Mgeni huku jamani!!

Karibu sana zingatia sheria zote za hapa
-Peleka uzi husika kwenye jukwaa husika, mfano swala la siasa hautakiwi kulipeleka kwenye jukwaa la mahusiano au jukwaa la hoja na habari mchanganyiko ili upate wachangiaji.
-Hairuhusiwi matusi (tafsida inaruhusiwa) kumdhalilisha au kumbagua member mwenzio, kufanya hivyo hupelekea ban.
-Marufuku kuleta mazungumzo uliyofanya pm jukwaani hii hupelekea ban.
-Ukihisi umemjua mtu anayetumia fake id, usiliseme hilo pale pale mfuate pm, kumtaja hapo hapo hupelekea ban.
-Marufuku kuandika kama upo FB au kufupisha vitu bila sababu mfano 'S' kuiandika 'X' hivyo sasa kua xaxa, au 'tu' kuiandika 'tyu'. Utanikera na utatukera wengi.
-Kuanzia leo nakubatiza jina la Mkuu, ukiitwa mkuu usishangae, sawa mkuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom