Mgodi wa Dhahabu wa STAMICO Wafungwa

Mgodi wa Dhahabu wa STAMICO Wafungwa

Dah idadi ya wanao isoma namba inaongezeka.
May napo kunawengine watafata.
Mwenyezi atuepushie kikombe hiki.
 
TBL ilitushinda, tutaweza mining! Hizi Kazi za kusimamia mashirika makubwa kama haya,zingekuwa zinaombwa na MTU binafsi,kupitia usahili,apatikane aliye bora,akiburunda,no mahakamani tu,
 
Magufuli anatakiwa kuwatumbua STAMICO pamoja na Mameneja wote wa STAMIGOLD. Hao ndio wameuangusha mgodi. Mameneja wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa kawaida kuiba mali za mgodi Ikiwemo dhahabu ambayo tayari imesha zalishwa kwa gharama. Mfano mkubwa kuna dogo alikamatwa na dhahabu ya 70M. Hiyo halamashauri unawalipa mishahara watumishi wangapi? Waioshiri wote kumilikishwa mgodi na waliokuwa watendaji wakubwa pale mgodini watupwe ndani kwa uchunguzi zaidi. Ikibidi wafirisiwe mali na kunyongwa kama enzi za nyerere tuuu. Ujingaaaaa
 
Kuna taarifa kuwa mgodi wa dhahabu ambao awali ulikuwa unamilikiwa na kampuni ya Barrick umesimamisha uzalishaji kutokana na kushindwa kujiendesha.

Kampuni ya Baarick ndiyo iliyoujenga mgodi huo, na kisha kufanya uchimbaji wa dhahabu na baadaye kuamua kuondoka. Waliondoka huku wakiwa wameacha deposit ndogo ambayo ilihitaji pit mpya. Mpaka Barrick wanaondoka kwenye mgodi huo, mgodi wa Tulawaka na ule wa North Mara, ndiyo inayotajwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa faida.

Serikali iliomba iachiwe deposit iliyokuwa imebakia, miundombinu yote ikiwemo plant na majengo. Mgodi huo ulikabidhiwa kwa STAMICO, nayo kwa kupitia kampuni yake ya STAMIGOLD waliamua kufanya biashara ya uchimbaji wa dhahabu, huku wakiwa wamepewa vitu vyote bure na mwekezaji, ikiwemo plant, majengo, miundombinu mingine zikiwemo barabara, waste dump, maji, umeme, n.k. Jambo la kushangaza ni kwamba pamoja na kupewa vitu vyote hivyo bure, mgodi huo umeshindwa kujiendesha kwa faida na kufikia kuzalisha dhahabu kwa gharama ya U$1,500 na kuiuza kwa U$1,200 kwa ounce moja.

Awali, hesabu zote zilifanyika, na kuonekana kuwa uchimbaji wa deposit iliyobakia, ungefanyika kwa faida. Mpaka sasa mgodi huo unadaiwa na wazabuni mbalimbali kiasi kinachofikia shilingi zaidi ya bilioni 50. Fedha hiyo sasa ni lazima italipwa na serikali kwa sababu STAMIGOLD hawana uwezo wa kulipa.

Tuna mambo ya kujiuliza:
1) Kama serikali ilipewa vitu vyote hivyo bure, ikashindwa kufanya uchimbaji dhahabu kwa faida, je ingegharamia kila kitu kungetokea nini?

2) Tumekuwa tukiwalaumu sana wawekezaji wa nje kuwa wanatuibia, lakini wao wanaweza kuchimba kwa faida, kulipa mrabaha, kulipa corporate tax (japo ni mpaka wanapokuwa wamerejesha mitaji yao), hivi sisi tuna uwezo wa kuanzisha na kuendesha hii miradi ya uchimbaji madini?

3) Serikali na Watanzania tunajifunza nini kuhusiana na sekta hii baada ya STAMIGOLD kushindwa kufanya shughuli za uchimbaji wakati wakiwa wamepewa karibia kila kitu bure?

4) Hivi Watanzania na serikali wanatambua kuwa utafiti na uchimbaji madini, siyo sawasawa na kuchota maji, na kuwa (mining business) ni kati ya biashara zenye uwezekano wa hasara kubwa kuliko biashara nyingine yeyote?

5) Hivi kuna faida gani kuanzisha miradi ambayo badala ya kuleta mapato kwa serikali, yenyewe ndiyo inayotafuna hela za walipa kodi?

6) Kwa nini serikali haioni busara kuachana kabisa na shughuli za kibiashara kutokana na uzoefu tulioupata kuwa serikali yetu haijawahi kuendesha biashara yoyote kwa faida?

7) Matukio haya yanatupigia kengele kuhusu utendaji mbovu wa TANESCO, ATCL, TTCL, POSTA, Reli, TPA, n.k. Ninaamini kuwa shughuli zote zinazofanywa na makampuni tajwa, kama zingekuwa zinafanywa na sekta binafsi, huenda tungepata faida kubwa kiasi cha kupindukia. Kwa bahati mbaya, serikali ambayo ina uzoefu mkubwa wa kushindwa kuendesha biashara ndiye msimamizi mkuu wa akampuni haya.

USHAURI
1) Tanzania tunahitaji sana wawekezaji wa nje na ndani katika sekta ya madini, pengine kuliko sekta zote kutokana na mahitaji makubwa ya mitaji, uzoefu na risk ambazo zipo kwenye sekta hii. Serikali haitafanikiwa kufanya uchimbaji wa madini yoyote kwa faida kwa mfumo uliopo. Jukumu la serikali liendelee kuwa katika usimamiaji wa sera na sheria.

2) Wawekezaji, wawe wa nje au wa ndani, ni wadau wa maendeleo. Mahusiano ya wadau hawa na serikali ni lazima yawe ya maelewano na kiurafiki kwa faida ya wananchi wote. Kwa sasa, wawekezaji, hasa kwenye sekta ya madini, wanaonekana kama adui wa serikali. Mfano mzuri ni suala la linaloitwa mchanga wa dhahabu lilivyochukuliwa na kushughulikiwa. Wengi hawajui athari zake lakini limeiamsha Dunia kuwa Tanzania siyo mahali salama kwa makampuni ya kigeni kuwekeza kwenye madini.

3) Serikali ni lazima ifanye kwa ukaribu sana na wawekezaji katika sekta hii. Kwa sasa, takwimu zinaonesha ukuuaji wa uchumi wetu unasababishwa na sekta ya madini na utalii. Hiyo ni ishara tosha kuwa serikali inatakiwa karibu sana na sekta hizi mbili kutokana na nafasi zake kwenye uchumi wa nchi. Mafanikio kwenye biashara siku zote huwa makubwa katika maelewano kuliko penye uadui, visa, visasi au kukomoana.

4) Serikali iangalie uwezekano wa shughuli zote za kibiashara, uendeshaji wake kufanywa na sekta binafsi na serikali kubakia tu kama wabia. Makampuni kama TANESCO, TTCL, ATCL, TPA, etc, yanatakiwa kubomolewa ili yasiendeshwe na serikali.

MWISHO
Kauli aliyoitoa Waziri Mkuu alipotembelea mgodi wa Buzwagi ilikuwa ya kiungwana. kwa maneno yake, alitamka, 'Tanzania bado tunahitaji sana wawekezaji wa nje. Tunayaomba makampuni ya madini yaendelee na shughuli za uchimbaji bila wasiwasi wowote. Kinachofanyika kwa sasa kuhusiana na mchanga wa dhahabu ni kuchukua vipimo, na kisha kuptia sheria zetu, na kujiridhisha kuwa tunacholipwa ndiyo tunachostahili kulipwa'. Kauli ile ilikuwa nzuri, na ndiyo iliyostahili kutolewa toka mwanzoni kabisa kuliko kauli zile kuwa , 'makampuni yamekuwa yanaiibia sana nchi hii', wakati hatujui hata tunaibiwa kwa namna gani na kiasi gani. Na naamini haikuwa sahihi kusimamisha upelekaji wa mchanga nje kabla ya kufanya uchunguzi kwanza, na kujiridhisha kuwa tumesimamisha kwa vile tunaamini kuna ukiukaji wa makubaliano.

Ambayo yametokea ni kujikwaa kwa namna fulani kwa serikali, ni wakati wa kujirudi, na kujenga mahusiano mapya ya kuaminiani, kirafiki na maelewano kati ya wawekezaji katika sekta ya madini, serikali na jamii.

Tutambue kuwa baada ya kukosekana kwa pesa ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini kwa karibia miaka mitano, sasa kuna pesa za kutosha kwenye masoko ya fedha Duniani ambayo ni kwaajili ya uwekezaji kwenye sekta ya madini. Tanzania haijaweza kufaidika na uwepo wa pesa hizi kutokana na Dunia kuiona Tanzania siyo mahali salama sana kwa mitaji ya nje.
acheni story za kutunga na kuonyesha chuki ya wazi kwa watanzania wenzenu ambao tangu 2014 tumekuwa tukiona kupitia taarifa mbalimbali kuwa wanazalisha dhahabu na hawakuwahi kufunga hata mara moja. ifikie sehemu tuwape moyo wataalam waliokataa kufanya kazi makampuni ya kigeni wanapambana kufa na kupona stamigold iendelee kuwepo. hata hao barrick hawakuanza na kupata faida hapo hapo tena wao huwa wanachimba hata mwaka mzima ndio plant inatembea lakini naskia stamigold walichimba na kukusanya wiki tu wakaanza tembeza plant na mpaka leo wapo. mgodi tena wa serikali sio kama duka la muhindi unaenda asubuhi limefungwa kama tulawaka ilifuata process za kufunga basi hata stamigold siku wakifikia huko watatangaza kwa umma wa watanzania ila kwa sasa mgodi unaendelea kama kawa acha wenye kupika maneno waisome namba kimya kimya
 
Hivi hii Tulawaka si ndio STAMICO ilitoa ripoti juzi kuwa wanajiendesha kwa faida na wameajiri watu 273???

Haya mambo haya bana.
 
Pamoja na wataalam kuishauri Serikali kuhusu mustakabali wa mashapo katika mgodi huo, ushauri wao haukuzingatiwa. Kampuni kubwa kama Barrick kusitisha shughuli zao za uchimbaji si bure, walikwisha ng'amua mashapo ndo yamekwisha na hivyo kuusukuma huo mzigo kwa Shirika. Laiti mngejua na masharti yaliyowekwa kamwe msingeandika kama mlivyofanya hapo juu. Hayo mabilioni wanayodaiwa ni pamoja na sh. Bilioni karibu tatu za kufanya uchimbaji ndani ya hifadhi ya Misitu ya Taifa. Ushauri haukuzingatiwa na matokeo ndo hayo tutayaona.
wewe yaelekea huna taarifa kamili ya huo mgodi wa stamigold ...navyojua mimi ABG ilikuwa kampuni kubwa ambayo ilijiwekea malengo makubwa hivyo kutokana na kiasi kilichobaki wao waliona hakitaendana na gharama zao za uendeshaji lakini kwa mchimbaji wa kati kama stamigold pangemfaa ndio maana wizara ikapachukua na wakaanza sehemu mpya kabisa ndani ya msitu w
Magufuli anatakiwa kuwatumbua STAMICO pamoja na Mameneja wote wa STAMIGOLD. Hao ndio wameuangusha mgodi. Mameneja wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa kawaida kuiba mali za mgodi Ikiwemo dhahabu ambayo tayari imesha zalishwa kwa gharama. Mfano mkubwa kuna dogo alikamatwa na dhahabu ya 70M. Hiyo halamashauri unawalipa mishahara watumishi wangapi? Waioshiri wote kumilikishwa mgodi na waliokuwa watendaji wakubwa pale mgodini watupwe ndani kwa uchunguzi zaidi. Ikibidi wafirisiwe mali na kunyongwa kama enzi za nyerere tuuu. Ujingaaaaa

hayo unayosema yangekuwa kweli sidhani kama kwa uongozi huu wa magufuli kama bado wezi hao wangekuwa wanaendelea taasisi yoyote mtu akitenda kosa si taasisi nzima inatumbuliwa bali muhusika na kwa nilivyosoma kwenye page ya stamigold huko kwenye mtandao wa facebook huyo jamaa alikabidhiwa polisi na dhahabu ilirudi ndani maana kuna cctv kamera so isingewezekana kutoka nayo
 
TBL ilitushinda, tutaweza mining! Hizi Kazi za kusimamia mashirika makubwa kama haya,zingekuwa zinaombwa na MTU binafsi,kupitia usahili,apatikane aliye bora,akiburunda,no mahakamani tu,
hiyo dhana ya migodi kuendeshwa na watu binafsi sijui wazungu sijui lini itaondoka kwa watanzania....stamigold huu ni mwaka wa 3 sasa wanazalisha dhahabu hata GGM na ACACIA hawakuanza tu kwa faida lazima ukubali kuendesha kwa gharama kubwa kwanza ndio badae uanze kuona faida ya unachozalisha. faida pia sio mpaka mauzo tu ajira zilizoko stamigold ukijumlisha na wakandarasi naskia ni 700 naa sasa imagine hiyo PAYE inayolipwa, naskia hadi wanakijiji wanafanya biashara ya kuuza mazao yao mgodini na halmashauri inalipwa kodi sasa kwanini tusi waamini wataalam wakibongo tunaishia kudoubt tu.
 
Mbona waliokula hiyo mifupa ya barick wanajulikana,wanatanua tu.
 
Wasomi watanzania, wengi wao ni wavivu, walafi , mafisadi , wala rushwa na wanapenda kulalamika kuliko kufanya kazi na ndio maana taasisi nyingi za serikali zipo hoi na Kuna miradi mingi ya serikali inafeli, mpaka sometimes nahisi kama tunapenda kutawaliwa. Yaani kwa kifupi tunashindwa kujisimamia kwa sababu ya tabia zetu mbovu.
Pamoja na wataalam kuishauri Serikali kuhusu mustakabali wa mashapo katika mgodi huo, ushauri wao haukuzingatiwa. Kampuni kubwa kama Barrick kusitisha shughuli zao za uchimbaji si bure, walikwisha ng'amua mashapo ndo yamekwisha na hivyo kuusukuma huo mzigo kwa Shirika. Laiti mngejua na masharti yaliyowekwa kamwe msingeandika kama mlivyofanya hapo juu. Hayo mabilioni wanayodaiwa ni pamoja na sh. Bilioni karibu tatu za kufanya uchimbaji ndani ya hifadhi ya Misitu ya Taifa. Ushauri haukuzingatiwa na matokeo ndo hayo tutayaona.
matokeo chanja yatafika tu maana kuchimba ndani ya msitu unalipia kila mti uliokata ndio maana wanapewa SML yaani special mining licence maana wanachimba ndani ya msitu...bilioni 3 kwenye dhahabu ni mauzo kidogo sana watalipa tu mdaiwa hafungwi....
 
tuwe positive na wataalam wetu wa kitanzania na tuwaombee kheri kuliko kuponda kila kinachofanyika kwa kulingaisha na mashirika mengine yaliyokufa sijui ATC, TRL n.k hao stamigold huu ni mwaka wa 3 wapo na naamini wataendelea kuwepo maana wana wataalam wenye experience ndani na nje ya nchi hawatatuangusha
 
Tunabaki kushangaaana!
vulture.jpg
 
STAMICO SASA ITABIDI ITAFUTE MABILIONI YA SHILINGI KUFUKIA MASHIMO KUKIDHI SHERIA YA MIGODI. KAZ KWELI KWELI
 
Magufuli anatakiwa kuwatumbua STAMICO pamoja na Mameneja wote wa STAMIGOLD. Hao ndio wameuangusha mgodi. Mameneja wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa kawaida kuiba mali za mgodi Ikiwemo dhahabu ambayo tayari imesha zalishwa kwa gharama. Mfano mkubwa kuna dogo alikamatwa na dhahabu ya 70M. Hiyo halamashauri unawalipa mishahara watumishi wangapi? Waioshiri wote kumilikishwa mgodi na waliokuwa watendaji wakubwa pale mgodini watupwe ndani kwa uchunguzi zaidi. Ikibidi wafirisiwe mali na kunyongwa kama enzi za nyerere tuuu. Ujingaaaaa

acha uzushi wewe dhahabu haikuibiwa huyo jamaa angetoka vipi na kuna cctv camera???? aliishia kuiacha getini ikarudishwa ndani na yy kupokelewa na polisi na kulala polisi nakesi naskia bado inanguruma....hiyo taarifa ya tukio la kujaribu kuiba dhahabu waliitoa kwenye page yao ya facebook
 
STAMICO SASA ITABIDI ITAFUTE MABILIONI YA SHILINGI KUFUKIA MASHIMO KUKIDHI SHERIA YA MIGODI. KAZ KWELI KWELI

sheria namba ngapi ya mgodi inasema mashimo yafukiwe? mgodi ukishafungwa unaweza kukabidhiwa ukawa hata chuo cha kijeshi mashimo yakatumika hata kwa mazoezi, kama umewahi kupita mgodi wwt mashimo huwa yanaifadhi maji na maji hayo huwa treated yanatumika kwa shughuli zingine ikiwemo kuogea so wataweza kufugia hata samaki
 
ukweli ni kwamba Mayans ski hayo kuna watu walishiba baada ya kupindisha mkataba wa awali
 
Hili lilikuwa lazima litokee ,, Serikali haiwezi kufanya biashara ya Mining hata siku mojo ikapata faida,, Kwenye hii biashara uwajibikaji unahitajika sana na tunavyojua Serikalini uwajibikaji hamna ,ndio maana hili haliwezekani.
huu ni mwaka wa 3 sasa stamigold inajiendesha kwa inachozalisha wala haina bajeti ya serikali kupitia wizara yoyote ...soon wataondoa hito dhana ya kutoamini wataalamu wa kitanzania......
 
Ukweli ni kuwa mwekezaji alituachia 'mahandaki' baada ya dhahabu kuisha!
Atakae kuelewa ni mimi tu, pengine na wengine walio wahi kufanya kazi kwenye mgodi huo wa tulawaka
 
Pamoja na wataalam kuishauri Serikali kuhusu mustakabali wa mashapo katika mgodi huo, ushauri wao haukuzingatiwa. Kampuni kubwa kama Barrick kusitisha shughuli zao za uchimbaji si bure, walikwisha ng'amua mashapo ndo yamekwisha na hivyo kuusukuma huo mzigo kwa Shirika. Laiti mngejua na masharti yaliyowekwa kamwe msingeandika kama mlivyofanya hapo juu. Hayo mabilioni wanayodaiwa ni pamoja na sh. Bilioni karibu tatu za kufanya uchimbaji ndani ya hifadhi ya Misitu ya Taifa. Ushauri haukuzingatiwa na matokeo ndo hayo tutayaona.
Huu ndio ukweli
 
Back
Top Bottom