Kwisense
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 475
- 1,138
Jamani naandika ujembe huu nikiwa Tarime mjini nikielekea kata ya Kibasuka kijiji cha Nyarwana kitongoji cha Mwara kwenye msiba wa ndg. Magige Mesenda alieuwawa kwenye vita inayopiganwa kati ya kitongoji cha Mwara na Matongo (Nyamongo) kwa sababu ya mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa miaka zaidi ya mitatu sasa, vita hiyo imekuwa ikipiganwa mara kwa mara, na polisi wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kuhakikisha usalama wa eneo hilo unaimarika lakini pale polisi wanapokuwa wametuliza amani ya eneo hilo huondoka kurudi vituoni na mapigano kuanza upya tena, na uongozi wa eneo husika umekuwa ukikaa kimya baada ya kuona fujo zimetulizwa bila kulitafutia swala hilo na kulipatia suruhisho la kudumu, hivyo basi baada ya polisi kuondoka kwenye eneo husika wananchi wamekuwa wakiviziana na kupigana, na wanazuiana hata kuchota maji kwa kina Mama kwenye mto Tigite (ambao ndio chanzo cha mgogoro), kuzuia hata wasio wenyeji wa maeneo husika wasipite njiani, kumekuwa kama Israel na Palestine jambo ambalo sisi Watanzania hautajalizoea, jana tu tarehe 30/09/2017 ameuwawa mtu mmoja na watatu kujeruhiwa, hivyo basi naomba ujumbe huu uwafikie Mkuu wa wilaya ya Tarime Mr Luoga, Mh William Lukuvi -WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI, WAZIRI WA OR-TAMISEMI, Waziri Mkuu Ndg Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara watutembelee kijijini waone wananchi wanavyopata shida bila kujua hatima ya kilio chao kinapata mwarubaini lini, namba yangu ya simu ni hii 0765196548, nawaomba viongozi wetu mtusikie kilio chetu sisi wananchi wa eneo husika tunapata mateso makubwa sana. Maana kwa imani kubwa tulionayo sisi wananchi wa chini na serikali hii ya AWAMU YA TANO CHINI YA RAIS DKT. MAGUFULI, HUU MGOGORO HAUKUPASWA KUSHUGHULIKIWA HIVYO. Nisaidieni kupaza sauti kwa hilo jambo jamani.
Naomba viongozi wetu tusaidie kumaliza huu mgogoro maana ni wa siku nyingi sana
Naomba viongozi wetu tusaidie kumaliza huu mgogoro maana ni wa siku nyingi sana