Mgeni lawama

Mgeni lawama

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
857
Reaction score
2,289
Hivi juzi nilipokea simu kutoka kwa ndugu huko mkoani. Akisema amepata kibarua mkoa nilipo hivyo anaomba aje akae kwangu.

Nilimkaribisha lakini nikamwambia mimi naishi kibachela nyumbani sipiki akasema ye anataka pa ku lala tu.
Alipofika akaanza kusema vyakula vya hotel hivi mara vile bora awe anapika. Akataka anunue gesi nikamwambia acha ntanunua(sikutaka akiondoka aseme aliacha gesi kwangu).

Huyu kijana kapika wiki kama 3 hivi kafulia na mimi sijawah kula akipika.

Sasa analalamika kwa ndugu zake mimi simjali narudi nimekula sijui kama amekula au laa. Kwa kifupi anataka nimlee kama familia na mimi nilishamwambia toka mwanzo nakula kwa mkopo mda mwingine ndio maana sipiki hata kama sina hela nakopa kwa mama ntilie. Huyu nimtimue au nifanyeje?
 
Kama bado upo stage za awali za kujitafuta usiruhu ugeni wa mtu anayetaka hifadhi ya muda fulani
 
Kuishi na ndugu au mtoto wa mtu,mwisho wake hua ni lawama tu,hata umlee kama mtoto mdogo ila tegemea maneno ya kua ulimtesa au aliteseka kwako,

Kama umekubali kuishi na ndugu basi jua kabisa kua hizo lawama hua haziepukiki,

Ni bora ukatae kuishi na ndugu ijulikane kua ulikataa,kuliko hizo story za ndugu kuteswa na wewe au kutomjali,

Huo ndio ushauri wangu,
The rest it's up to you.
 
Hivi juzi nilipokea simu kutoka kwa ndugu huko mkoani. Akisema amepata kibarua mkoa nilipo hivyo anaomba aje akae kwangu.

Nilimkaribisha lakini nikamwambia mimi naishi kibachela nyumbani sipiki akasema ye anataka pa ku lala tu.
Alipofika akaanza kusema vyakula vya hotel hivi mara vile bora awe anapika. Akataka anunue gesi nikamwambia acha ntanunua(sikutaka akiondoka aseme aliacha gesi kwangu).

Huyu kijana kapika wiki kama 3 hivi kafulia na mimi sijawah kula akipika.

Sasa analalamika kwa ndugu zake mimi simjali narudi nimekula sijui kama amekula au laa. Kwa kifupi anataka nimlee kama familia na mimi nilishamwambia toka mwanzo nakula kwa mkopo mda mwingine ndio maana sipiki hata kama sina hela nakopa kwa mama ntilie. Huyu nimtimue au nifanyeje?
Mkumbushe kua aliomba sehema ya kulala tu kama mwanzo usisahau kumwambia ye ni boya
 
Umenikumbusha hili shairi:-

Mgeni siku ya kwanza
mpe mchele na panza;
mtilie kifuani,
mkaribishe mgeni.

Mgeni siku ya pili
mpe ziwa na samli;
mahaba yakizidia,
mzidishie mgeni.

Mgeni siku ya tatu
jumbani hamuna kitu.
mna zibaba zitatu,
pika ule na mgeni.

Mgeni siku ya nne
mpe jembe akalime.
akirudi muagane,
aende kwao mgeni,

Mgeni siku ya tano
mwembamba kama sindano,
hayeshi masengenyano,
asengenywayo mgeni.

Mgeni siku ya sita;
mkila mnajificha;
mwaingia vipembeni
afichwaye ni mgeni.

Mgeni siku ya saba,
si mgeni ana baa.
hata moto mapaani
katia yeye mgeni,

Mgeni siku ya nane;
njoo ndani tuonane.
atapotokea nje,
natuagane mgeni,

Mgeni siku ya kenda;
enenda mwana kwenenda!
usirudi nyuma nenda,
utokomee mgeni.

Mgeni siku ya kumi
kwa mateke na magumi.
hapana afukuzwaye,
Ila ni yeye mgeni.
 
Mkuu usimtimue, we mwambie kuanzia mwezi ujao tutaanza kuchanga Kodi, atasepa mwenyewe.
 
Hivi juzi nilipokea simu kutoka kwa ndugu huko mkoani. Akisema amepata kibarua mkoa nilipo hivyo anaomba aje akae kwangu.

Nilimkaribisha lakini nikamwambia mimi naishi kibachela nyumbani sipiki akasema ye anataka pa ku lala tu.
Alipofika akaanza kusema vyakula vya hotel hivi mara vile bora awe anapika. Akataka anunue gesi nikamwambia acha ntanunua(sikutaka akiondoka aseme aliacha gesi kwangu).

Huyu kijana kapika wiki kama 3 hivi kafulia na mimi sijawah kula akipika.

Sasa analalamika kwa ndugu zake mimi simjali narudi nimekula sijui kama amekula au laa. Kwa kifupi anataka nimlee kama familia na mimi nilishamwambia toka mwanzo nakula kwa mkopo mda mwingine ndio maana sipiki hata kama sina hela nakopa kwa mama ntilie. Huyu nimtimue au nifanyeje?
usiku akilala mzamishie zaga afu asubuhi muombe msamaha mwambie bahati mbaya zaga liliteleza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom