Mgodi wa dhahabu waibuka shuleni; Walimu, wanafunzi waacha masomo, wachimba madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgodi wa dhahabu waibuka shuleni; Walimu, wanafunzi waacha masomo, wachimba madini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Makunga Peter, Bukombe  MGODI mpya wa machimbo madogomadogo ya dhahabu umeibuka katika Shule ya Msingi Nganzo, wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga na kufanya viongozi wa wilaya kwa kushirikiana na mwalimu mkuu wa shule hiyo kuufanya kuwa mradi wao wa kujiingizia fedha.
  Machimbo hayo yaliyoibuka takriban miezi miwili iliyopita yamesababisha shughuli na masomo katika shule hiyo kusuasua kutokana na walimu na wanafunzi kujiingiza katika shughuli za uchimbaji huku wakisahau kuzingatia masomo hali ambayo imesababisha utoro mkubwa wa wanafunzi.
  Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho yalipo machimbo hayo, Boniphace Mashebela, alisema kuwa machimbo hayo madogo kwa sasa yanamilikiwa na kamati ya shule na kijiji lakini yanaendeshwa kwa ridhaa ya Ofisa Elimu wa Shule za Msingi, Fides Munyogwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Kuruletera Majige, kwa kigezo kuwa machimbo hayo yapo katika eneo la shule.
  Mmoja wa wachimbaji wadogo wanaoendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo, Masamaki Kambale, alisema wao wapo hapo kisheria na si wavamizi kwani wao hufika na kuripoti ofisini kwa mwalimu mkuu pamoja na mtendaji wa kijiji na wao hugawiwa viwanja kabla ya kuzamisha maduwara yao.
  Masamaki alisema kuwa kila duara linasajiliwa kwa sh 40,000, ambapo fedha hizo hupewa mwalimu mkuu na mtendaji wa kijiji na pindi duara linapofikia kuanza uzalishaji kila utoapo mifuko 10 ya mawe kati ya hiyo miwili ni mali ya viongozi hao wa wilaya hiyo.
  Alisema kuwa kwa upande wa kamati ya shule na mtendaiji wao hutoza ushuru wa sh 1,000.
  Kwa upande wake Ofisa Madini wa Wilaya ya Kahama na Bukombe, Medard Msengi, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya shutuma hizo alisema mgodi huo mpaka sasa ofisi yake haiutambui na kuomba kuongozana na waandishi wa habari hadi katika eneo hilo kujionea.
  Ofisa huyo alipofika alijionea kuwa machimbo hayo yanaendeshwa kinyume cha sheria, kwani kipimo kutoka shimo hadi shimo kinatakiwa kiwe futi 10 kwa 10 lakini hayo yapo futi mbili hadi tatu, hali ambayo inaweza kusababisha maafa ya watu kufunikwa na kifusi wakati wowote wa uchimbaji.
  Aidha, alitoa ushauri kuwa ni bora machimbo hayo yakafungwa kwa kuwa yapo katika eneo la shule, hali ambayo inachangia wanafunzi kutosoma vizuri na walimu kukimbilia kufanya biashara hiyo ya uchimbaji, hali ambayo itadhoofisha maendeleo ya elimu katika shule hiyo kwani hayana uataratibu wowote. Alisema katika eneo hilo hakuna vyoo, hakuna mtaalamu anayetambulika katika ofisi yake ambaye anashughulikia madini katika eneo hilo maarufu kama waangalizi wa madini ili kufanya hali ya usimamizi katika eneo hilo kuwa rahisi na kudhibiti wanafunzi na walimu kufanya kazi hiyo. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe alipoulizwa kwa njia ya simu, alisema kuwa kweli machimbo hayo yapo katika eneo la shule na kuongeza kuwa tayari ameshatoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya maandishi, ila alikanusha kuwa yeye hahusiki katika kuchukua mifuko katika eneo hilo na kuiuza kama inavyosadikiwa.
   
 2. D

  Danniair JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tunashukuru kwa utajiri huo lakini tunawatahadharisha kuwa waharakishe kuuvuna kabla serikali haijawapatia inaowaona wanafaa kuvuna dhahabu hiyo kutoka nje ya nchi hii, kwani vya kwetu vimekuwa ni mali za watu toka nje ya nchi nasi tumefanywa duni na viongozi tuliowachagua. INAUMA
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hii nchi ina madini kila sehemu tatizo viongozi wetu vichwa panzi!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Yeah Wachume Mapema na Wajiendeleze kabla ya Serikali takatifu inayopenda Wafadhili; Nakumbuka Kabla ya Geita Machimbo kuchukuliwa na Serikali wananchi ndio walikuwa wachimbaji na wanauza kwa Benki Kuu; Ilikuwa kila Mtu na familia yake na pesa; yaani unaona jinsi familia ilivyokuwa inatoka haraka kwenye Umasikini... Sio sasa hivi
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ngoja tufanye utafiti kama yapo mengi afu ni chonge na obama ili niweze pata 10 percent fast
   
 6. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  sijui itakuwaje dhahabu ikigundulika maeneo ya Mtogole
   
Loading...