Mgeja ni mradi wa mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeja ni mradi wa mafisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  CCM wamvaa Mgeja


  na Bakari Kimwanga


  [​IMG] WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wamemjia juu mwenyekiti wao wa mkoa, Khamis Mgeja, wakisema anatumiwa na kundi la mafisadi kujinufaisha kwa maslahi yake binafsi. Katika taarifa yao waliyoituma kwenye vyombo vya habari, wanachama hao walisema wanashangazwa na hatua ya kiongozi huyo kuanzisha malumbano na viongozi wa chama na serikali.
  Wanachama hao walikuwa wakirejea hatua ya mwenyekiti wao huyo ya kuanzisha malumbano na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela.
  Wanachama hao walisema kitendo kinachofanywa na Mgeja ni aibu na fedheha kwa chama kwani anachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kuitisha kikao cha kufanya tathmini ya kina kwa nini kata na majimbo mengi katika mkoa wake yamekwenda upinzani.
  Taarifa hiyo iliyosainiwa na Juma Maganga kwa niaba ya wanachama wenzake toka wilayani Kahama alisema itakuwa vema mwenyekiti huyo akatangaza kujiuzulu uenyekiti wa CCM wa mkoa huo.
  Hata hivyo Maganga alisema kuna umuhimu kwa viongozi wa CCM Taifa kumtafari kwa kina Mgeja na kumuuliza nini nia yake.
  Hivi karibuni Mgeja alinukuliwa na vyombo vya habari kuhusu azma yake ya kuwasilisha hoja binafsi katika kikao cha Halamshauri Kuu ya CCM, juu ya kauli ya Waziri Sitta, kuhusu msimamo wake dhidi ya ushindi wa kampuni ya kufua Umeme ya Dowans kulipwa na Tanesco sh 185 bilioni.
  Hali hiyo imeibua malumbano na kufufua kile kinachoitwa pande mbili zinazohasimiana ndani ya CCM.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Mgeja hana ubavu wa kumvaa Mzee wetu Sitta kama hana mafisadi kumpa tafu.........................hili lipo wazi kabisa.............lakini for how long?
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Mgeja darasa la saba atakaa meza moja na mzee six?

  Nazi haishindani na Jiwe!!

  Chana NaE!
   
Loading...