Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
Kuna migogoro ya wakulima na wafugaji ambao walianza kulumbana, kugombana na sasa wanauana huku serikali ikionyesha kushindwa kabisa kuzuia mauaji hayo.
Ukiangalia mgogoro uliopo bungeni juu ya Naibu spika na wabunge wa upinzani unapata picha kwa nini hili sakata la mauaji ya wakulima na wafugaji haliishi.
Hivi kwa nini bunge lina wenyeviti watatu? Wanachaguliwa kuongoza vikao vya bunge, lakini kwa vile kuna mgogoro (ambao unaweza kushughulikiwa) kati ya NS na wabunge kwa nini wenyeviti hawapewi nafasi ya kuongoza vikao bali NS mwenye mgogoro kaamua haachi nafasi ili wabunge wale watoke? Nchi inakosa uchangiaji muhimu kwa nini?
Yaani kiburi cha mtu mmoja kinasababisha haya yote?
Kihistoria ya bunge michango ya wabunge wa upinzani imekuwa muhimu sana na imekuwa ikitoa msaada mkubwa kwa serikali kurekebisha mambo kwa faida ya nchi na tunaikosa.
Hakuna wa kuliona hili hata ndani ya Bunge na kumwambia Naibu spika kuwa cheo chake hata kazi za ofisini zipo nyingi tuu na awaachie wenyeviti nchi inufaike?
Mgogoro wa wabunge utaishia kuwa kama wa wakulima na wafugaji siku sio nyingi. Au aliye muweka NS ndio kamwambia komaa hapo kwenye kiti kama uliyewekewa super glu?