna tatizo kama anavyojinasibu zito na wenzake mbona ulikuwa ni waraka wa siri na kwanini usingefuata taratibu za chama kama waraka halali wa chama,na kuwashirikisha wenzake? 5;Katibu mkuu alisema kuwa mjadala wa zito ulikuwa umefungwa sasa haikuwa haki kwa Dr slaa,zito na mbowe kuundeleza katika majukwaa ya hadhara, kutokana na hilo limechangia kuongeza kasi ya mjadala na kusababisha wananchi waanze kukata tamaa na chama.
USHAURI
1;Zito asifukuzwe uwanachama lakini avuliwe nyadhifa zake zote ndani ya chama na abaki kama mwanachama na mbunge tu.Tukifanya hivyo itasaidia kuondokana na mgogoro huo na viongozi na wanachama kupata muda wa kujenga chama na kukiandaa kwa chaguzi zinazotukabili tayari kwa ushindi. 2;Zito kama kweli wewe unapigania haki kama unavyojinasibu hunabudi kukubali kukaa kando ili kukinusuru chama na migogoro isiyo na tija,unapaswa kufuata taratibu na kanuni za chama usione wewe ni muhimu sana au ni maarufu sana kulikochama.Chama cha siasa si klabu ya mpira ambayo mchezaji anaweza kuwa maarufu kuliko hata timu yenyewe. 3;Mh mbowe usigombee nafasi yeyote ndani ya chama labda ubunge au uraisi kama utataka ili kuondokana na propaganda zinazoenezwa kuwa wewe na zito mnaleta mgogoro ndani ya chama kwasababu ya uwenyekiti wa chama. 4;Nafasi ya mwenyekiti ni ya kila mtu kulingana na katiba ya chama,mwanachama yeyote ana haki ya kugombea nafasi hiyo. Lakini kwa mustakabali wa chama,zito na mbowe wasigombee nafasi hizo na wawaache wanachama wengine ambao ni makini,sio wasaliti na wenye moyo na uwezo wa kujenga chama kama,au zaidi ya mwenyekiti wa sasa mh mbowe. 5Viongozi wa chama wajikite katika ujenzi wa chama badala ya kushughulikia migogoro inayowapotezea muda mwingi bali kitengo cha sheria na katiba kipewe mamlaka hayo chini ya wanasheria makini na mahiri kama lisu,marando na wenzake.Pia kuwepo na kitengo cha propaganda chenye watu mahiri wa IT na wenye uwezo wa kupambana kwa hoja katika mitandao na hadhara mbalimbali ili viongozi watumie muda mwingi kukiandaa chama kwa ushindi chaguzi zinazokuja na kuacha kupoteza muda mwingi kujibishana na maadui. 6.Kamati kuu ya chama iamuru kufanyika uchunguzi kuhusu tuhuma anazozitoa zito kwa mwenyekiti na katibu kama ni za kweli ili hatua zichukuliwe kwa kufuata taratibu na kanuni za chama ili kila mtu asione ameonewa. 7;Chama tawala kiache utaratibu wa kuchochea na kupandikiza migogogro ndani ya vyama vya upinzani,waache wananchi wenyewe wachague mbivu na mbichi na sio kutumia muda na rasilimali za uma kupambana na wapinzani badala ya kujikita kwenye maendeleo.Kama wanaona hawawezi kushindana basi waondoe mfumo wa vyama vingi kibaki kimoja tuendelee kujenga nchi na sio kuchochea migogoro ndani ya vyama hivyo inayosababisha migogoro ndani ya jamii mfano,udini,ukabila,ukanda nk,inayochochewa kwa kasi na siasa chafu za chama tawala CCM. 8;Vyama vingine kama cuf,nccr,tlp nk,wafanye siasa na si kusubiri matukio na kisha kutoa matamko ambayo hayana tija kwa jamii huku wananchi wakizidi kuteseka na matatizo mbalimbali.Kama vyama hivyo haviwezi kupambana na ccm na chadema basi vifutwe vibaki vyama venye uwezo wa kufanya siasa na kigezo cha ukata wa fedha ndani ya chama ndio sababu mimi sikiafiki kabisa kwa sababu mtu huwezi kuanzisha chama kama huna uwezo wa kukiendesha,hii ni kwa maslahi mapana ya wananchi wawe na wigo mpana wa kuchagua chama makini chenye sera za kuwasaidia. MWISHO; Ni bora udikteta wenye tija kwa nchi kuliko demokrasia isyo na tija kwa wananchi na nchi kwa ujumla.Kama demokrasia imetushinda basi twende kwenye udikteta wenye tija kwa nchi na kama huu mfumo wa vyama vingi umetushinda basi turudishe mfumo wa chama kimoja na sio kuleta migogoro ndani ya jamii inakopelekea kurudisha juhudi za kupambana na maradhi,ujinga,umaskini na ufisadi.
 
Back
Top Bottom